Bashiru aanza ziara Kigoma, Zitto Kabwe azuiwa kufanya mkutano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Wakati mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akizuiwa kufanya mkutano wa hadhara na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma leo Ijumaa Januari 17, 2020, katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameanza ziara ya siku tatu mkoani humo.

Polisi mkoani Kigoma kupitia barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, M.R Mayunga yenye kumbukumbu namba KIG/A.24/60/VOL.1/114 ya Januari 16, 2020, wamemzuia Zitto kufanya mkutano wake leo kwa sababu za usalama na taarifa za kiintelijensia.

Akizungumza na Mwananchi leo katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema baada ya kuwasili mjini Kigoma, Dk Bashiru ataelekea eneo la Kazuramimba Wilaya ya Uvinza kwa ajili ya vikao vya ndani na viongozi wa chama na jumuiya zake.

“Jumamosi Januari 18, 2020 Katibu mkuu atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani na kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miaka minne katika jimbo la Kigoma Kaskazini inayoongozwa na Peter Serukamba (CCM),” amesema Vyohoroka.

Kwa mujibu wa katibu huyo, Jumapili Januari 19, 2020, Dk Bashiru aliyetokea katika ziara mkoani Tanga na kuwapokea madiwani wanane wa CUF waliojiunga CCM, atakuwa na kikao cha ndani na mabalozi wa CCM na viongozi wa chama hicho tawala na jumuiya zake.

Akizungumzia kuzuiwa kwa mkutano wa Zitto, katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema sababu zilizotajwa na polisi hazina mashiko na zinalenga kumzuia Zitto asitekeleze majukumu yake halali ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Shaibu amesema mkutano huo ulipangwa kufanyika katika viwanja vya Mwanga Center manispaa ya Kigoma Ujiji.

Chanzo: Mwananchi

Zaidi, soma: News Alert: - Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe
 
Hivi ni demokrasia gani mbunge anazuiwa na watu wasiochaguliwa na katibu asiye chaguliwa na wananchi ndiye anaruhusiwa. Tanzania bado sana inasikitisha mpaka leo jamani.
 
Inawezekana polisi Kigoma hawana resources za kutosha kuhakikisha usalama wa mikutano miwili kwa wakati mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Sisi tupo Kigoma na Leo Zitto Kabwe alikuwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani. Huwa mambo ya Jeshi la Police ni kuhakikisha madhara ovu kwa Binadamu hayatokei kukiwa na dalili labda iwe kwa Bahati Mbaya. Zitto Kabwe anajua hali ilivyokuwa tete. Shaibu aende kumuuliza Kaila kilichopo Kigoma.

Sasa hivi Wanaandaa vijana wa ACT, amepatiwa Mafuta ya kujaza kwenye pikipiki na kupewa 10,000 kila mmoja eti Wajifanye Zitto Kabwe anaonewa Wakati ameokolewa.

Upinzani wanaona umuhimu wa Jeshi la Police baada ya kuokolewa. Police Kigom wamefanya kazi nzuri. Siyo kwamba Zitto eti Kigoma ana Nguvu kisiasa, ila angedhulika wangelaumiwa Jeshi la Police na kupata cha kuichafua Serikali. 😎😎😎😎😎😎
 
Ni vyema na haki ya Bashiru kukagua kazi iliyofanywa na serikali yake,maana ikifanya vibaya haitachaguliwa tena.

macson
 
Zito asitafute sababu yeye ni mbunge alipaswa kuishi kigoma na kufanya mikutano kila siku bila tatizo ila yeye anaishi kinondoni na kuzunguka hapa mjini amesikia dk bashiru yupo kule anatafuta sababu eti alipanga kufanya mikutano

Poor you zito

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akafanyie mkutano Twitaa, fesibuku na intagaramu kama alivyozoea. Kaona Dr. Bashiru katangaza ziara ndipo na yeye anaweka mikutano. Siku zote alikuwa wapi?

Queen Esther
 
NTWA MWIKEMO, Acha upuuzi wewe mdudu. Ni bora ukae kimya kuliko kuongea upuuzi halafu watu watoe matusi, wapigwe ban.

Uchaguzi wa 2020 CCM ndio mtajua jinsi gani raia wamewachoka.
 
Wewe ndie msemaji wa jeshi la polisi? Umeyajuwaje yote haya ?
Kwani kwenu hakuna somo la Polisi Jami au Mrundi wewe. Hapa Tanzania tuna Police Jamii na ndiyo maana tunaelewa na kuzingatia ushirikiano na Jeshi la Police Tanzania 😆😆😆😆😆😆
 
Wakati mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akizuiwa kufanya mkutano wa hadhara na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma leo Ijumaa Januari 17, 2020, katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameanza ziara ya siku tatu mkoani humo.

Polisi mkoani Kigoma kupitia barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, M.R Mayunga yenye kumbukumbu namba KIG/A.24/60/VOL.1/114 ya Januari 16, 2020, wamemzuia Zitto kufanya mkutano wake leo kwa sababu za usalama na taarifa za kiintelijensia.

Akizungumza na Mwananchi leo katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema baada ya kuwasili mjini Kigoma, Dk Bashiru ataelekea eneo la Kazuramimba Wilaya ya Uvinza kwa ajili ya vikao vya ndani na viongozi wa chama na jumuiya zake.

“Jumamosi Januari 18, 2020 Katibu mkuu atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani na kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miaka minne katika jimbo la Kigoma Kaskazini inayoongozwa na Peter Serukamba (CCM),” amesema Vyohoroka.

Kwa mujibu wa katibu huyo, Jumapili Januari 19, 2020, Dk Bashiru aliyetokea katika ziara mkoani Tanga na kuwapokea madiwani wanane wa CUF waliojiunga CCM, atakuwa na kikao cha ndani na mabalozi wa CCM na viongozi wa chama hicho tawala na jumuiya zake.

Akizungumzia kuzuiwa kwa mkutano wa Zitto, katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema sababu zilizotajwa na polisi hazina mashiko na zinalenga kumzuia Zitto asitekeleze majukumu yake halali ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Shaibu amesema mkutano huo ulipangwa kufanyika katika viwanja vya Mwanga Center manispaa ya Kigoma Ujiji.

Chanzo: Mwananchi

Zaidi, soma: News Alert: - Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe
Nchi imefika mahali patamu sana ! sababu zote zipo

FB_IMG_1570952637609.jpg
 
Sis kwetu hatukusomeshwa darasani kuhusu hio polisi jamii. Ila tumejifunza uraiani jinsi hao polisi wanavyoinyanyasa jamii!
Kwani Zitto Kabwe anavyowanyonya Madiwani na kuwalazimisha wakubaliane na Mawazo yake ni haki na haki ya aina hiyo umejifunzia huko kuwaahidi Madiwani kuwapatia 10% kutoka kwenye miradi mikubwa ya Serikali. Pia hata unavyoonesha ni Msukule wa siasa hujui kinachoendelea.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom