[Bashiri]: Sam Mahela kumfuata Godwin Gondwe

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,085
Kufuatia huyu Kaka'etu aliyepata heshima kubwa sana kwenye tasnia ya Uandishi wa Habari na Utangazaji nchini kupitia IPP Media,

Ambaye pia ni mwalimu wa fani hiyo Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam,
mwenye elimu ya kiwango cha master's degree kwenye Mawasiliano ya Umma,

Pia ni nguli wa voice over kwenye matangazo mbalimbali yakiwemo ya kampuni ya simu ya Airtel
wa kuitwa #Godwin_Gondwe (G.G),

Ambaye historia yake inabainisha kuwa alishawahi kuwa muhudumu wa grocery(enzi hizo),
na kuwa mfanya usafi wa vyoo (hospitali ya Bugando huko Mwanza )
kabla ya kuingia kwenye tasnia ya habari
Kuteulia kuwa mkuu wa wilaya ya Handeni, Tanga,

(Ingawa yeye si mwanahabari wa kwanza kuteuliwa nafasi kama hiyo)
Nimeamua KUBETI(kubashiri) kuwa na huyu Kaka'etu mwingine huyu wa ITV wa kipindi cha #DAKIKA_45 huyu wa kuitwa #Sam_Mahela
muda si mrefu anaweza kuja kufikiriwa kwenye kitengo fulani nyeti sometime to come.

ANGALIZO:
Hapa mimi NIMEBETI(nimebashiri) kwa mtazamo wangu tu
kama mwananchi wa kawaida,
Bashiri hii wala haiendani na uhalisia au mikakati yoyote.

_____
Kwa mantiki hii
hata huyu kaka'angu #Adam_Mchomvu huyu naye akiamua kukaza
Wakubwa wanaweza 'kumwona' au japo kumfikiria kwenye baadhi ya kada kwa mbaaaaaaaaliiiiiii!!!!!.

NIMEMALIZA!
 
Hahaha....hapo na Mimi nacopy mkeka wako na sidhani kama utachanika,kwasababu anatoka ITV ndio maana nimeamua kukusupport.
Reference
Betty mkwasa
Makungu
Godwin Gondwe
Emmanuel Buhohela
etc
 
Hahaha....hapo na Mimi nacopy mkeka wako na sidhani kama utachanika,kwasababu anatoka ITV ndio maana nimeamua kukusupport.
Reference
Betty mkwasa
Makungu
Godwin Gondwe
Emmanuel Buhohela
etc
Buhohela yuko wapi?
 
Kwa uendeshaji ule wa kipindi hasa dk 45 anaweza akafikiriwa japo umewasahau wale wa mawingu waliopigiwa simu kabisa na mkulu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom