mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,306
- 6,514
Tanzania na Afrika yote, wanasiasa wanaofaa ni wale wenye chembechembe za unafiki mithili ya aliyekuwa Rais wa Zambia, marehemu Levy Mwanawasa. Unakuwa mtetezi wa usiyoyapenda.
Afrika wanasiasa wenye kufanikiwa ni wale wenye kujipendekeza kwa viongozi wao kwenye vyama, wanakuwa watiifu hata kwa mambo ambayo wao wenyewe yanawauma. Wananyamaza na kuvumilia. Wanaficha kucha.
Tanzania katika mkondo wa Afrika, wanasiasa wakosoaji hawafai na mara nyingi huwa hawapewi nafasi. Afrika, hata uwe na uwezo mkubwa kiasi gani, kama mdomo wako ni mkubwa na unawasema viongozi au kuukosoa mfumo lazima udidimizwe.
Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), Afrika Kusini, Julius Malema, alikuwa kijana pendwa wa Rais wa nchi hiyo aliye pia Rais wa Chama cha African National Congress (ANC), Jacob Zuma.
Nyota ya Malema iling’ara vizuri mno akiwa kiongozi wa Jumuiya ya Vijana ya ANC. Tatizo lilijitokeza pale Malema alipojifanya ana mdomo mkubwa wa kumsema Zuma. Alisimamishwa uongozi kisha akatimuliwa uanachama, ikabidi aanzishe chama chake.
Kama Malema, tabia ya kukosoa viongozi au mfumo ndani ya vyama, unawafanya wanasiasa wa Tanzania, Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wawe hawafai katika siasa za Afrika.
Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo pamoja na swahiba wake, mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na mshauri wa ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, siasa za Tanzania na Afrika yote haziwafai. Maana si waona jambo wakakaa kimya.
Tangu Bashe alipotokeza na kuweka wazi hisia na mtazamo wake kuhusu jinsi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alivyokatwa jina katika mchakato wa kuomba tiketi ya CCM kuwania urais mwaka jana, anashambuliwa. Bashe anaitwa mbunge wa Chadema mwenye tiketi ya CCM.
Kosa la Bashe ni kutoa mawazo yake. Afrika wanachama hawatakiwi kuwa na mawazo hasi kwenye vyama vyao kisha wakayaweka wazi. Wanatakiwa wanyamaze kama hawayaoni. Siasa za Afrika hulea wanasiasa wenye rangi mbili.
Kile anachokitetea hadharani sicho kilichopo kwenye moyo wake. Wanahitaji Bashe aseme Lowassa alitendewa haki hata kama moyoni mwake kuna ukweli tofauti. Afrika, watu huamini kuwa mwanachama kukosoa chama chake tayari anakuwa mfuasi wa chama kingine.
Bashe alisema yeye na Lowassa hawana uhusiano tena wa kisiasa baada ya mbunge huyo wa zamani wa Monduli kuhamia Chadema. Hata hivyo, anaona kwa afya ya chama yapo mambo ambayo Lowassa alifanyiwa hayakuwa sawa. Akasema si Lowassa tu, wengi wameonewa.
Maneno hayo yanamgharimu zaidi Bashe kwa sababu alikuwa mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya Lowassa CCM, ambayo ilivuma kwa umaarufu wake kupitia jina la Safari ya Matumaini.
Wanatakiwa akina Mutharika
Mwanawasa anafanana sana na aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika. Wote Mungu aliwachukua wakiwa madarakani wakiongoza nchi zao. Zaidi, waliingizwa madarakani na vyama vilivyokuwa vinatawala.
Upacha wa Mutharika na Mwanawasa ni jinsi ambavyo waliweza kucheza mizungu ya siasa za Afrika. Walikuwa wanyenyekevu mno kwa viongozi wao hata kuaminika kuwa kama wataachiwa madaraka basi watawalinda wakuu wao.
Mutharika akiwa mwanachama wa Chama cha United Democratic Front (UDF), alionesha utiifu wa hali ya juu kwa mwasisi na mwenyekiti wa chama hicho, Bakili Muluzi ambaye alikuwa Rais wa Malawi kuanzia mwaka 1994 mpaka 2004.
Uadilifu mdogo wa viongozi wengi Afrika, husababisha wanapotaka kuondoka madarakani wahangaike kutafuta warithi ambao watawalinda, wengine wakichezea Katiba na kujiongezea muda wa kubaki madarakani.
Muluzi baada ya kushindwa jaribio la kupindisha Katiba ilibidi aone njia pekee ni kuweka mrithi atakayemlinda akishatoka madarakani. Akamuona Mutharika ni mtu sahihi kwa namna walivyoelewana.
Hakujua kuwa unyenyekevu wa Mutharika ulikuwa ni wa kinafiki kama yalivyo mahitaji ya siasa za Afrika. Mutharika alikuwa na mengi yasiyompendeza kwa Muluzi mpaka kwenye chama cha UDF.
Mutharika alibaki mkimya, Muluzi akampigania kupata tiketi ya UDF kuwa mgombea urais na alimfanyia kampeni ya nguvu akawa Rais wa Malawi. Baada ya Mutharika kushinda ndiyo hapo akafungua kucha zake.
Unyenyekevu wa Mutharika kwa Muluzi na UDF uliisha mara tu alipoapishwa kuwa Rais wa Malawi. Alianza kumshughulikia Muluzi kwa tuhuma za ufisadi. Kwa vile Muluzi ndiye alikuwa kiongozi wa UDF, Mutharika alianzisha chama kingine cha Democratic Progressive Party (DPP).
Baada ya kuanzisha chama chake aliendelea kuwanyoosha watu wa UDF akiwemo Muluzi mpaka alipofikwa na mauti mwaka 2012 akiwa ameshaiongoza Malawi kwa miaka saba na miezi 11 kuanzia Mei 2004.
Hali kama hiyo ilitokea Zambia. Mwanawasa alikuwa mwaminifu asiyempinga mtangulizi wake na aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Movement Multi-Party Democracy (MMD), Fredrick Chiluba.
Muda wa Chiluba kuondoka madarakani ulipowadia na baada ya kushindwa jaribio lake la kuisigina Katiba ili aendelee kutawala, alimwona Mwanawasa ni mtu sahihi kumwachia madaraka, kwani angemlinda.
Chiluba alimpigania Mwanawasa ndani ya MMD kisha akamfanyia kampeni ya nguvu mpaka akachaguliwa kuwa Rais wa tatu wa Zambia. Ongezea upacha mwingine wa Mutharika na Mwanawasa kuwa wote ni marais wa tatu wa nchi zao baada ya mamlaka ya kikoloni, Uingereza.
Mwanawasa baada ya kuapa kuiongoza Zambia alianza kumshughulikia Chiluba. Ni hapo ndipo watu wakastaajabu. Kumbe Mwanawasa alikuwa mpole kwa Chiluba kuficha kucha tu.
Kimsingi siasa za Afrika zinataka akina Mwanawasa na Mutharika. Watu ambao wanaweza kujifanya wapole wakichekelea kila kinachofanyika bila kukosoa, wakisubiri waaminiwe wapewe mamlaka ndipo wachanue makucha.
Siasa za Afrika hazitaki watu ambao hawawezi kutabasamu usoni hata kama mioyo yao imenuna. Haitaki watu kama Bashe wenye kuamini kuwa unaweza kumkosoa kiongozi au mfumo kwenye chama kisha ukabaki mwanachama mtiifu.
Siku zote ukijifanya unajua kukosoa na kupigania unyoofu ndani ya chama utajikuta unanyooshwa wewe. Wengi tu walijikuta wakihama vyama vyao au ndoto zao za kisiasa kutoweka baada ya kukutana na misukosuko mikubwa kutoka kwa wakubwa wao.
Zitto, Kitila walishindwa
Hivi sasa Malema anabaki na kumbukumbu kuwa alishiriki harakati nzito za kumuingiza Zuma madarakani, ikiwa ni baada ya kumchachafya kila upande, Rais wa pili wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.
Ni kama ambavyo Zitto na Profesa Kitila wanavyokumbuka kuwa mchango wao ni mkubwa uliokifanya Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani leo hii. Kasoro kubwa ni kuwa Zitto na Kitila walishindwa siasa za Kiafrika, wakajipambanua kama wakosoaji.
Kama Zitto angebaki mnyenyekevu kwa mfumo ndani ya Chadema, vilevile kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, pengine sasa hivi angekuwa ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho, hasa baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kujiuzulu na kustaafu siasa mwaka jana.
Ingewezekana vipi Dk Vincent Mashinji apewe ukatibu mkuu kumruka Zitto? Hata hivyo, hayo ndiyo matokeo ya kuzishindwa siasa za Afrika. Zitto alikuwa mkosoaji wa wazi kuhusu mambo mengi Chadema. Gharama yake ikawa kubwa.
Profesa Kitila na uwezo wake mkubwa kitaaluma alipaswa kuvumilia maisha ya ukimya. Hata kama alimwona Mbowe hafai, alipaswa kumsifu na kumtetea. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kupanda madaraja ya kisiasa Afrika, maana inafahamika kuwa wakubwa Afrika huwa hawakosei.
Matokeo ya kushindwa siasa za Afrika ndiyo ambayo yamewafanya Zitto na Kitila wawe ACT-Wazalendo leo hii, bega kwa bega na swahiba wao, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Hali hiyo inatia shaka majaliwa ya Bashe, maana viongozi wa vyama vya siasa Afrika wanafanana, si wepesi kukubali kukosolewa. Hulka hii si kwa viongozi wa vyama vilivyopo madarakani tu, hata vile vya upinzani, maana wote baba na mama ni mmoja.
Kama ambavyo Bashe anashambuliwa kwa kuitwa mbunge wa CCM mwenye tiketi ya Chadema, ni suala la kujiuliza; kiongozi gani CCM anaweza kuvumilia ukosoaji wa Bashe kuwa Lowassa alionewa? Ukizingatia Lowassa huyo ndiye anayeinyima usingizi CCM.
CHANZO: MAANDISHI GENIUS