Bashe, Zitto ni wanasiasa wasiofaa Afrika

mcubic

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Messages
10,235
Likes
4,404
Points
280
mcubic

mcubic

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2011
10,235 4,404 280
Tanzania na Afrika yote, wanasiasa wanaofaa ni wale wenye chembechembe za unafiki mithili ya aliyekuwa Rais wa Zambia, marehemu Levy Mwanawasa. Unakuwa mtetezi wa usiyoyapenda.

Afrika wanasiasa wenye kufanikiwa ni wale wenye kujipendekeza kwa viongozi wao kwenye vyama, wanakuwa watiifu hata kwa mambo ambayo wao wenyewe yanawauma. Wananyamaza na kuvumilia. Wanaficha kucha.

Tanzania katika mkondo wa Afrika, wanasiasa wakosoaji hawafai na mara nyingi huwa hawapewi nafasi. Afrika, hata uwe na uwezo mkubwa kiasi gani, kama mdomo wako ni mkubwa na unawasema viongozi au kuukosoa mfumo lazima udidimizwe.

Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), Afrika Kusini, Julius Malema, alikuwa kijana pendwa wa Rais wa nchi hiyo aliye pia Rais wa Chama cha African National Congress (ANC), Jacob Zuma.

Nyota ya Malema iling’ara vizuri mno akiwa kiongozi wa Jumuiya ya Vijana ya ANC. Tatizo lilijitokeza pale Malema alipojifanya ana mdomo mkubwa wa kumsema Zuma. Alisimamishwa uongozi kisha akatimuliwa uanachama, ikabidi aanzishe chama chake.

Kama Malema, tabia ya kukosoa viongozi au mfumo ndani ya vyama, unawafanya wanasiasa wa Tanzania, Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wawe hawafai katika siasa za Afrika.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo pamoja na swahiba wake, mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam na mshauri wa ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, siasa za Tanzania na Afrika yote haziwafai. Maana si waona jambo wakakaa kimya.

Tangu Bashe alipotokeza na kuweka wazi hisia na mtazamo wake kuhusu jinsi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alivyokatwa jina katika mchakato wa kuomba tiketi ya CCM kuwania urais mwaka jana, anashambuliwa. Bashe anaitwa mbunge wa Chadema mwenye tiketi ya CCM.

Kosa la Bashe ni kutoa mawazo yake. Afrika wanachama hawatakiwi kuwa na mawazo hasi kwenye vyama vyao kisha wakayaweka wazi. Wanatakiwa wanyamaze kama hawayaoni. Siasa za Afrika hulea wanasiasa wenye rangi mbili.

Kile anachokitetea hadharani sicho kilichopo kwenye moyo wake. Wanahitaji Bashe aseme Lowassa alitendewa haki hata kama moyoni mwake kuna ukweli tofauti. Afrika, watu huamini kuwa mwanachama kukosoa chama chake tayari anakuwa mfuasi wa chama kingine.

Bashe alisema yeye na Lowassa hawana uhusiano tena wa kisiasa baada ya mbunge huyo wa zamani wa Monduli kuhamia Chadema. Hata hivyo, anaona kwa afya ya chama yapo mambo ambayo Lowassa alifanyiwa hayakuwa sawa. Akasema si Lowassa tu, wengi wameonewa.

Maneno hayo yanamgharimu zaidi Bashe kwa sababu alikuwa mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya Lowassa CCM, ambayo ilivuma kwa umaarufu wake kupitia jina la Safari ya Matumaini.

Wanatakiwa akina Mutharika

Mwanawasa anafanana sana na aliyekuwa Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika. Wote Mungu aliwachukua wakiwa madarakani wakiongoza nchi zao. Zaidi, waliingizwa madarakani na vyama vilivyokuwa vinatawala.

Upacha wa Mutharika na Mwanawasa ni jinsi ambavyo waliweza kucheza mizungu ya siasa za Afrika. Walikuwa wanyenyekevu mno kwa viongozi wao hata kuaminika kuwa kama wataachiwa madaraka basi watawalinda wakuu wao.

Mutharika akiwa mwanachama wa Chama cha United Democratic Front (UDF), alionesha utiifu wa hali ya juu kwa mwasisi na mwenyekiti wa chama hicho, Bakili Muluzi ambaye alikuwa Rais wa Malawi kuanzia mwaka 1994 mpaka 2004.

Uadilifu mdogo wa viongozi wengi Afrika, husababisha wanapotaka kuondoka madarakani wahangaike kutafuta warithi ambao watawalinda, wengine wakichezea Katiba na kujiongezea muda wa kubaki madarakani.

Muluzi baada ya kushindwa jaribio la kupindisha Katiba ilibidi aone njia pekee ni kuweka mrithi atakayemlinda akishatoka madarakani. Akamuona Mutharika ni mtu sahihi kwa namna walivyoelewana.

Hakujua kuwa unyenyekevu wa Mutharika ulikuwa ni wa kinafiki kama yalivyo mahitaji ya siasa za Afrika. Mutharika alikuwa na mengi yasiyompendeza kwa Muluzi mpaka kwenye chama cha UDF.

Mutharika alibaki mkimya, Muluzi akampigania kupata tiketi ya UDF kuwa mgombea urais na alimfanyia kampeni ya nguvu akawa Rais wa Malawi. Baada ya Mutharika kushinda ndiyo hapo akafungua kucha zake.

Unyenyekevu wa Mutharika kwa Muluzi na UDF uliisha mara tu alipoapishwa kuwa Rais wa Malawi. Alianza kumshughulikia Muluzi kwa tuhuma za ufisadi. Kwa vile Muluzi ndiye alikuwa kiongozi wa UDF, Mutharika alianzisha chama kingine cha Democratic Progressive Party (DPP).

Baada ya kuanzisha chama chake aliendelea kuwanyoosha watu wa UDF akiwemo Muluzi mpaka alipofikwa na mauti mwaka 2012 akiwa ameshaiongoza Malawi kwa miaka saba na miezi 11 kuanzia Mei 2004.

Hali kama hiyo ilitokea Zambia. Mwanawasa alikuwa mwaminifu asiyempinga mtangulizi wake na aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Movement Multi-Party Democracy (MMD), Fredrick Chiluba.

Muda wa Chiluba kuondoka madarakani ulipowadia na baada ya kushindwa jaribio lake la kuisigina Katiba ili aendelee kutawala, alimwona Mwanawasa ni mtu sahihi kumwachia madaraka, kwani angemlinda.

Chiluba alimpigania Mwanawasa ndani ya MMD kisha akamfanyia kampeni ya nguvu mpaka akachaguliwa kuwa Rais wa tatu wa Zambia. Ongezea upacha mwingine wa Mutharika na Mwanawasa kuwa wote ni marais wa tatu wa nchi zao baada ya mamlaka ya kikoloni, Uingereza.

Mwanawasa baada ya kuapa kuiongoza Zambia alianza kumshughulikia Chiluba. Ni hapo ndipo watu wakastaajabu. Kumbe Mwanawasa alikuwa mpole kwa Chiluba kuficha kucha tu.

Kimsingi siasa za Afrika zinataka akina Mwanawasa na Mutharika. Watu ambao wanaweza kujifanya wapole wakichekelea kila kinachofanyika bila kukosoa, wakisubiri waaminiwe wapewe mamlaka ndipo wachanue makucha.

Siasa za Afrika hazitaki watu ambao hawawezi kutabasamu usoni hata kama mioyo yao imenuna. Haitaki watu kama Bashe wenye kuamini kuwa unaweza kumkosoa kiongozi au mfumo kwenye chama kisha ukabaki mwanachama mtiifu.

Siku zote ukijifanya unajua kukosoa na kupigania unyoofu ndani ya chama utajikuta unanyooshwa wewe. Wengi tu walijikuta wakihama vyama vyao au ndoto zao za kisiasa kutoweka baada ya kukutana na misukosuko mikubwa kutoka kwa wakubwa wao.

Zitto, Kitila walishindwa

Hivi sasa Malema anabaki na kumbukumbu kuwa alishiriki harakati nzito za kumuingiza Zuma madarakani, ikiwa ni baada ya kumchachafya kila upande, Rais wa pili wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

Ni kama ambavyo Zitto na Profesa Kitila wanavyokumbuka kuwa mchango wao ni mkubwa uliokifanya Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani leo hii. Kasoro kubwa ni kuwa Zitto na Kitila walishindwa siasa za Kiafrika, wakajipambanua kama wakosoaji.

Kama Zitto angebaki mnyenyekevu kwa mfumo ndani ya Chadema, vilevile kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, pengine sasa hivi angekuwa ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho, hasa baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa kujiuzulu na kustaafu siasa mwaka jana.

Ingewezekana vipi Dk Vincent Mashinji apewe ukatibu mkuu kumruka Zitto? Hata hivyo, hayo ndiyo matokeo ya kuzishindwa siasa za Afrika. Zitto alikuwa mkosoaji wa wazi kuhusu mambo mengi Chadema. Gharama yake ikawa kubwa.

Profesa Kitila na uwezo wake mkubwa kitaaluma alipaswa kuvumilia maisha ya ukimya. Hata kama alimwona Mbowe hafai, alipaswa kumsifu na kumtetea. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kupanda madaraja ya kisiasa Afrika, maana inafahamika kuwa wakubwa Afrika huwa hawakosei.

Matokeo ya kushindwa siasa za Afrika ndiyo ambayo yamewafanya Zitto na Kitila wawe ACT-Wazalendo leo hii, bega kwa bega na swahiba wao, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Hali hiyo inatia shaka majaliwa ya Bashe, maana viongozi wa vyama vya siasa Afrika wanafanana, si wepesi kukubali kukosolewa. Hulka hii si kwa viongozi wa vyama vilivyopo madarakani tu, hata vile vya upinzani, maana wote baba na mama ni mmoja.

Kama ambavyo Bashe anashambuliwa kwa kuitwa mbunge wa CCM mwenye tiketi ya Chadema, ni suala la kujiuliza; kiongozi gani CCM anaweza kuvumilia ukosoaji wa Bashe kuwa Lowassa alionewa? Ukizingatia Lowassa huyo ndiye anayeinyima usingizi CCM.

CHANZO: MAANDISHI GENIUS
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,214
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,214 280
Kazi kweli
 
Lituye

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
653
Likes
879
Points
180
Lituye

Lituye

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
653 879 180
Kuna tofauti kubwa kati ya ukosoaji na Usaliti lazima ujue ndugu. Mkosoaji huwa na lengo la kujenga na hukosoa ktk mazingira sahihi.

Zito, Kitila na Mwigamba hawakuwa wakosoaji walikuwa na Ajenda zao walizo tumwa.

Ndio mana wakaunda chama Chao ambacho Nguvu kubwa ilikuwa kuvishambulia vyama vya upinzani badala ya ccm.

Lakini kwa maelezo yako unamaanisha sasa hata Lipumba ameonewa na viongozi Wa CUF kwa kumfukuza uanachama.
 
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
6,730
Likes
1,593
Points
280
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
6,730 1,593 280

Bashe anafanya kazi ya lowassa ccm. Itamgharimu wanaccm hawatamvumilia. Uamuzi wa kumkata edo ni mojawapo ya hatua muhimu wanaccm walifanya. Ikiwa mtu anapinga ccm sio nyumbani kwake. Kuepusha shida bora kufunga virago mapema.
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,513
Likes
2,006
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,513 2,006 280
Kofi Olomide amewahi kuimba "Lokuta eyaka na ascenseur,kasi verite eyei na escalier mpe ekomi" akiwa na maana kuwa "Uongo siku zote hutumia lifti kupanda ghorofani ilhali ukweli hutumia ngazi japo hufika".

Uliowataja hapo juu ni watumia ngazi kupanda ghorofani hivyo kamwe hawamhofii anayetumia lifti.Ni baadhi ya watu makini,weledi na wenye upeo mpana kuhusu SIASA hususan za sie watu weusi.Sie wengine ni mashabiki tu na hakuna tunalolisimamia kwa uadilifu zaidi tu ni kufuata upepo unapoelekea.

Wanakosoa pasipoeleweka,Hawafuati mkumbo,Hawaogopi vyama vyao vya siasa kwa kuhofia kufukuzwa uanachama,Ni waumini wa ukweli na mengine mengi.Tatizo lao na wengine ni kuwa-Hawako tayari kufukuzwa uanavyama,Wachumia tumbo,Waoga nk.

Chanzo cha hili suala la kuwaona kuwa hawafai katika Siasa za Afrika ni kufeli kwa taasisi ya Familia,Jamii,Dini,na Taifa kwa ujumla.Tumekuzwa katika Mfumo m'bovu mno (Sijui kama uliowataja nao wamekuzwa hivyo).Ukiwa mkweli na mwenye msimamo utapingwa na kuonekana hufai katika mazingira yako lakini mwisho wa siku ukweli hujitenga na uongo,unafiki,ushabiki na umaamuma.

Ukiwa mkweli katika Ngazi ya kifamilia Unapingwa,Shuleni nako unapingwa,Katika nyumba za ibada ndiyo kabisa,Vyuoni ndio funga kazi,Kwenye vyama vya siasa ni majanga,Katika ngazi ya utaifa ndiyo usiseme.Kwa mtu anayekuzwa katika mazingira haya kamwe hawezi kuwa Muumini wa ukweli,Asiyefuata mkumbo,Mshabiki,Mzandiki,Muongo nk.Inabidi tubadili fikara zetu ili tuweze kwenda katika namna ya Kumpendeza Mungu na siyo Shetani.

Unataka uchukiwe na mjinga?.Mwambie akikosea
Ukweli siku zote unapigwa mawe uongo uzidi kuenea
Wenye nia hawana nguvu,na wenye nguvu hawana nia
Wanaridhika na moja wanaogopa kutafuta mia-Fareed Kubanda (Fid Q) fT Bi kidude-Juhudi za wasiojiweza..

Zitto,Bashe nk ni viongozi wanaofaa Afrika.Wanapaswa watujenge kifikara ili tusiwe Waoga,Wanafiki,Mashabiki nk ili kuendana na baadhi ya sifa nilizozitaja hapo juu.
 
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined
Aug 12, 2011
Messages
5,569
Likes
4,898
Points
280
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined Aug 12, 2011
5,569 4,898 280
Kazi kweli...
 
yorkshire

yorkshire

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2016
Messages
1,368
Likes
1,260
Points
280
Age
37
yorkshire

yorkshire

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2016
1,368 1,260 280
Bashe nae unàmuweka kwenye kundi la wanamageuzi?!!!,...huyo ni kibaraka wa upande wa pili na sasa hivi amejipambanua vizuri...haingii akilini kuwashughulikia watendaji wabovu iwe kosa hapo ndo utapatajibbu anapigania mlengo upi.
 
Kingsharon92

Kingsharon92

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Messages
6,640
Likes
7,412
Points
280
Kingsharon92

Kingsharon92

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2015
6,640 7,412 280
Mimi nauliza Hivi aliyekatwa kule Dodoma katika mbio za kuwania Urais alikuwa Lowassa pekee yake au kulikuwa na wengine? Kwa sababu kila siku Lowassa alionewa kwani aliyechaguliwa hakuwa na haki au waliokatwa mbona wako kimya
 
M

mwaura Tesha

Member
Joined
Oct 18, 2014
Messages
49
Likes
22
Points
15
Age
35
M

mwaura Tesha

Member
Joined Oct 18, 2014
49 22 15
Kwa bashe yupo vizuri ila zitto anauma nakupuliza
 
Mango833

Mango833

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2011
Messages
3,769
Likes
19,092
Points
280
Mango833

Mango833

JF-Expert Member
Joined May 4, 2011
3,769 19,092 280
wanasiasa wanaofaa Africa ni kama kibajaji
 
Tua Ngoma

Tua Ngoma

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Messages
2,244
Likes
4,359
Points
280
Tua Ngoma

Tua Ngoma

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2015
2,244 4,359 280
Tofautisha wanasiasa wanamapinduzi kama Malema ,na wanasiasa vibaraka,wala rushwa,wachonganishi,wanafki,na wasaliti kama Zitto kabwe,NAOMBA UMPE HESHIMA YAKE MALEMA,USIMFANANISHE NA UPUUZI.
 
Geofrey Maseta

Geofrey Maseta

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2015
Messages
1,119
Likes
903
Points
280
Geofrey Maseta

Geofrey Maseta

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2015
1,119 903 280
Tofautisha wanasiasa wanamapinduzi kama Malema ,na wanasiasa vibaraka,wala rushwa,wachonganishi,wanafki,na wasaliti kama Zitto kabwe,NAOMBA UMPE HESHIMA YAKE MALEMA,USIMFANANISHE NA UPUUZI.
Yaani huyo jamaa poyoyo kweli kweli ..ana fananisha njegere na njugu mawe ....zitto na mwigamba ni wasaliti na watu wa kujifanya wazalendo ili kujaza matumbo yao tu ...afande sele kawaumbua wazi wazi ...mbona hakuna aliye kanusha? Nyambafu
 
Comi

Comi

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Messages
3,340
Likes
487
Points
180
Comi

Comi

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2011
3,340 487 180
Yaani huyo jamaa poyoyo kweli kweli ..ana fananisha njegere na njugu mawe ....zitto na mwigamba ni wasaliti na watu wa kujifanya wazalendo ili kujaza matumbo yao tu ...afande sele kawaumbua wazi wazi ...mbona hakuna aliye kanusha? Nyambafu
Du! Kidonda kikipata dawa raha kweli. Nashangaa wote wako kimya kama hawakupata taarifa zake ila wakisikia vyama vingine tayari wanatoka na matamko yao
 
T

Tao

Member
Joined
Nov 10, 2018
Messages
27
Likes
58
Points
15
T

Tao

Member
Joined Nov 10, 2018
27 58 15
Hao wawili hawana lolote
1.huyo wa nzega ni kibaraka wa mafisadi wakuu hapa nchini
2 huyo wa kigoma naye anafanya siasa za matukio ili kujaza matumbo
Ujasiri wao huo ni wa kishetani
Hawana jipya
Mengi wanayozungumza bungeni ni ya kawaida saana.
Si wana mapinduzi hata kidogo
 
manengelo

manengelo

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Messages
11,096
Likes
17,975
Points
280
manengelo

manengelo

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2018
11,096 17,975 280
Tutafika tu hata kama kwa kuchelewa
 
Forum statistics

Threads 1,273,260
Members 490,343
Posts 30,475,598