Bashe usiache mbachao kwa msala upitao, Mshauri Lowassa akaangalie mifugo kama alivyoahidi


K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,067
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,067 280
“Ninamini kuwa Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wake 2015. Kwa kuwa Lowassa alituhumiwa kwa mengi, CCM wangeweza kumuita na kumueleza tuhuma zake na sababu za kuondolewa kwa jina lake ili umma ujue anasema Bashe katika mahojiano na gazeti amabayo habari hiyo iliandikwa ukurasa wa mbele na kuendelezwa siku iliyofuta.

Nimesesoma mara mbili taarifa itokakano na mahojiano hayo maalum na mbunge huyo wa Nzega mjini, Hussein Bashe (CCM), lakini kila nikitafakari taarifa hiyo nashindwa kuelewa malengo na madhumuni ya mbunge huyo aliyoyazungumza katika mahojiano hayo.

Bashe anasema si Lowassa pekee wengi wameonewa CCM ndio kichwa cha habari ya kilichopo mbele ya gazeti hilo lililofanya mahojiano na Bashe.

Kilichonifanya nitafakari baada ya kusoma mahojiano hayo mara mbili mbili na kushindwa kabisa kuelewa malengo ya Bashe ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa chama chake.

Labda la kumshauri Bashe kuwa ”asiache mbaacho kwa kwa msala upitao” anaweza kuwa msemaji wa kumtetea mtu binafsi tena Kada wa chama kingine.

Bashe anapaswa kujua kuwa kisiasa Edward Lowassa hana thamani tena ndani ya CCM na wana CCM. Labda Lowassa anaweza kuendelea kuwa na thamani kwa CCM na wana CCM kama huko aliko anaendelea kutumiwa na CCM kwa manufaa ya CCM na wanachama wake.

Hata kama Lowassa ataamua kurejea tena CCM kama makada wenzake wa zamani walivyoamua kurejea hatakuwa na ndoto zake tena za kutaka urais akiwa nadani ya CCM, labda ndoto hiyo iwe ni ugonjwa sugu usiopona,

Bashe anapaswa kufahamu kuwa kimsingi ya Loawassa yameshapita ndani ya CCM, hayapo na wala hayatarejea tena kama bado anawaza hayo anapotoka, badala ya kuifikiria CCM ambayo imeshikikilia dhamana yake ya ubunge.

Pamoja kuwa ni haki yake ya kikatiba na ya kidemokrasia kutoa maoni na mawazo yake kwa kadri anavyoona. Sawa lakini hakuna haki isiyokuwa na mipaka pamoja na kanuni zake

Katika mambo amabyo watanzania tutaendelea kumuenzi baba wa taifa Mwl. Nyerere ni kuiacha nchi katika misingi imara ya kuwapata viongozi wake wa kisiasa haswa ndani ya CCM.

Kila mwanachama wa CCM anajua ukweli kuwa linapokuja suala la urais Mwl. Nyerere hakuwa namasihara hata kidogo , suala la mapenzi ya mtu, ama sababu ya sura yake, imani ya dini yake au dhehebu lake, kabila lake na utajiri wake hauna nafasi.

Bashe atambue kuwa CCM inayo misingi yake imara kabisa ya kikanuni ya kupata viongozi wake wa ndani chama. Misingi na kanuni hizi zilikuwepo tangu enzi za Mwl. Nyerere hadi CCM ya sasa ya Rais Magufuli.

Kwa kifupi Lowassa na Bashe wake, wao wenyewe ndio amabao hakujitendea haki wala hawakukitendea haki chama chao,CCM katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais ndani ya chama hicho. Kwamba wao wae juu ya misingi na kanuni za uteuzi kwa nafasi hiyo ya urais wa CCM. Kwa hakika hakujitendea haki wao wala chama chao katika hilo.

Kama Lowassa na Bashe pamoja na wapambe wao walidhani kuwa wanaweza kuwa juu ya CCM, wanaweza kuwa juu ya kanuni na misingi ya uteuzi kwa nafasi ya urais walikosea sana.

Mwisho kabisa nimpongeze Bashe kwa ujumbe alioutoa ambao unamkatisaha tamaa kabisa Lowassa huko aliko, ujumbe wenyewe ni huu Bashe anasema ana uhakika wa CCM kushika dola kwa mika 20 baada ya sasa, “Nina uhakika CCM itaendelea kushika dola kwa zaidi ya miaka 20 ijayo, ni miaka mingi kisiasa” hapa anazungumzia kipindi cha tatu baada ya rais Magufuli, hakika kabisa kwa ujumbe huu hamtendei haki Lowassa zaidi ya kumkatisha tama.

Kwa ujumbe huu wa Bashe, ina maana ndoto ya Lowassa kupata urais wa Tanazania ni ndoto ya mchana anapaswa kuachana nayo, asimamie kauli yake ya kwenda kuangalia mifugo yake kama alivyowaahidi watanzania aliposema kishindwa katika uchaguzi atakwenda kuangalia mifugo yake na kuachana na siasa.
 

Forum statistics

Threads 1,274,104
Members 490,586
Posts 30,501,122