Bashe: Taifa linahitaji maombezi 'limekosa mwelekeo kutokana na mapepo' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe: Taifa linahitaji maombezi 'limekosa mwelekeo kutokana na mapepo'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Mar 8, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Hussein Bashe amesema kuwa taifa linahitaji kuombewa na viongozi wa dini kwa madai kuwa kuna pepo mbaya anayelisumbua.

  Bashe alitoa kauli hiyo juzi jioni katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye uzinduzi wa DVD inayojulikana kwa jina la ‘Muziki wa Injili' iliyoimbwa na Kwaya ya Mbiu ya Kanisa la Wasabato, Tandale.

  Aliwaomba viongozi hao kufunga na kuiombea Tanzania ili kuliondoa pepo linalosababisha kuwepo kwa hali ya kutoelewana kati ya viongozi wa juu wa nchi kwa lengo la kuondoa matendo ya kifisadi na udini yanayochochewa na wanasiasa walioshindwa kutimiza wajibu wao.

  Bashe alisema kuwa kilichoifanya nchi ifike hapa ilipo ni viongozi walioshindwa kuwajibika kwa wananchi waliowachagua na badala yake wameamua kutengeneza fitina ikiwemo kutumia kivuli cha udini.

  "…Taifa limekosa mwelekeo kutokana na pepo mbaya ambaye ameanzia juu hali inayoashiria kuwa wanasiasa wameshindwa hivyo inahitajika nguvu ya viongozi wa dini kutushika mkono wanasiasa na kutuonyesha njia sahihi," alisema na kuwaongoza waamini kuchangia sh milioni 22 zitakazotumika kuwafungulia chuo cha ufundi stadi vijana wa Tandale.
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  pepo la ufisadi lililoko CCM ni kiburi sana hata likemewe vipi halitoki dawa ni kuwaomba viongozi wa dini waitambue NGUVU YA UMMA na kuisupport ili tuiondoe CCM!
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  tatizo hawa wa ccm sometimes wanaongea haya bcs walikosa uongozi au walifanyiwa tuu! SIWAAAMINI KABISAA HAWA CCM WOOTE WACHAFUU!
   
 4. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo umenifurahisha tunakemea pepo kwa jinsi ya rohoni baada ya hapo tunarudi mwilini kwa matendo..GOOOOD!!!
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hayo maneno yenye red, kweli kayasema kwa dhati au ndo maandalizi ya 2015!!!!:A S 13:
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Sasa anza huku HABARI CORP kwanza...Bwana Bashe
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Bashe...tumeshaomba sana, tunachosubiri ni majibu ya maombi yetu...ambayo ni chama na serikali mbadala ya kuiongoza nchi yetu ya Tanzania na si CCM
   
 8. G

  Godwine JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  dogo hajui somalia ilipoteza uelekeo toka zamani? au anaongelea bongo?
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  dogo ni mfanyakazi wa habari corparation ambayo ni ya rostam haziz sasa pimeni maneno yake na vitendo
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu nakwambia mpaka ifike hiyo 2015 tutaona mengi kwani tayari wameshaanza mbio kabla ya filimbi, huyo Bashe ndiye aliyeshiriki kwa nguvu kubwa ya kipesa aliyopewa na Rostam pamoja na EL kumg'oa Seleli wa Nzega ili aupate Ubunge na kweli alishinda lakini kumbe hakujua kuwa kundi jingine ndani ya CCM lilikuwa linaona bora ubunge aupate yule Mrundi kwani yeye Bashe si kutoka kundi la Makamba na JK, sasa naona wameanza kujipanga kwa nguvu zote kwani ni juzijuzi tu EL naye alikuwa na waimbaji sijui wa wapi vile na alitoa kauli kama hii ya Bashe na eti EL ataishawishi serikali kuongeza mishahara...mmmhhhhh ama kweli shetani kavaa joho/Kanzu madhahabuni
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Taratibu mh. Bashe hayo mapepo unayoomba yakemewe yasije yakawalipukia nyie wenyewe na chama chenu!!!
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi tutakuwa tunamwamini mtu kwa kuangalia kwanza historia yake. Pamoja na mazuri ambayo bashe ameongea sina uhakika kama ana 'moral authority' ya kuongea hivyo hadharani. Mtanisaidia wenzangu.
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,607
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Makanisa huwa yanajaa kama watu either wana shida na matatizo kama ilivyo kwa watanzania wengi,ama kama wamebarikiwa,makanisa huwa yananufaika either or,hata hivyo makanisa ya Afrika yanajaa kutokana na wakazi wake kuwa masikini na wenye magonjwa mengi wasiokuwa na matumaini ya maisha kabisa,wenye njaa na wasiokuwa na elimu,ndo ukweli huo.

  Na huyo bashe anayedai nchi ina mapepo and so iombewe,je anajua nani kalitupia Taifa mapepo na kwasababu gani?Badala ya kuendelea kuomba mchawi asituloge ama kututupia mapepo,kwanini tusimkamate huyo mchawi,tummalizie mbali yeye na mapepo yake?Kiutaratibu,mtu huyaachia mapepo yaingie ama huyakaribisha yeye mwenyewe,sasa nani kakaribisha mapepo kiasi kwamba yamewatawala viongozi na hivyo kufanya maamuzi ya kimapepo?Sidhani kama kila mwananchi wa Tanzania ameyakaribisha mapepo,lazima kuna walioyakaribisha,sidhani kama ni wote.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  unajua saa nyingine hata haya mapepo tunayaonea tu, hivi ni kweli Watanzania hatujuhi matatizo yetu kweli kiasi cha kumsingizia pepo?
  Unataka kuniamboa issue ya Dowans, EPA, IPTL na zingine kama hizo ni mapepo, hayo ni mapepo ya aina gani?

  yeye (Bashe) alipotolewa na kina Kingwangwalah anataka kutuambia lilikuwa ni pepo? au hajuhi sababu gani zilizomnyima kuongoza jimbo la Nzega?
   
 15. m

  moshdar JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 1,731
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  matatizo yetu watz kwa sasa ni ya kiuchumi zaid and so need uvumbuzi wenye mantiki kiuchumi. huyu dogo Hussein akafungue kanisa....aah no i mean msikiti(hussein) akatangaze injili njema kwa watu wote. mtu kama huyu eti ndo mafisadi walitaka kumwingiza kwenye ubunge then wampe uwaziri....halafu eti tunatarajia watanzania tusiendeleee kuliwa na funza???!!! how ikiwa watu wenyewe ndo kama hawa??
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Bashe,wakati ule mwenyekti wa ccm alipotengewa majini yamlinde kutoka kwa she yahya mbona hakusema tukemee?? Au kuna majini mazuri na mabaya?anyway!
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aliyekaribisha mapepo humjui? Ulikuwepo kwenye mkutano wake pale jangwani alipozirai? anga lilikuwa limejaa uchafu mtupu! nchi hii inahitaji maombi ya kweli, ama sivyo blah blah zitakuwa nyingi lakini shida zinabaki pale pale...
   
 18. c

  chetuntu R I P

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi mbio za 2015,ametumwa na kikosi kazi, wameshaanza kupiga jaramba. Tutamtambua Bashe kwa matendo. Anatamka maneno hayo huku bado analala na kuamkia kwenye lindi la ufisadi ulitopea! Tuanze kumuombea yeye na task force ya RA.
   
 19. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  mwaka wa kauli tata.....na bado nategemea mengi toka kwake na ile kambi yetu
   
 20. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Binafsi simfahamu bali najaribu kufikiri juu ya ulichokisema,nani ambae hapa JF atakuja na kusema yeye ni Msafi hana uhusiano na Mafisadi PAPA au Nyangumi.
  Ninaanza wanao lala na kuamka kwa mafisadi PAPA ama Nyangumi

  wafanyakazi wa vodacom RA ni shareholder
  wafanyakazi wa CRDB Mengi ni shareholder
  Wafanyakazi GGM Mafisadi wanaopora rasilimali zetu wapo huko
  Wafanyakazi wa TIGO Mafisadi wanaotuibia sekunde unalipa kwa garama dk
  Wafanyakazi Airtel mafisadi wanaotuibia kwa matangazo mazuri tofauti
  na garama halisi
  Wafanyakazi wa Bank M
  Wafanyakazi wa Quality Group
  wafanyakazi wa Twiga Cement
  Wafanyakazi wa IPP
  kwa njia moja ama nyingine wengine humo ni mawakala wa vocha za mafisadi ama tunawasaidia kuhamisha rasilimali za nchi tunafanya kazi kwenye Mabenki tuna shiriki kuhamisha peasa zao kwenda ulaya.
  now tujiulize tunahaki hiyo ya kumnyoshea BASHE mkono? kuhusiana na hoja kwamba anafanyakazi kwa RA?

  wana JF tujadili issue na sio personalities.
   
Loading...