Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Bashe amemshauri spika wa Bunge Mh.Job Ndugai Kugombea tena ubunge 2025.
Bado nashangazwa na hii tabia ambayo rasmi imeshajijenga kwenye serikali. Kwa nini mnawaza sana uchaguzi wa 2025? Ni miezi michache tu tumetoka kwenye uchaguzi wa 2020.
Sasa badala ya kuanza kuleta Maendeleo kwa wananchi,nabaki kushauriana kugombea 2025. Tatizo nini hasa?
Wenyewe Mara kadhaa mmekiri kuwa uchumi umeshuka sana, kwa nini msitumie nguvu kubwa kupandisha huo uchumi hadi hiyo 2025 kuliko kuwaza kugombea tu?
Tumewakosea wapi? Kwa nini hizi mambo msianze mwishoni mwa 2024 au mwanzoni mwa 2025. Chama ni chenu mtaamua kwa kwa kadri mnavyoweza kupitishana huko chamani. Ila kwa Sasa tunataka Maendeleo tu
Kuna tatizo kubwa sana CCM.
Na yoye haya yameasisiwa na mwenyekiti wao aliyeanza kutangaza kugombea mapema.
----
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kubadili uamuzi wake wa kutogombea tena ubunge wa Kongwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Bashe ametoa kauli hiyo jana jioni Oktoba 11, 2021 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa korosho wa wilaya za Mpwapwa, Kongwa na Manyoni.
Mkutano huo ulifanyika katika Chuo cha Veta Kongwa na Spika Ndugai alikuwa Mwenyekiti aliyeongoza majadiliano ambayo yalianza saa 4 asubuhi- hadi saa 12 jioni.
Bashe amesema mipango mizuri ambayo imeanzishwa na Ndugai haipaswi kubezwa na kuwa akija mwingine huenda asiendeleze kwani kila mmoja ana mipango yake.
"Nilisoma kwenye mitandao kuwa ukitaka kustaafu na Rais John Magufuli, lakini Mungu ana mipango na makusudi yake, leo tuko na Samia Suluhu Hassan ambaye tunakwenda naye hadi 2030, naomba ufikiri namna ya kubadili uamuzi wako," amesema Bashe.
Naibu Waziri amesema itakuwa na maana kama Ndugai atakubaliana na wazo hilo ambalo litampeleka kukamilisha ndoto za watu wa Kongwa hasa kwenye dhahabu ya kijani ambayo ni korosho.
Kauli ya Bashe iliibua shangwe kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo ingawa Ndugai mwenyewe hakujibu kitu wakati watu walipokuwa wanapiga makofi.
Katika hatua nyingine, Bashe amesema serikali itahakikisha inakamilisha mipango yake ili wakulima wa Kongwa, Mpwapwa na Manyoni wanufaike na Kilimo hicho.
Ameahidi serikali inakwenda kujenga kiwanda cha kubangulis korosho katika kijiji cha Mbande ili wakulima wavune na kubangua korosho zao hapo.