Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,154
- 10,809
Kwenye interview hii aliyofanya na clouds tv naibu waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe amesema alishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati rais Magufuli pale alipoiba taarifa za kamati kuu na kutangaza kuwa haogopi kufa, pia kwenye sakata la korosho kushuka bei hayati rais Magufuli alimpigia simu saa nane usiku na kumhoji kama kweli kuna binadamu ambaye haogopi kufa pia akamwambia kama korosho zitaendelea kukosa soko na kushuka bei basi yeye Hussein Bashe ndiyo atakuwa naibu waziri wa kwanza kutumbuliwa.
Naibu waziri Hussein Bashe amemwelezea hayati Magufuli kwa mambo manne.
1. Magufuli kama reformer: hayati Magufuli alikuwa anatamani sana kubadilisha namna watanzania na serikali yao wanavyofikiri na kufanya kazi.
2. Magufuli kama pan africanist : hayati Magufuli alikuwa anaamini waafrika wanaweza bila msaada wowote ule.
3. Magufuli kama muunimini na mfuasi wa waasisi wa mataifa ya Afrika kama Nkwame Nkuruma na Julius Nyerere ndiyo maana aliweza kuhamishia serikali Dodoma na kufufua ujenzi wa bwawa la stiglers gorge uliokwama tangu maiaka ya sabini.
4. Magufuli kama muumini wa kujitegemea : hayati Magufuli alikuwa anaamini kuwa hakuna namna nyingine ya kuwafanya watanzania waendelee zaidi ya kuwahubiria kuwa wanaweza wao wenyewe na lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa sana ndiyo maana aliruhusu kila mtu afanye kazi kwa uhuru ikiwemo wamachinga.
Husseni Bashe pia amemwelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa mtu wa huruma sana na kama unataka kujua hilo ni mpaka utakapopatwa na tatizo lako binafsi, mfano ni yeye Bashe alipofiwa na mama yake mzazi mwaka 2017, mtu wa kwanza kwanza kuwa karibu yake mpaka msiba unaisha ni Magufuli.
Bashe amemwelezea Rais Samia kuwa ni mtu wa practical na siyo theory na akasema kama kuna mtu anadhani kuwa miradi iliyoachwa na hayati Magufuli haitakamilika chini ya rais Samia basi anapoteza muda wake bure, kwani siyo rais wa maneno mbali vitendo.