Bashe: Nilishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati Magufuli, Rais Samia ni photocopy ya Magufuli

Magufuli alikuwa na mazuri na mabaya yake kama tulivyo wengine wote, tusijidanganye, kuendelea kumsema vibaya hakutufanyi wengine tuwe watakatifu.
Angalau unasema ukweli kwa mara ya kwanza oops, khe khe khe khe khe heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga
2339015_Screenshot_20200303-141241-picsay.jpeg
 
Sifa zote hizi hakuwa nazo Magufuli.

Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga. Hakuwa tofauti na mwendawazimu ambaye ajiona ana nguvu na kuamua kumsogelea mtu mwenye mabomu na AK 47.

Anaamini Tanzania tunaweza kujifanyia mambo yetu wenyewe kwa kuanzisha miradi mikubwa kwa kukopa kimya kimya na kupora fedha za watu. Nadhani hakujua kuwa kukopa Sana kwa siri na kupora fedha za watu siyo jambo endelevu na lenye tija. Ujasiri wa kijinga.

Mfano huu unaonesha jasiri wa nmna hii ni mpumbavu.

Wachache sana tulimuelewa
#kataawahuni
 
Bashe anaakili sana anayajua mapungufu ya Magufuli lakini ameeleza vizuri sifa za Magufuli ambazo zinamtofautisha sana na viongozi wengine!
Lakini Mama akimpa Uwaziri Mkuu sasa hivi tutaanza kusikia kelele za Nchi kuibiwa na Wataliban.
 
Jiwe alinizingua Sana , hata hvyo jamaa alikuwa mpambanaji

Kweli alikuwa mpambanaji na mwenye uthubutu laiti angekuwa anafanya utafiti kabla ya kukurupuka katika maamuzi yake pengine matokeo mabaya ya uamuzi wake yangeepukika!!
 
Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga. Hakuwa tofauti na mwendawazimu ambaye ajiona ana nguvu na kuamua kumsogelea mtu mwenye mabomu na AK 47.
Yule jamaa yenu ana ujasiri wa kijinga sana, jibaba zima unakimbilia ulaya kwenda kupumuliwa na wanaume wenzio kama huo siyo ujasiri wa kijinga ni nini?
Wanakupumulia, halafu wanakutangaza kuwa wewe ni mkuu wa washikishwa ukuta na wewe unashangilia, kama huo siyo ujasiri wa kijinga ni nini?
 
Yule jamaa yenu ana ujasiri wa kijinga sana, jibaba zima unakimbilia ulaya kwenda kupumuliwa na wanaume wenzio kama huo siyo ujasiri wa kijinga ni nini?
Wanakupumulia, halafu wanakutangaza kuwa wewe ni mkuu wa washikishwa ukuta na wewe unashangilia, kama huo siyo ujasiri wa kijinga ni nini?
Alikuwepo shetani ikulu....by Askofu Mwingira
 
Kweli alikuwa mpambanaji na mwenye uthubutu laiti angekuwa anafanya utafiti kabla ya kukurupuka katika maamuzi yake pengine matokeo mabaya ya uamuzi wake yangeepukika!!
Unaweza kutaja mambo 5 aliyokurupuka?
 
Kwenye interview hii aliyofanya na clouds tv naibu waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe amesema alishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati rais Magufuli pale alipoiba taarifa za kamati kuu na kutangaza kuwa haogopi kufa, pia kwenye sakata la korosho kushuka bei hayati rais Magufuli alimpigia simu saa nane usiku na kumhoji kama kweli kuna binadamu ambaye haogopi kufa pia akamwambia kama korosho zitaendelea kukosa soko na kushuka bei basi yeye Hussein Bashe ndiyo atakuwa naibu waziri wa kwanza kutumbuliwa.

Naibu waziri Hussein Bashe amemwelezea hayati Magufuli kwa mambo manne.
1. Magufuli kama reformer: hayati Magufuli alikuwa anatamani sana kubadilisha namna watanzania na serikali yao wanavyofikiri na kufanya kazi.
2. Magufuli kama pan africanist : hayati Magufuli alikuwa anaamini waafrika wanaweza bila msaada wowote ule.
3. Magufuli kama muunimini na mfuasi wa waasisi wa mataifa ya Afrika kama Nkwame Nkuruma na Julius Nyerere ndiyo maana aliweza kuhamishia serikali Dodoma na kufufua ujenzi wa bwawa la stiglers gorge uliokwama tangu maiaka ya sabini.
4.Magufuli kama muumini wa kujitegemea : hayati Magufuli alikuwa anaamini kuwa hakuna namna nyingine ya kuwafanya watanzania waendelee zaidi ya kuwahubiria kuwa wanaweza wao wenyewe na lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa sana ndiyo maana aliruhusu kila mtu afanye kazi kwa uhuru ikiwemo wamachinga.
Husseni Bashe pia amemwelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa mtu wa huruma sana na kama unataka kujua hilo ni mpaka utakapopatwa na tatizo lako binafsi, mfano ni yeye Bashe alipofiwa na mama yake mzazi mwaka 2017, mtu wa kwanza kwanza kuwa karibu yake mpaka msiba unaisha ni Magufuli.
Bashe amemwelezea Rais Samia kuwa ni mtu wa practical na siyo theory na akasema kama kuna mtu anadhani kuwa miradi iliyoachwa na hayati Magufuli haitakamilika chini ya rais Samia basi anapoteza muda wake bure, kwani siyo rais wa maneno mbali vitendo.


Bashe kamtendea haki Magufuli kwa aina hizo 4. Hongera sana Bashe
 
Bashe, Msukuma na Adam Malima walipanga wamvimbie live Mzee kwny Mkutano Mkuu wa chama

Walihifadhiwa sehemu salama wasihudhurie mkutano huo na baada ya muda wakalamba uteuzi
Alimaanisha nini alipomuiliza kama haogopi kufa?
 
Katuthibitishia kwamba alikuwa muuaji. Bashe angekomaa hivi sasa angekuwa marehemu.

Siri zinaendelea kufichuka
Shida ya hawa vijana ni kwamba wanapokosa madaraka wanakuwa kasuku wakubwa mnoo wa kupiga kelele na kukosoa, wakiingizwa madarakani wanageuza antena/dishi, in short hawako consistency.
 
Back
Top Bottom