Bashe: Nilishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati Magufuli, Rais Samia ni photocopy ya Magufuli

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,068
2,000
Kwenye interview hii aliyofanya na clouds tv naibu waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe amesema alishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati rais Magufuli pale alipoiba taarifa za kamati kuu na kutangaza kuwa haogopi kufa, pia kwenye sakata la korosho kushuka bei hayati rais Magufuli alimpigia simu saa nane usiku na kumhoji kama kweli kuna binadamu ambaye haogopi kufa pia akamwambia kama korosho zitaendelea kukosa soko na kushuka bei basi yeye Hussein Bashe ndiyo atakuwa naibu waziri wa kwanza kutumbuliwa.

Naibu waziri Hussein Bashe amemwelezea hayati Magufuli kwa mambo manne.

1. Magufuli kama reformer: hayati Magufuli alikuwa anatamani sana kubadilisha namna watanzania na serikali yao wanavyofikiri na kufanya kazi.

2. Magufuli kama pan africanist : hayati Magufuli alikuwa anaamini waafrika wanaweza bila msaada wowote ule.

3. Magufuli kama muunimini na mfuasi wa waasisi wa mataifa ya Afrika kama Nkwame Nkuruma na Julius Nyerere ndiyo maana aliweza kuhamishia serikali Dodoma na kufufua ujenzi wa bwawa la stiglers gorge uliokwama tangu maiaka ya sabini.

4. Magufuli kama muumini wa kujitegemea : hayati Magufuli alikuwa anaamini kuwa hakuna namna nyingine ya kuwafanya watanzania waendelee zaidi ya kuwahubiria kuwa wanaweza wao wenyewe na lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa sana ndiyo maana aliruhusu kila mtu afanye kazi kwa uhuru ikiwemo wamachinga.

Husseni Bashe pia amemwelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa mtu wa huruma sana na kama unataka kujua hilo ni mpaka utakapopatwa na tatizo lako binafsi, mfano ni yeye Bashe alipofiwa na mama yake mzazi mwaka 2017, mtu wa kwanza kwanza kuwa karibu yake mpaka msiba unaisha ni Magufuli.

Bashe amemwelezea Rais Samia kuwa ni mtu wa practical na siyo theory na akasema kama kuna mtu anadhani kuwa miradi iliyoachwa na hayati Magufuli haitakamilika chini ya rais Samia basi anapoteza muda wake bure, kwani siyo rais wa maneno mbali vitendo.

mjasiri na mali

JF-Expert Member
Aug 2, 2018
888
1,000
hivi duniani tunahangakia matumbo tyu au kuna mengine?kabla hajapata ulaji alikuwa mkosoaji mzuri wa mwendazake ila baada ya kupewa unaibu waziri kageuka wakala wa kusifia hata pasipostahili sifa..

kama serikali yetu ingewekeza kwenye vipaji bila shaka kwenye unafki wangeweka kipaumbele
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
12,492
2,000
Sifa zote hizi hakuwa nazo Magufuli.

Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga. Hakuwa tofauti na mwendawazimu ambaye ajiona ana nguvu na kuamua kumsogelea mtu mwenye mabomu na AK 47.

Anaamini Tanzania tunaweza kujifanyia mambo yetu wenyewe kwa kuanzisha miradi mikubwa kwa kukopa kimya kimya na kupora fedha za watu. Nadhani hakujua kuwa kukopa Sana kwa siri na kupora fedha za watu siyo jambo endelevu na lenye tija. Ujasiri wa kijinga.

Mfano huu unaonesha jasiri wa nmna hii ni mpumbavu.
 
passioner255

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
1,938
2,000
Sifa zote hizi hakuwa nazo Magufuli.

Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga. Hakuwa tofauti na mwendawazimu ambaye ajiona ana nguvu na kuamua kumsogelea mtu mwenye mabomu na AK 47.

Anaamini Tanzania tunaweza kujifanyia mambo yetu wenyewe kwa kuanzisha miradi mikubwa kwa kukopa kimya kimya na kupora fedha za watu. Nadhani hakujua kuwa kukopa Sana kwa siri kupora fedha za watu siyo jambo endelevu na lenye tija. Ujasiri wa kijinga.

Mfano huu unaonesha jasiri wa nmna hii ni mpumbavu.
Nonsense
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
32,772
2,000
westbrookwtf.png
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,513
2,000
Rule of thumb: huwezi kuwa bingwa kwa kuondoa/kumzuia mshindani wako kwenye mpamabano

Ndio maana tunaambiwa usimsifu mkimbiaji bila kumsifu mkimbizaji pia

Mathalani utakuwa Mjinga sana unapomsifu Magu bila kumsema Lisu

Halikadharika nitashangaa ukimsifu SSH bila kumpongeza ................... anaempelekesha!!!

................. huu ndio mtihani wetu kwa sasa
 
sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
1,887
2,000
Kwenye interview hii aliyofanya na clouds tv naibu waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe amesema alishawahi kushukiwa kama mwewe na hayati rais Magufuli pale alipoiba taarifa za kamati kuu na kutangaza kuwa haogopi kufa, pia kwenye sakata la korosho kushuka bei hayati rais Magufuli alimpigia simu saa nane usiku na kumhoji kama kweli kuna binadamu ambaye haogopi kufa pia akamwambia kama korosho zitaendelea kukosa soko na kushuka bei basi yeye Hussein Bashe ndiyo atakuwa naibu waziri wa kwanza kutumbuliwa.

Naibu waziri Hussein Bashe amemwelezea hayati Magufuli kwa mambo manne.
1. Magufuli kama reformer: hayati Magufuli alikuwa anatamani sana kubadilisha namna watanzania na serikali yao wanavyofikiri na kufanya kazi.
2. Magufuli kama pan africanist : hayati Magufuli alikuwa anaamini waafrika wanaweza bila msaada wowote ule.
3. Magufuli kama muunimini na mfuasi wa waasisi wa mataifa ya Afrika kama Nkwame Nkuruma na Julius Nyerere ndiyo maana aliweza kuhamishia serikali Dodoma na kufufua ujenzi wa bwawa la stiglers gorge uliokwama tangu maiaka ya sabini.
4.Magufuli kama muumini wa kujitegemea : hayati Magufuli alikuwa anaamini kuwa hakuna namna nyingine ya kuwafanya watanzania waendelee zaidi ya kuwahubiria kuwa wanaweza wao wenyewe na lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa sana ndiyo maana aliruhusu kila mtu afanye kazi kwa uhuru ikiwemo wamachinga.
Husseni Bashe pia amemwelezea hayati Magufuli kuwa alikuwa mtu wa huruma sana na kama unataka kujua hilo ni mpaka utakapopatwa na tatizo lako binafsi, mfano ni yeye Bashe alipofiwa na mama yake mzazi mwaka 2017, mtu wa kwanza kwanza kuwa karibu yake mpaka msiba unaisha ni Magufuli.
Bashe amemwelezea Rais Samia kuwa ni mtu wa practical na siyo theory na akasema kama kuna mtu anadhani kuwa miradi iliyoachwa na hayati Magufuli haitakamilika chini ya rais Samia basi anapoteza muda wake bure, kwani siyo rais wa maneno mbali vitendo.

Bashe anaakili sana anayajua mapungufu ya Magufuli lakini ameeleza vizuri sifa za Magufuli ambazo zinamtofautisha sana na viongozi wengine!
 
CHARLES2016

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
375
500
Sifa zote hizi hakuwa nazo Magufuli.

Magufuli alikuwa na ujasiri wa kijinga. Hakuwa tofauti na mwendawazimu ambaye ajiona ana nguvu na kuamua kumsogelea mtu mwenye mabomu na AK 47.

Anaamini Tanzania tunaweza kujifanyia mambo yetu wenyewe kwa kuanzisha miradi mikubwa kwa kukopa kimya kimya na kupora fedha za watu. Nadhani hakujua kuwa kukopa Sana kwa siri kupora fedha za watu siyo jambo endelevu na lenye tija. Ujasiri wa kijinga.

Mfano huu unaonesha jasiri wa nmna hii ni mpumbavu.
Brainwashed idiot!!

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom