Martin Maranja Masese
Member
- Apr 24, 2011
- 29
- 542
Upatikanaji pembejeo
Teknolojia duni za Kilimo
Utekelezaji bajeti ya kilimo
Kilimo cha kutegemea Mvua
Ukosefu wa Huduma za Mikopo
Unafuu upatikanaji zana za kilimo
Uhaba wa mafunzo ya kilimo bora
Ukosefu wa masoko kwa shughuli za Kilimo
Malizeni hayo, ndiyo mwage sifa kwa Hussein Bashe kwamba anaupiga mwingi. Kilimo kinatakiwa kuondoka katika mipango na michoro juu ya karatasi nyeupe, mipango iwekwe katika Utekelezaji. Wakulima wanataka changamoto hizo zitatuliwe, siyo kuvaa kombati na kuanzisha kauli mbiu.
Pia, ambao mnasema Bashe anaupiga mwingi, mtuonyeshe matumizi ya teknolojia katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa masoko. Mnatakiwa mtuonyeshe jinsi mradi wa kilimo utakavyokuwa na mnyororo wa thamani kwa kuweza kuuza bidhaa hata nje ya nchi.
Sekta ya kilimo ya Tanzania - ambayo inachangia karibu theluthi ya Pato la Taifa la nchi na kuajiri asilimia 75 ya idadi ya watu - ina fursa ya kuongeza mapato na kuboresha maisha. Mmekubalianaje? Mnafungamanisha sekta ya kilimo na viwanda na miradi mikubwa iliyopo nchini?
Sote tunafahamu, uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta ya kilimo unakumbana na uhaba wa mitaji, viwango vya chini vya uwezo na ujuzi wa biashara. Mnayo mikakati gani eneo hilo? Vipi, sera zinazokwamisha ukuaji, mmeziondoa? Au mmeridhika tu kauli mbiu ya Agenda 10/30?
Miongoni mwa changamoto kubwa kwa wakulima ni ukosefu wa masoko ya bidhaa zao za kilimo na mabadiliko ya tabia nchi. Ninyi wasukuma agenda za Hussein Bashe mnatakiwa kuja kwetu na mbinu zitakazokuwa na suluhisho la changamoto hizo, siyo kusema "Bashe anaupiga mwingi" tu.
MMM, Martin Maranja Masese