Bashe kuongea na vyombo vya Habari, ni kueleza ukweli na kukanusha upotoshaji unaoendelea

Bashe ni miongoni mwa wabunge wa vvm walio na akili..... nafikiri jamaa alitaka amtoe ili asipinge bajeti ya viwanda vya machinga...du! @
cc. Lizaboni
 
Nimemuona Bashe amehojiwa Azam TV ameingia ubaridi amesema hawezi kuongea chochote kwakuwa katibu mkuu ataongea yeye.
 
Naona wameanza kujitekenya na kucheka wenyewe....chezea dozi ya Mwenyekiti wewe.

Na siku zote 'zimwi likujualo halikuli ukakwisha"
Ingawa pia hakuna ugonjwa mbaya duniani kama ugonjwa wa fikra finyu kwani hupelekea kuzaa kansa inayoitwa "unafiki".
 
Ivi huyo jamaa ni raia halali?
Ili uwe raia halali inabidi uwe na nidhamu ya woga au mdomo wenye glue?????? Inabidi uwe na pua kama kitumbua ndo uwe raia au inabidi uwe na rangi ya mpingo??? Tumechoka kusikia hii. Nchi hii siyo wa wabantu pekee kuna wengine tulikutwa humu kama wasonji, wabarbaig, wasandawi, wamasaai, wahima wa ngara na biharamulo, sasa tumeanza kuambiwa siyo raia wakati tumekuwa hapa zaidi ya miaka zaidi ya kalne 9 sasa nyinyi wakuja toka naigeria na senegal mmekuwa raia kuliko sisi? Soma history halafu rudi hapa.
 
Bashe ndio mbunge pekee wa CCM aliye na ujasiri. Nafkiri ni kwa kuwa hana njaa sana
Apana kwa sababu ni Msomali na hawa ndugu zetu wana msimmamo.

Miaka ya 70 tulikuwa na mwanajeshi Pilot alikuwa anaitwa Major Omar alitoka Tanga , ilitokea vita kati ya Ethopia na Somalia, wakati huo Tanzania ilikuwa Rafiki wa nchi zote mbili ambazo zilikuwa na siasa za kiujamaa.

Major Omar alikuwa Rubani wa Ndege ya uchukuzi. Waliamriwa kupeleka Askari wa ki Ethopia waliokuwa wako mafundishoni Tanzania pamoja na Planners wa kijeshi wa Kitanzania.

Major Omar aligoma na akawa tayari kuhukumiwa, Nasikia Nyerere alimuita akamuuliza kwa nini umevunja Amri, nasikia akamjibu kwa sababu Raisi wewe umevunja Amri na katiba ya Tanzania ya NOn Alignment na baadala ya kuwapatanisha umeamua kuiunga mkono nchi moja.
 
Back
Top Bottom