Bashe, Kigwangalla vita kali Nzega. Bashe amsasambua Mh. Kigwangalla

Maelezo marefu ya Bashe juu ya mbunge wake yananipa shida sana.

  • Kwanini Bashe aliamua kuisaliti nafsi yake na imani yake juu ya UKWELI na sasa kuja kunung'unika hivi?
  • Kwanini hukusimamia ukweli tangu mwanzo?
  • Bashe alijua fika kwamba mbunge alikwenda mahakamani kwenda kutoa kiapo cha uongo kwanini alijiingiza kumfanyia kampeni mtu muongo na aliye "ruin future" ya mtu mwingine?
  • Bashe alijua hata utata wa elimu ya mbunge wake, alijua mikakati mibovu ya kujinufaisha ya mbunge wake, bado Bashe alifunga macho nakuendelea kumkampenia mtu huyo, sasa Bashe anaitoa wapi 'moral authority' ya kumsuta Hamis Kigwangalah?
Eti anamshauri muovu amsaidie mtu aliye mdhulum! ni sawa na kumshauri jambazi arudishe japo kidogo cha alivyo pora. Bashe, if you belive in God who is omnipotent, omniscient and omnipresent don't make a grave mistake of personifying HIM. Huna sababu yoyote ya msingi ya kulalama kwetu kwa kuwa ulikumbatia uovu kwa nia ya kunufaika nao kwa jina la CCM.

Majambazi yakizidiana huishia kuuana.
 
Huyu mbunge, nadhani anayo kesi "jinai" ya kujibu.
Kupora haki ya mtu!
 
Ndiyo shida kurusha mawe ukiwa kwenye. Nyumba ya vioo. Na bado watalipuana hawa ni. Vidagaa tusubiri mapapa na Yale manyagumi baada ya zoezi Lao la kujivua ngamba. Mgao wote wa EPA na rada,rechmond ,iptl na mauchafu. Mengine yaliyojificha yatawekwa. Wazi. Na ukweli. Utawaweka huru. Lipua
 
Kwa maelezo haya Bashe hata kama kaishia darasa la saba,anaonekana msomi na mjuvi wa kupanga hoja kumshinda huyo Mbunge wake anayejitapa na 'usomi' wake unaotiliwa shaka
 
Ni kichwa lakini ameingia ndani sana kumwambia kingwangala hana Baba,kama kweli hana Baba yeye hakupenda kuto kuwa na Baba.

Hiyo siyo kashfa wala tusi.Hakuna mtu asiyekuwa na baba.Huwezi kuzaliwa bila baba.Bashe kampe homework mbunge wake,kuwa yeye hamtambui baba yake tangia wanasoma.Sasa mbunge aje hapa ajibu mapigo ya Bashe!
 
tunalipa mishahara mataperi na wezi wa vyeti
ina maana ccm wamekuwa wasaliti kiasi hiki
huyu jamaa wanamlipa fadhila gani? maana serikali hii na kulipa fadhila
 
Maelezo marefu ya Bashe juu ya mbunge wake yananipa shida sana.

  • Kwanini Bashe aliamua kuisaliti nafsi yake na imani yake juu ya UKWELI na sasa kuja kunung'unika hivi?
  • Kwanini hukusimamia ukweli tangu mwanzo?
  • Bashe alijua fika kwamba mbunge alikwenda mahakamani kwenda kutoa kiapo cha uongo kwanini alijiingiza kumfanyia kampeni mtu muongo na aliye "ruin future" ya mtu mwingine?
  • Bashe alijua hata utata wa elimu ya mbunge wake, alijua mikakati mibovu ya kujinufaisha ya mbunge wake, bado Bashe alifunga macho nakuendelea kumkampenia mtu huyo, sasa Bashe anaitoa wapi 'moral authority' ya kumsuta Hamis Kigwangalah?
Eti anamshauri muovu amsaidie mtu aliye mdhulum! ni sawa na kumshauri jambazi arudishe japo kidogo cha alivyo pora. Bashe, if you belive in God who is omnipotent, omniscient and omnipresent don't make a grave mistake of personifying HIM. Huna sababu yoyote ya msingi ya kulalama kwetu kwa kuwa ulikumbatia uovu kwa nia ya kunufaika nao kwa jina la CCM.

Majambazi yakizidiana huishia kuuana.

Kulindana, uongo, uchawi, kuua, kutetea maovu na uporaji wa mali ya umma huo ni utaratibu wetu CCM hivyo usimshangae Bashe kukaa kimya na kumpigia kampeni Kigwangala hata JK alinyamazia maovu ya EPA na Richmond na aliwapigia kampeni waharifu na leo hii anataka wajivue gamba. Kwahiyo msishangae wana JF huo ni utaratibu wetu wana CCM!!!
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.... ati tunakubali Bashe leo msafi, kesho atakuwa Lowassa keshokutwa Rostam

tusiwe black and stupid

tunatumiwa na hamis atakua mbuzi wa kafara kuhoji umeme kwenye swali kwa wizara yao

kesho mtasikia zaidi ila mwenye uzalendo atajua na kumlinda hamisis


acheni ujinga wa kutumiwa na wezi wa rasilimali zetu

Mzee wa Ugoko!Acha Kupotosha na Kuua Move!Kitendo cha Saidi aka Hamis Kuhoji swala la Tanesco na Symbion halimpi Uhalali na Kinga ya Kutohojiwa Ufisadi wake Wa-Elimu!Saidi nae Fisadi hatari sana,Kama ameweza Kuiba Jina la Mwenzake asome yeye!Tena niwahi somaga Gazeti flani siku za nyuma kwamba MBA yake alipeleka 'Insha' Road Safety in TZ!wala hajagongo 'Thesis' kama mie Mkweche
Kweli Ujinga Una-Gauge!
Side B!MSD yako leo Inaandamwa na Mdada mmoja kwenye TZ Daima!Kumbe imeharibu na ARVs!Na Ifutwe
 
Bashe pamoja na kuongea point nyingi lakini mimi nina-question credibility na cleanness yake pamoja na busara yake. Haya mambo hakustahili kuyaweka hadharani wakati wote ni watoto wa mama mmoja yaani Chama Cha Magamba. Sisi hii vita tusiiparamie na kuanza kutoa comment nyepesi nyepesi eti Bashe ni kichwa" Hakuna kichwa hapa bali upungufu wa busara kutoa siri zenu kwa maadui. Hivi angekuwa ni mume anaeleza JF jinsi mke wake alivyo kitandani na tabia zake mngethubutu kumsifia kwamba huyu mume ni kichwa au mngemwona hana busara.

Bashe haya ni mambo ya chumbani kayaongeleeni huko huko kwenye chama cha magamba kwani sisi kuyajua hayatatusaidia kitu. Hivi ni nani miongoni mwa wana JF ana uhakika kwamba kila Bashe alichosema ni kweli. Lazima mwuelewe kuwa Bashe asingekuwa ubunge monger asingeandika kwa uchungu hivyo. Hiki ni kilio cha samaki na machozi yanaondoka na maji pole sana kwani alikuwa hajui CCM wote ni majangili na ni ujanja wa kuzidiana tu hakuna haki mle.
 
Jamani swala hapa ni Mh Mbunge, ni kujivua madaraka, au amfikishe mahakamani Basha kama anaona kamsingizia, maana record si iko hapa ya kimaandishi? Vinginevyo yeye na mama yake wana kesi ya kujibu, hasa mama yake. Huyu kijana kazurumiwa haki yake, jumuia ya watanzania haitakiwi kulifumbia macho hili.

Jamaa na macho yake hayo ya kulembua kama kala kungu, ndo tunamtaka afike mahakamani ajieleze uzuri
 
AHaaaaaaaaaaa nimekumbuka kesi moja ya mtumishi mmoja wa serikali ambaye mwaka jana kama sijasahau alifukuzwa kazi alipogundulika ali forge cheti cha form 6 na kuingia university na kupata degree.
Utagundua kwamba yule bwana ingawa ali forge cheti cha A level lakini bado alifanya vizuri sana chuo kikuu na ali graduate. Hiyo haikumfanya asifukuzwe kazi na kunyang'anywa degree yake! Oohhh poor him!
Leo tuna kesi ya Kigwangala ambayo ni same case. Ebu tuone nani atamchukulia hatua. Na hasa kwa sababu yeye ni wa chama cha magamba!
Wasipomchukulia hatua basi waliochukuliwa hatua walionewa na serikali yao hii hii!
 
nimeukubali ule usemi uliotolewa na mwana JF mwenzetu kuwa ''wenye taaluma za mashaka salama yao iko CCM'' duh kumbe mh. Na manjonjo yote yale eti Dr. Kigwangalah PhD, MD, MBA kumbe jina la uzulumati, na hii issue ya WAMA na mchongo wa stimulus package huwa anakanusha saana kumbe mnafiki mkubwa asiye hata na chembe ya aibu analambalamba lips na kurembua ktk mahojiano star tv huku ana siri ya moyoni ya kudhulumu haki ya mtoto wa maskini. Kiukweli nimeudhika vibaya eti sababu mamiyo alikuwa na wadhifa CCM ndo uibe jina???!? Na hii dhambi inakuotea mlangoni and it will destroy you. RIGHT WILL NEVER BE DENIED BUT IT ONLY DELAYED. Ole wako
 
Pukudu,

ha ha ha ha ha jamaa huwa analembua kama kungu mimi nikiambiwa mtoto si halali sitashangaa. Hivi Basha hebu tutatulie hili hata huko shule ya msingi alikuwa analembua hivi hivi kama shoga?
 
Jamani tuwe rational kidogo, hivi kwa darasa la saba kama kuna lolote lililotokea yeye Kigwangala alikuwa nafasi gani kulishawishi? Kwa umri huo ni wazi walioshiriki walikuwa ni watu wazima na yeye kama mtoto alipaswa tu kutekeleza. Lakini pia hatua kutoka primary hadi kuwa daktari ni kubwa sana, wengi tu walifaulu or rather kuchaguliwa std VII lakini hawakumaliza hata form two leo hii Hamis ni Daktari tunaweza kuhoji uwezo wake wa darasani ukizingatia mitihani migumu aliyofaulu?
 
MAKALA HII INAUKWELI MKUBWA SANA KWA BAADHI YA MAMBO, NI KWELI Dr KINGWANGALLAH ALISOMA NA BASHE, JAPO NAYE ALIKUWA ANAJULIKANA KAMA HUSSEIN MOHAMED.
JINA LA BASHE NI JIPYA PIA.
UWEZO WA BASHE SHULENI HAUKUWA MKUBWA SANA HAPO KITONGO NA HATA ALIPOKWENDA BADRI SIDHANI IWAPO ALIPATA MUUJIZA GANI HADI KUFAULU.
KINGWANGALLAH NI KICHWA HAKUFAULU LAKINI ALIKUWA NAUWEZO WA DARASANI NAKUMBUKA NIKIWA FM 4 ALIKUWA ANANIFUNDISHA BIOS NA CHEMISTRY HE KNEW THE SUBJECT VERY WELL. MUHIMBIRI NI KATI YA VYUOMakini na vigumu sana kwa mtu wa kawaida kumaliza hivyo kumalizakwake hakuna shaka japo jina aliiba.
BASHE NI MSOMALI , MGENI, WAKUJA NA SIO MWANANZEGA KWA VIGEZO VIFUATAVYO
1. UKIANGALIA KOO ZA NZEGA AMBAZO KWA KWELI ZILITOA MACHIFU NA VIONGOZI NA ZILIKANDAMIZWA NA WAZAZI WAKE BASHE. WALIKUJA KUWANYONYA WATANZANIA WAKATI WA UKOLONI HIVYO HAFAI KUWA KIONGOZI WETU.
2. BASHE AMEKUWA MTUMISHI WA MTUAMBAYE ANASIFA MBAYA TANZANIA , MAISHA YAKE YANATEGEMEA UFISADI NAHAJACHUKUA HATUA YA KUACHANA NA AMA KUMSHAURI BRO ROSTAM ABADILIKE NA KUTUONEA HURUMA AACHANE Na ufisadi YEYE ANATAKA NAFASI YA KUNYONYA ZAIDI.
NAJUA WAPO VIJANA WENGI WA NZEGA WENYE SIFA NA HAWANA HATA DOA KAMA ENG JOSEPH PIUS, JOSEPH MASSIMBA, DR REBECA SAMWEL NA WENGINE WENGI TUTAWASHAWISHI WAGOMBEE NA TUTAWAPA MCHANGO WA HALI NA MALI WASHIDE.
ASANTE BASHE KWA TAALIFA LAKINI WEWE PIA HUFAI

Habari ndugu gwaje inawezekana wazazi wa bashe waliwanyonya wazazi wenu huko nzega,bashe ninamfahamu nimesoma nae mzumbe majina yake ni Hussein Mohamed Ibrahim Bashe haya ndio majina yake na sote tulifahamu sana majina matatu 2008 tulimshauri ikiwa ni mkakati wa yeye kutafuta jina litakalo kuwa alama yake hatukulipenda jina la HUSSEIN tulimshauri atumie Jina la BASHE kwanza ni jina Tofauti,na si jina Common kwahiyo itamsaidia kujitangaza ktk siasa za uchaguzi wa 2008 hilo alifanya na jina hilo LIMEKUWA BRAND.

Hoja ya bashe kuwa na uwezo mdogo tangu nimemfahamu sijawahi kumsikia akijisifia kwamba alikuwa ana akili sana shule ya msingi tuliosoma nae mzumbe tunafahamu hilo,amekuwa kiongozi wetu kwakuwa si mjivuni.

Umewataja wana nzega wenye sifa nadhani vizuri waende nzega wana nzega wataamua kama wao wanafaa watawapa nafasi ila takwimu zilizopo zilizoonekana 2010 ni Bashe Selelii kigwangala

Nimekuwa mfatiliaji wa Mijadala Mingi hapa na bidii HK amekuwa akimtuhumu bashe kwa mambo mengi sana hata alipozomewa akasema Bashe na naamini kilichomsukuma Bashe kujibu ni Mchango wa HK wa Tar 3 june 2011 Nimpongeze,Mgogoro huu pia umekuwa ukimgusa Dk Lwaitama ambae amekuwa akimpinga sana HK.Tusipotoshe mada haina mahusiano na alicho hoji HK bungeni haya mambo yametufumbua sana macho.Nashukuru sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom