Bashe apigwa mshangao kuhusu suala la makinikia

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
HUU NDIO MSHANGAO WA HUSSEIN BASHE

"Mheshimiwa Rais, naomba naomba nikupe taarifa - tarehe 21 Julai, Mkurugenzi Mtendaji wa ACACIA ametangaza kuwa shareholders wa ACACIA hawatawalipwa gawio kwa sababu cashflow yao imepungua kwa asilimia 80% kufuatia uamuzi wako wa kuzuia makontena ya makinikia. Hivyo hawatalipwa hadi ufumbuzi wa makontena hayo utakapopatikana.

"Sasa najiuliza mbona walisema ule mchanga tu na wala hakuna thamani? Sasa iweje leo makapi yawe na thamani ya asilimia 80% kiasi cha kufanya shareholders wakose gawio?"

Mheshimiwa Hussein Bashe
Mbunge - Nzega Mjini (CCM)
(akiongea kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Tabora)

7ad5fdc0f40b6b7a6217f637ed0e940c.jpg
 
Kama Leo nilivyoshangaa maana nikienda panda treni ya gongo la mgogo kwenye kile kichwa nimeona imeandikwa <b>Made in RSA</b> sasa na yaliyokuja bahati mbaya sijui yalitoka wapi? Sijaweza piga picha sina ujasiri huo
 
Kama Leo nilivyoshangaa maana wakati nikienda panda treni ya gongo la mboto kwenye kile kichwa nimeona imeandikwa <b> Made in RSA </b> sasa na yaliyokuja bahati mbaya sijui yalitoka wapi? Sijaweza piga picha sina ujasiri huo
 
Yaani huwa hakuna unafiki mkuu kama huu wa CCM ambapo mwaka huu au miaka fulani wanatengeneza matatizo ili mwaka au miaka fulani waje kuonekana wanatatua matatizo yale waliyoyatengeneza wao wenyewe...

Yaani si ajabu hata hili la mchanga kwa sasa likawa ni tatizo ambalo CCM itataka kujichukulia ujiko wakati fulani ujao...
 
Bashe ni aina ya wanasiasa ambao wakiongea basi mwenye akili zinazojielewa lazima atasikiliza ni nini kinachoongelewa.

Siku zote ni lazima anachokiongea kiwe na substance kwa jamii nzima. Ni mwanasiasa ambaye CCM inapaswa kumtunza ili miaka michache ijayo aweze kuifaa Tanzania.
 
Yaani huwa hakuna unafiki mkuu kama huu wa CCM ambapo mwaka huu au miaka fulani wanatengeneza matatizo ili mwaka au miaka fulani waje kuonekana wanatatua matatizo yale waliyoyatengeneza wao wenyewe...

Yaani si ajabu hata hili la mchanga kwa sasa likawa ni tatizo ambalo CCM itataka kujichukulia ujiko wakati fulani ujao...
Na wewe tengeneza LA kwako ili uje ulitatue ukiingia madarakani kwani tatizo nini?
 
Kama Leo nilivyoshangaa maana nikienda panda treni ya gongo la mgogo kwenye kile kichwa nimeona imeandikwa <b>Made in RSA</b> sasa na yaliyokuja bahati mbaya sijui yalitoka wapi? Sijaweza piga picha sina ujasiri huo
Kijana hata hilo la kushangaa waluiotengeneza hivyo vichwa ni wamarekani ambao pia wamefungua brach yao south africa kwa ajili ya kuchukua Soko la africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom