Bashe amshukuru Rais Magufuli kwa kumteua

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1563733039191.png


Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kueleza kuwa atahakikisha anakuwa msaidizi mwema wa Waziri Japhet Hasunga ili kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele.

Bashe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, “Mimi niseme tu kwanza nimshukuru Rais kwa imani yake kwangu ambayo amenipa, kwa jukumu langu nimepewa kwenda kumsaidia Waziri Japhet Hasunga, kwenda kuhakikisha tunafikia malengo na matamanio ya Watanzania”.

Bashe amesema, “Hii ndiyo sekta iliyoajiri Watanzania wengi, inaendesha uchumi wa nchini inachangia asilimia 28 ya GDP na asilimia 70 ya ajira lakini ina changamoto nyingi, nina amini katika ushirikiano tutafanikiwa”
 
Hired to be fired- ndiyo hali ya sasa. Inatueleza kwa nini alikuwa wa kwanza kufanya press!
 
Picha iliyoambatanishwa hapo juu ni tofauti na muonekano wa sasa hivi wa ndugu Bashe.
Sijui kwa nini amekonda namna ile??

Kapige kazi mwanafunzi mtiifu wa Mzee wa Monduli
 
Bashe kwanza nikupe pole kabla ya pongezi, kupewa madaraka kwenye awamu hii ni kaa la moto. Kwa kuwa wewe ni kijana na upo kwenye wizara muhimu sana basi tumia ushawishi wako kwa vijana ili wajishughulishe na kilimo, usisahau kuwa this is your opportunity for pursuing your political carrier, it's a do or die.
 
Naunga mkono hoja...

Ila tu asiende nje ya mstari wa mzee baba...

Ishu ya uraia itakuwa imefungwa rasmi. Maana kuna maFisiem yalimkalia kooni sana huyu kijana. Na hivi sasa yataweka nguvu kwenye ishu ya uraia wa Kinana.

Ni swala la muda tu
Mwakani uchaguzi wapinzani wake lzm wafufue maiti
Nalog off
 
Back
Top Bottom