Bashe afuata ushauri wa Mpina aurejesha mfumo BPS kwenye Mbolea, vyombo husika vichukue hatua kwa Bashe kulidanganya Taifa

Mtumishiwetu

Senior Member
Jul 13, 2022
187
334
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Waziri wa Kilimo Leo Julai 13, 2022 amekutana kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Victoria Kwakwa kujadili maeneo ya ushirikiano kwenye IDA20.

Pamoja na mambo mengine Bashe amesema mazungumzo yao pia yamegusia Swala la bei ya mbolea, na mpango wa serekali kutoa Ruzuku kwenye msimu unaokuja wa kilimo na kuwa swala la Ruzuku kuwa Temporary measure kipindi hiki ambacho hali ya mbolea kupanda linapewa kipaumbele.

Na uamuzi Wizara kurudisha mfumo wa Bulk procurement kwenye sekta ya mbolea ili kuwasaidia wazalishaji wa ndani, jambo hili Bashe alililikataa mwenyewe Bungeni wakati akihitimisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo na Baadaye wakati wa kuhitimisha Bajeti Kuu ya Serikali na kwa nyakati zote alitumia lugha chafu za kumshambulia Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kuwa amepotosha kuhusu suala la Mbolea alipohoji kwanini Serikali iliua mfumo wa Bulk Procument na kufuta bei elekezi ya mbolea iliyosababisha wakulima kuuziwa mbolea kwa bei kubwa sana.

Leo Bashe anaungana na ushauri wa Mpina na kuufanyia kazi kwa kurejesha mfumo wa BPS ambao ulisaidia sana kupunguza bei ya mbolea huku tayari Bashe alishalihadaa Taifa kupitia Bunge kwamba Mpina amepotosha.

Mpina alitaka iundwe Tume ya Bunge kuchunguza suala la bei ya Mbolea lakini hakusikilizwa.

Ushauri wangu kama Bashe amejitokeza hadharani na kuonesha kuwa yeye ndiye alidanganya kuna umuhimu bajeti nzima ikawa imejaa mambo ambayo sio ya kawaida mfano mdogo ni huu wa mbolea

@bashehussein?

Bashe kiburi na ulevi wa madaraka unamponza sasa alichomtukania Mpina bungeni ni nini ilihali mwenzake alikuwa anamshauri jambo jema sasa hiyo aibu ataificha wapi sasa na alishawaamisha wabunge na watanzania kuwa Mpina mpotoshaji kuhusu Mfumo huo wa Bulk Procurement wa Mbolea ambao ni kweli tuliona ulivyokuwa umeleta tija sana na kudhibiti bei holela za mbolea.
 
Bei imeshuka?
huo Mfumo wa BPS aliokuwa anahoji Mpina bungeni kuwa kwanini uliondolewa? ndio ulikuwa unafanya bei ya mbolea kuwa ya uhalisia sasa wao kina waliufuta ili wawaachie rafiki zao wauze mbolea kwa bei wanayotaja sasa kwa kurejeshwa kwa mfumo huo ni wazi bei zitashuka

Msikilize Hapa Bashe

Yote kwa yote mimi kama mkulima napenda bei ya pembejeo ishuke ili tulime zaidi.
Bei ni lazima ishuke kwa sababu mfumo huo ndio ulishusha bei ya mbolea kuanzia 2017 hadi walipoufuta Juni 2021 ndio bei ikapanda hadi 140,000 kwa mfuko.
 
Bashe kiburi na ulevi wa madaraka unamponza sasa alichomtukania Mpina bungeni ni nini ilihali mwenzake alikuwa anamshauri jambo jema sasa hiyo aibu ataificha wapi sasa na alishawaamisha wabunge na watanzania kuwa Mpina mpotoshaji kuhusu Mfumo huo wa Bulk Procurement wa Mbolea ambao ni kweli tuliona ulivyokuwa umeleta tija sana na kudhibiti bei holela za mbolea.
Kiingereza kingi badala ya kusikiliza kwa makini ushauri wa wabunge huwezi kujua kila kitu siku moja na ukizingatia uwaziri wenyewe ndio kwanza ameunza hata mwaka hajamaliza ndio anaanza kugombana na wabunge
 
Ni muhimu sana kuwasikiliza wengine huwezi kujua kila kitu
 
Bashe aache ubabaishaji afanye kazi kwa kufuata misingi ya kisheria sasa yeye si alisema bungeni kwamba Mpina muongo kiko wapi sasa, Spika nakuomba umugize Bashe aje aombe radhi bunge lijalo juu ya uongo wake
 
Bashe anaponzwa na uanaharakati na sifa kubwa ya mwanaharakati na kujiona anajua kila kitu hayupo tayari kusikiliza mawazo ya mwingine kama mnabisha msikilizeni Lissu muone ukweli
 
Bashe anaponzwa na uanaharakati na sifa kubwa ya mwanaharakati na kujiona anajua kila kitu hayupo tayari kusikiliza mawazo ya mwingine kama mnabisha msikilizeni Lissu muone ukweli
 
mimi humu niliwaambia kuwa bashe ni mbabaishaji na huwa anawahadaa watu kwa kutumia kiingereza kuonesha kuwa ni smart na tabia hiyo anayo january makamba pia hawa vijana ni weupe kichwani sifa kubwa wsliyonayo ni kujiona wao ni bora zaidi kuliko wengine.
 
Mpina ni kichaa, JPM alituthibitishia kwamba wote wanaumwa ugonjwa huo wa kichaa
 
Hizi nchi za hovyo sana. Taifa linashindwa kujitengenezea mbolea ya wakulima wake, ajabu!

Jesus is LORD
 
Back
Top Bottom