Based on True Story

albab

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
1,031
1,996
Heshima kwenu waungwana.

Nikiwa na umri wa Kati ya miaka 5 mpaka 14 nilipata kuishi mkoani Tabora kwenye moja ya Kota ya shule kongwe ya sekondari iliopo karibu kabisa na kituo Cha reli (gari Moshi), hapa nilipata marafiki wengi Sanaa ambao kiukweli tulisaidiana Sanaa katika masomo kipindi hicho nikiwa primary.

Nikiwa hapa Kota tuliishi kwenye magorofa wenyewe tulipaita magorofani na baadae kuhamia nyumba za kawaida kiutoto Yale yalikua Ni maisha murua Sanaa hasa nyakati za jioni kukutana watoto wote wakota na kucheza. Japo migogoro na matusi ilikua haiishi hasa kwa wanawake ambapo Kila siku ilikua lazima nyumba flani na flani kutoleana matusi ya nguoni. Katika kipindi hicho sikujua sababu hasaa kwahiyo sikufatilia

SONGA NAMI SASA.....
Maisha ya Kota yalikua Safi Sanaa hasa kwa familia yangu Mana sikuona tatizo kubwa sanaaa ila kinachonifanya leo niandike bandiko hili kitakushangaza pia na utapata kujua mengi zaidi.

Nikiwa darasa la sita hivi tuliondoka Tabora baada ya BAMDOGO aliekua anafanya kazi shuleni hapo kuugua Sanaa hivyo hapakua na namna ila kurudishwa kwao na tatizo kubwa likiwa ni TB. Hapo nilipoteza marafiki wote kwa kukosa mawasiliano ahsante Facebook miaka kadhaa nyuma nilikuja kuwapata wengi na mawasiliano yakadumu mpaka Sasa wengi wakiwa wafanyakazi nasisi tukiganga njaa mitaani. Na hapa utamu unaanza

Katika mazungumzo mengi tumekua tukijadili maisha ya pale Kota na hapa ndipo nilipostuka kusikia idadi kubwa Sanaa ya walimu na wafanyakazi shuleni pale kuwa wamefariki hii inajumuisha pia wake wa walimu waliokua pale miaka hiyo...

Na ndipo nakuja kustuka mtandao mkubwa Sanaa wa ngono uliokuepo pale Kota kupelekea ugonjwa wa ukimwi kusambaa Sanaa shuleni pale inasikitisha kuwa familia nyingi watoto walibaki yatima baada ya wazazi wao kufariki.

Kwa haraka Kati ya mwaka 2001-2007 walimu wengi au wake zao walifariki kwa ugonjwa huu kwa idadi ya haraka si chini ya 7.

Pia katika majadiliano ndipo napata jibu kuwa ugomvi usoisha pale Kota kwa wanawake ilikua Ni sababu ya kuchukuliana mabwana au waume za watu. Inaonekana ugonjwa huu uliketwa na bwana mmoja hakua mwalimu ila.mfanyakazi flani tu.. na baada ya hapo kusambaa na kuingia katika Kila nyumba. Kwa haraka ukiacha magorofani kwa nyumba za chini Kati ya familia 7 Ni familia moja tu iliyobaki salama na Ni kwasababu huyu alikua na umri mkubwa so haikua rahisi kumuingia ukizingatia walimu wengi walikua Kati ya 30 mpaka 35 kwa umri kwa kipindi hicho huku yeye akiwa na zaidi ya 43.

Miaka hiyo hyo BAMDOGO alifariki huku Mke wake waliechana baada ya kuugua nae akifariki Miaka miwili mbele kwa ugonjwa wa UKIMWI....

Baada ya kugundua maovu ya wazazi wetu na walezi wetu tulishauriana kwa pamoja tukapime wotee japo Mimi tayari nilikua nshapima so ilibidi kuwapa moyo wengine na 2011 tulitekeleza Hilo huku wawili wakigundulika walikua na ugonjwa wakaanzishiwa dawa na mpaka Sasa jamaa wanaafya njema kabisaaa na huwezi kujua kwa kuwaona.

Sio mjuzi Sana wa kuandika ila kwa wachache waliopata kuijua hii shule wanaelewa nilichoandika na nakumbusha pia ugonjwa huu upo.

Pia huko Kota jamaani punguzeni kugegedana au jilindeni aisee inasikitisha sanaaa sanaaa.

Maandalizi mema ya sikukuu ya Idi.
 
Maisha ya kota mrundikano, ni hatari sana.

Binafsi uzao wa baba umeteketea sana kwa hii kitu mika ya 90.na hatukupata kujua watoyo wao sababu ya umri kuwa mdogo, tunakuja kufahamu siku hizi baada ya kulinganisha dalili zao na kisha kuuliza.
 
Na

Miaka hiyo asee ukimwi ulikua unaua sanaaa
 
Tbr mkoa uliokosa fursana entertainment Kwa kipindi kirefu ndio kisa cha maambukizi hayo kuwa juu si maeneo hayo tu mliokuwepo ni mji mzima wengi walitangulia mbele ya haki enzi hizo ukizingatia dawa za kupunguza makali na mwamko wa watu Kwa ugonjwa ulikua mdogo sana
Umenikumbusha hayo yalikua moja ya sehemu za kupendeza mjini... Yaani kuanzia geti la chuo cha uhazili unashuka hadi hapo Tabora Hotel unateremsha sasa Station palivutia mno enzi hizo treni ipo kila siku!Railway ilikua na nguvu na kuheshimika kweli kweli!!
 
Umenikumbusha mbali sanaaa Kaka kipindi hicho Tabora hotel tulikua tunaenda kula tende...
 
Umenikumbusha mbali sanaaa Kaka kipindi hicho Tabora hotel tulikua tunaenda kula tende...
We jamaaaa hahahahaahhaaha utajiumbua humu😂😂😂

Bila Shaka tulikua tunacheza wote pale uwanjani na kula zambarau
 
Back
Top Bottom