BASATA yamfutia Usajili Msanii Dudubaya kwa kukataa wito wake

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Baraza la sanaa limemfutia msanii Godfrey Tumaini "Dudubaya" leseni, kwahiyo hatakiwi kujihusisha tena na muziki. Mwanzoni msanii huyo alitoa kashfa tofauti kwa kutumia clips za video kwenye Instagram, sababu za kufungiwa ni pamoja na kutoa matusi, na Baraza la Sanaa lilipomwita alisema hataenda kuwasikiliza.

********

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfutia usajili Msanii wa Muziki, Godfrey Tumaini maarufu Dudu Baya kutojishughulisha na shughuli zozote za sanaa kuanzia leo Januari 07, 2020.

Baraza hilo limeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Msanii huyo kukiuka wito wa kutakiwa kufika BASATA baada ya kutoa lugha zisizo na maadili kuhusu Wasanii katika Mitandao ya Kijamii.

Inaelezwa kuwa Dudu Baya alisema ameuona wito huo na hatakwenda huku akilitaka Baraza hilo kutatua migororo iliyopo kati ya baadhi ya vyombo vya habari na Wasanii ili muziki usonge mbele.

Itakumbukwa kuwa Februari 27, 2019, Dudu Baya alikamatwa na kuhojiwa na Polisi ikiwa ni agizo la Waziri wa Sanaa, Harrison Mwakyembe baada ya kusambaa kwa video zake akionekana kumdhihaki Ruge Mutahaba.

2.jpg
 
Hii ni kutokana na msanii huyo kukataa kutii wito wa kwenda Basata kuhojiwa kutokana na matamshi yake aliyokuwa akiyatoa katika interviews alizokuwa akizifanya, na video zilizokuwa zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hivyo Basata imesisitiza, ni marufuku kwa mtu yeyote, msanii, au kikundi cha watu kufanya kazi za sanaa na msanii Dudu Baya kuanzia leo Jumanne, Jan 07, 2020, hiyo ni baada ya Msanii Dudu Baya kukaidi kufika ofisi za Basata kwa mahojiano leo saa nne kamili asubuhi.

Msanii Dudu Baya kwa upande wake amekuwa akijitetea neno alilotumia kufi..wa lipo hata kwenye vitabu vya dini, na hata viongozi wa kidini wamekuwa wakilitumia hivyo haoni kosa lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana yake hapo hata nyimbo zake kupigwa kwny tv/radio ni marufuku au?

dodge
 
hv Basata hawana ushirikiano na vyombo vya usalama, lbl msanii akiwazingua wanaenda kumbeba kama gunia la mahindi.?
 
Back
Top Bottom