BASATA wapo wapi? Wasanii wa muziki siku hizi wanaimba matusi waziwazi, tena bila uoga

ifike mahali kama taifa tuone hii hatari iliyopo mbele yetu, wasanii wa muziki siku hzi wanaimba matusi waziwazi tena bila uoga.

Hakuna aliye msafi kabisa wote wanaimba matusi tu yaani hata kusikiliza mbele ya watoto inakua ni aibu.

Je, ina maana BASATA hawaoni mambo haya? Wengine wameona kuimba haitoshi wameamua kuvua nguo kabisa na kupanda stejini kutumbuiza.

Tunaelekea wapi jamani?
Nadhani tukiilaumu basata huku asilimia 90% ya raia bado tunasapoti huo muziki basi tatizo linabakia kuwa ni sisi raia ndio hatupo sawa.

Kimsingi kama Raia wakisema ni marufuku kusikiliza mziki huo mziki ndani ya majumba na kuboycott mziki usio na maadili mazuri hapo utaona kama nyimbo itakayofuatia itakuwa na upuuzi mwingine.....
 
Na waangaliaji wakubwa wa TV ni watoto wadogo, vipindi ni hiyo miziki na wawasha TV hizo ni wadada wa kazi...

Kuna kizazi fulani cha watoto kinachotengenezwa miaka hii, in near future watakuwa wamepinda hatari...
Kwangu sitaki matumizi ya king'amuzi kabisa.

Ukiwa na watoto download programs za watoto weka kwenye external hard drive weka hapo wajifundishe.

Ukiwaachia sijui diesitivii sijui staatime utakuja kukuta watoto wote wa kike na wakiume wanacheza kigodoro tena wakiwa wamevaa madela ya mamazao
 
Biashara gani inayoharibu future ya taifa la badae?
Marekani wanavaa bikin, na nyimbo wanacheza kwa bikini miaka nenda rudi ni taifa bora, ila ss uku tz kila siku madili unashangaa kitoto miaka 10 bkr hakina, amezaa, mara watu wanapigana umber ruty men kwa men wengi sana

Huwa nashindwa kuelewa tatizo ni nn kwamba ni ulimbukeni au ndo akili zetu zinapenda matope
 
Huwa sina kawaida ya kukaa chini kuangalia tv kabisaaaaa. Kuna siku bahati mbaya nilikutana na mwanamuziki anaimba matusi hadi nikajiuliza hivi huyu ana wazazi kweli?
Tumekwama kuna shida kubwa sana hata hatujui nani wa kuja kutukwamua. Kwenye graduation za shule za msingi na sekondari wanapigiwa nyimbo za matusi na TV zetu zinabeba huu uchafu. Nakuunga mkono kuna wakati unajjuliza hivi hawa watoto sio watanzania ama.
 
Hata kama ndo mambo ya kisasa lkn Tuangalie na upande wa pili
Basata wanajitahidi kwa upande wao mkuu, video za nyimbo zisizo na maadili huwa wanatoa taarifa kwa vituo vya tv kuwa wazioneshe kuanzia saa4 huko usiku na maonyo kibao kwa vituo na wasanii kujirekebisha..

Shida ni kwa viongozi wetu kwakuwa wasanii ndio mtaji wao hutawasikia suala la maadili, shida nyingine ni sisi wasikilizaji ndio mambo tupendayo kuimbiwa, ukiimba kuhusu kilimo 'utaula wa chuya' hivyo BASATA KAZI WANAYO maana hawapati sapoti si kwa viongozi wakisiasa wala sisi wasikilizaji.
 
Wanatia kinyaa mimi bongofleva ninazosikiliza ni zile za kitambo kipindi waimbaji walipokuwa bado wanaakili.
Tena hapo ndo umenena' Bora kusikiliza muziki wa bongo kuanzia 90's mpka 2009 hivi ngoma za heshima na ndo playlist yangu. Hawa wa siku hizi hatari tupu nna jirani yangu mmoja huyo akirudi tu kwake unaeza sema ana darasa la maneno ya kishenzi humo ndani si kwa mizike yake na jumamosi tuko wote jumuiya.
 
🤣🤣🤣🤣Saivi kila kitu ni biashara, mtu anafanya ili amridhishe fulani apate pesa
Ata Ambwene Mwasongwe mkuu? Huyu ndo binafsi yangu nyimbo zake nazikubali sanaaaaaa, anaanzaga kama kastori fuln mwisho anafanya connection na masuala ya Sir God. Hakika namwelewa na nyimbo zake zina mafundisho mengi sana. But hao wengineeeeeee, sijui labda Joel Lwanga nae anafuata uimbaji wa Ambwene ila yy anaingizia biashara sanaaaa
 
Tumekwama kuna shida kubwa sana hata hatujui nani wa kuja kutukwamua. Kwenye graduation za shule za msingi na sekondari wanapigiwa nyimbo za matusi na TV zetu zinabeba huu uchafu. Nakuunga mkono kuna wakati unajjuliza hivi hawa watoto sio watanzania ama.

Unaenda kwenye mahafali ya mwanao wa std7 unamkuta anaimba. Ninogesheeee ninogesheeeee baby😥😥😥😥 Na viuno anakata🤣🤣
 
Huwa sina kawaida ya kukaa chini kuangalia tv kabisaaaaa. Kuna siku bahati mbaya nilikutana na mwanamuziki anaimba matusi hadi nikajiuliza hivi huyu ana wazazi kweli?
Kuanzia huko wasafi sjui konde ggy etc wote ni matusi

Sisi manconcious tunasikiliza hip hop tu ujumbe kwenda mbele

Lkn hao wavaa jeana znazobana wavaa vikuku mguuni ....ni big NO

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom