BASATA ingilieni kati suala la hakimiliki za biti kuondoa uchawa wa Maproducer

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
837
1,358
Sasa BASATA mnafanya kazi nzuri kuzuia au kupunguza unyonyaji wa wasanii, Sasa Kuna inshu kubwa ya hao mnaowatetea pia hao ni wanyonyaji wakubwa Sana wa Maproducer, yaani producer wamebaki chawa, ifwatwe Sheria biti ibaki Mali ya producer na Kama diamond akiuza stream mil 10 basi na lizer apate chake haloo,

Maproducer wanaogopa wanapigwa laki 2, 3,6 mchezo umeisha, tunataka maendeleo ya Maproducer.
 
Hilo swala sio la serikali bali ni producer anatakiwa kusajili beat yake awe na hati miliki.
P.funk anasajili na anazimiliki kihalali ndiyo maana aliweza kulipwa pesa nyingi kwenye ile issue ya Chamilion kuimba juu ya mdundo wake uliotumika kama sound track.
 
Kuna viTu viwili...
1. Producer anatengeneza biti lake msanii anakuja anapewa aweke vocal zake ...

2. Msanii anakuwa na wimbo wake anamfuata producer amtengenezee biti la wimbo wake!

Sasa je makubaliano yapoje?

Producer ndie anasema nitatengeneza biti (sample) kwa kiasi kadhaa na kumiX na kumaster then akilipwa chake ,

Kazi inakuwa ya mwimbaji msanii,
Ndio mmiliki wa wimbo..
Labda kama huyo producer ana lebo!
Vinginevyo producer anakuwa Ameshalipwa pesa yake before hata wimbo haujasikika kwenye media,
 
Mambo yakiwa hivyo kuna muda msanii atakua producer na hmn kitu mtawafanya ikibidi wataenda kutafuta ma producer nje ya nchi au underground na kuwafanya bora ili wafanye kazi za wasanii.

Tamaa ya kuwa juu kwa kila mtu na ya kutaka pesa huwa inaharibu nature au culture ambayo imepelekea mziki kukua na kuleta maelewano mazuri kati ya producer, msanii na menejimenti yake.
 
Wimbi la maproducer kuwa wengi imepelekea baadhi ya maproducer kujipendekeza Kwa wasanii wakubwa

Unakuta producer anamcheki msanii "oya mwanangu Nina beat Kali sn hapa wakati natengeneza nilikuwa nakuona wewe Yani" kisha msanii anakuja anaweka mistari bure kabisa,producer anachofurahia ni kusikia sign yake kwenye nyimbo ya msanii mkubwa na kufurahia pale beat alilolitengeneza limeifanya nyimbo kuwa trend

Siku hizi Hadi producers anafurahi wimbo alioufanya yeye ukiwa on trend you tub..hata hasipate kikubwa kwake poa tu
 
Kuna viTu viwili...
1. Producer anatengeneza biti lake msanii anakuja anapewa aweke vocal zake ...

2. Msanii anakuwa na wimbo wake anamfuata producer amtengenezee biti la wimbo wake!

Sasa je makubaliano yapoje?

Producer ndie anasema nitatengeneza biti (sample) kwa kiasi kadhaa na kumiX na kumaster then akilipwa chake ,

Kazi inakuwa ya mwimbaji msanii,
Ndio mmiliki wa wimbo..
Labda kama huyo producer ana lebo!
Vinginevyo producer anakuwa Ameshalipwa pesa yake before hata wimbo haujasikika kwenye media,
Hao ni producers ambao hawajitambui ndio hao wamekuwa chawa.

Ukisikiliza sana interview za p funk na masta j kuhusu hakimiliki na Sheria zake ni kuwa kila anayehusika katika wimbo anatakiwa afaidike.

Na Pia duniani kote, kama studio sio Lebo anacholipia msanii ni studio time sio beat Bali beat huwa ni mali ya producers.

Mfano mzuri ni P funk na Prof j, Prof j haikuwa kwenye Lebo ya bongo records yeye alikuwa analipa pesa wakati WA kurekodi lakini bit zote ni za p funk, ndio maana p funk alichukua pesa yote ya biti ya nikusaidieje.

Pesa anayolipa mwanamuziki Kwa producer haimfanyi yeye kuwa mmiliki WA kila kitu kwenye wimbo. Tafuta mikataba ya COSOTA uitazame.
 
Mambo yakiwa hivyo kuna muda msanii atakua producer na hmn kitu mtawafanya ikibidi wataenda kutafuta ma producer nje ya nchi au underground na kuwafanya bora ili wafanye kazi za wasanii.

Tamaa ya kuwa juu kwa kila mtu na ya kutaka pesa huwa inaharibu nature au culture ambayo imepelekea mziki kukua na kuleta maelewano mazuri kati ya producer, msanii na menejimenti yake.
Natamani waende nje ndipo watajua nini maana ya haki miliki, nje hamna upuuzi kama wanao fanyiwa maproducer wa bongo. Hii ni biashara inatakiwa win win kama wenzetu ulaya. Sio bongo msanii ananufaika huku aliye tengeneza biti hapati hata senti. Hata hao maproducer wachanga watawachoka kwani kadri siku zinavyo enda majukumu yana ongezeka, mwisho wa siku nao watataka kunufaika ubunifu wao.
 
Kuna viTu viwili...
1. Producer anatengeneza biti lake msanii anakuja anapewa aweke vocal zake ...

2. Msanii anakuwa na wimbo wake anamfuata producer amtengenezee biti la wimbo wake!

Sasa je makubaliano yapoje?

Producer ndie anasema nitatengeneza biti (sample) kwa kiasi kadhaa na kumiX na kumaster then akilipwa chake ,

Kazi inakuwa ya mwimbaji msanii,
Ndio mmiliki wa wimbo..
Labda kama huyo producer ana lebo!
Vinginevyo producer anakuwa Ameshalipwa pesa yake before hata wimbo haujasikika kwenye media,
Hapo umezungumza vitu viwili ambavyo vyote producer bado ana haki.
1.mrabaha ie producer anatengeneza muziki ambao lazima awe na sehemu ya malipo kila mahali huo muziki unapotumika kwa sababu yeye ndio mmiliki wa huo mdundo
2.kutengeneza mdundo kwenye nyimbo ya msanii ie hapa producer analipwa muda anaitumia wakati aliyengeneza huo mdundo
Kiujumla Sasa hivi Tanzania maproducer ni wachache wengi ni machawa ndio maana hata ubunifu umepungua, maproducer hawaumizi kichwa kwa sababu ya njaa na hawawezi kuwabana wasanii walipe mirabaha kwaiyo wanalipwa studio time tu, utakuta wanasample midundo online. We angalia ni wasanii wangapi siku hizi anaweza kutengenezewa mdundo na P funk au masta j maana hawa maproducer hawana njaa na wanaojitambua
 
Back
Top Bottom