BASATA, huu wimbo wenye maneno "dela jipya, chupi la zamani", haudhalilisha wanawake, na kwanini msiupigie marufuku?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Wadau, kwa wale mliosikia huu wimbo, maneno hayo kweli yanafaa kutumiwa kwa wimbo unaopigiwa katika vituo kama vya radio, kwenye daladala na sehemu nyingine za public?

Binafsi maneno hayo naona yana ukakasi na hivyo nashauri huu wimbo upigwe marufuku na ufanyiwe marekebisho ndio uruhusiwe kupigwa katika vituo vya radio at kusikilizwa kwenye vyombo vya usafiri kama daladal n.k.

Assume uko na mzazi wako halafu wimbo huu unapigwa sijui unajisikiaje( ukutu nae kavaa dela).

Huu wimbo unadhalilisha wanawake na walioutunga hawana maadili kabisa.

Nyimbo kama hizi zisiruhusiwe kupugwa kwwnye public lands vyumbani au nyumbani kwa watu wanaozipenda.

Ukweli ni kwamba, hata neno "chupi" tu wakati mwingine watu huona tabu kulitanka na badala yake hutumia maneno kama "kufuli" n.k.

Kila nikiusikia naona kero wacha leo niseme.
 
Mkuu twambie wimbo wa nani? msanii husika anaitwa nani? uhuru wa habari na maoni ndio huo..... n
 
Niliwahi kuleta uzi kuhusu huu wimbo kule jukwaa la entertainments nikaishia kutukanwa tu na magreat thinker.

Kuna nyimbo zinapigwa huwezi kusikiliza ukiwa na watoto wako, wazazi au watu unaowaheshimu.

Tanzania ya viwanda!.
Maneno ya hovyo kabisa na yanatia kinyaa kuyasikiliza.
 
May be ni kweli wimbo una maneno yasiofaa. Lakini je...wanawake wanadhalilishwa kivipi yaani?
 
Back
Top Bottom