BASATA: Diamond amestahili kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya show ya ufunguzi wa AFCON 2017

Hivi nyie nani kawaroga kwa hiyo bendera ni kwaajili ya wacheza mpira pekee au

Muelewe akiboronha pale katika uzinduzi itakua ngumu kwa mtanzania yeyote kupata nafasi ya kuperfom kwenye issue kama zile

Akifanya vizuri basi watanzania watakua n chance kubwa ya kupata fursa ya kuperfom pia

Achenk majungu acha dogo akawakilishe nchi japo kwa dakika chache wanaolalamika acheni wivu wa kike

Kama vikundi vya sanaa tu huwa wanapewa bendera za nchi sasa diamond ana kosa lipi au hana haki ipi ili asipewe
 
4130c5ed0198afab099cdc83936e60b9.jpg

utoto gan sasa hapo kafanya mkubwa fella au nn kibaya kaandike hapo
Hajaandika utoto kama alivyosema Rutashobolwa, labda amkosoe kwa uandishi mbovu but sio content ya andiko
 
4130c5ed0198afab099cdc83936e60b9.jpg

utoto gan sasa hapo kafanya mkubwa fella au nn kibaya kaandike hapo

Achana na habari za bendera hapa nimefurahi kuona uyu ndio meneja sasa katoa ufafanuzi kwani bendera bei gani mbona wale wahuni wa BBA tumewapa wakafanyie ufirauni wao mara kibao ambacho kiko wazi ni wehu wa wizara kwenye soka ambayo ni hoja kuu tumeshindwa kupeleka timu alafu mtu anaenda kwenye harakati zake binafsi tumekomaa kama muwakilishi wetu ni aibu ingekua tamasha la muziki sio kesi kabisa alafu tujiulize majirani zetu vipi au wehu huu tumefanya sisi tu.
 
Hajaandika utoto kama alivyosema Rutashobolwa, labda amkosoe kwa uandishi mbovu but sio content ya andiko
Sioni kaandika nini kibaya. Ujumbe wake umefika vema kabisa. Naamini ameeleweka kuliko hata riziwan.
 
4130c5ed0198afab099cdc83936e60b9.jpg

utoto gan sasa hapo kafanya mkubwa fella au nn kibaya kaandike hapo
Ushabiki ukizidi unakuwa zuzu team kibakuli wapi radhi kuonana domo akipondwa ila yeye akirudisha au mmoja wa mameneja wake akilitolea ufafanuzi unakuwa ni utoto yaani mpk nahisi hawajielewi siku iz awa mashabiki wa bushman
 
Achana na habari za bendera hapa nimefurahi kuona uyu ndio meneja sasa katoa ufafanuzi kwani bendera bei gani mbona wale wahuni wa BBA tumewapa wakafanyie ufirauni wao mara kibao ambacho kiko wazi ni wehu wa wizara kwenye soka ambayo ni hoja kuu tumeshindwa kupeleka timu alafu mtu anaenda kwenye harakati zake binafsi tumekomaa kama muwakilishi wetu ni aibu ingekua tamasha la muziki sio kesi kabisa alafu tujiulize majirani zetu vipi au wehu huu tumefanya sisi tu.
Unajua kipindi atakapotaka kutumbuiza atatambulishwaje kwenye stage au nn maana ya kuliwakilisha taifa ebu tueleweshe ww unaejua maana maandishi meng lkn 0 content
 
Kumekuwa na sitofamu katika mitandao ya kijamii kuhusu ni nani anastahili kukabidhiwa bendera ya Taifa ili kuwakilisha nchi, baada ya Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye kwajili ya show yake ya kutumbuiza ufunguzi wa michuano ya Afcon 2017 inayofanyikia nchini Gabon weekend hii.

Mashabiki wengi katika mitandao hiyo wamekuwa wakizozana bila kupata jibu kwamba ni kwanini Daimond alikabidhiwa bendera hiyo kwa ajili ya kuwakilisha Tanzania wakati anaenda kufanya show yake binafsi.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii kuhusu suala hilo Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza amesema bendera ya Taifa anaweza kupewa mtu yeyote ambaye anaenda nje ya nchi, na safari yake ina manufaa kwa taifa lake.

“Suala wa Waziri Nape ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ndani ya Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumkabidhi Diamond bendera ya Taifa ni jambo zuri kwa sababu ingawa Diamond anakwenda kufanya show yake lakini tukumbuke yule ni mtanzania pekee pale ambaye anakwenda kuliwakilisha Taifa lake kwa show yake mbele ya maelfu ya watu Afrika nzima, jina lake linatambulika pale lakini wao wanamtambua yule kama mtanzania na hata akifanya vizuri sifa zinaenda kwa yeye pamoja na Taifa lake,” alisema Nngereza.

Pia Nngereza alidai mtanzania yeyote anaweza kukabidhiwa bendera ya katifa kama anaenda kufanya tukio lolote ambalo linaweza kuipatia sifa nchi yake kwa namna yoyote.

“Mtu yoyote ambaye anaenda nje ya nchi kwa ajili ya matamasha makubwa au kama kuna namna ambavyo anaenda kufanya kitu ambacho kimpatia yeye faida pamoja na Taifa lake anaweza kukabidhiwa bendera, awe mtanzania tu. Kwa hiyo hata ukiwa mtangazaji, mchezaji, vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali wanaweza kukabidhiwa bendera kama wakihiitaji kwa sababu kuna wengine hawatoi taarifa kuhusu matukio yao lakini kama ukitoa taarifa na mamlaka ikaona kuna umuhimu wa kufanya tunafanya hivyo kwa sababu ni kwa ajili ya taifa letu,”

Nchi hii imejaa liwa mambo ya ajabu.
 
Hawezi kupewa bendera msilazimishe makosa. Labda aje msemaji wa ikulu au protocali wa serikali kueleza hili jambo.
Diamond amepewa nafasi hio kwa malipo. Amealikwa kutumbuza sio kuiwakilisha Taifa katika kutumbuiza...amealikwa kibinafsi kama msanii.
Sio kweli kila mtu anapewa kama anavo sema huyu Basata. Wamekosea wakubali makosa pale hakuna bendera ya tanzania itapeperushwa tusidanganyane....
 
Riziwani amesema ukweli bila kupepesa naye ameanza kujielewa, daimond kupewa bendera ni sawa ila na Hao tsifa stars walipaswa wawepo kwenye kukabidhiwa bendera
 
Naona wengine wanaicheka Taifa Stars kwa kuishambulia TFF japo hakuna anayesema tumeenda mara ngapi huko katika miaka 35 iliyopita.
Nimeona uzi hapa juu ya Millard Ayo kuwa mtangazaji wa mashindano hayo lakini sijaona anayeuliza tratibu za kumpata zilikuwaje na alishindanishwa na nani! >>>CAF yamteua Millard Ayo kuripoti moja kwa moja michauno ya AFCON2017 kutoka Uwanjani
Tusichoelwa ni kuwa wenye akili zao wako kwenye biashara na sisi tunaingia kwenye kuwafanyia promo bila hata kung'amua.
Hebu angalia hiyo picha ya kukabidhi bendera, kuna banner ya DSTV ambao nao wanadhamini mashindano hayo. Kwa hiyo lililo wazi ni DSTV wanamtumia waziri kuboost biashara zao. Kumbuka wakati Mbwana Samatta anaagwa kilichoonekana kwenye background ni nembo za serikali tu! Kwa lugha nyepesi mnadhani waziri ndiye aliorganize hii au DSTV ndio waliorganize na 'kumtumia' waziri!?

Hii ni ngoma ya DSTV katika kupenya soko la bongo hivyo tufurahie kwa staha, tusipostuka tutaendelea kutumiwa hadi mwisho wa dunia.
 
Imba na wewe tukusikie!
Kama kweli unaujua muziki tena kwa jicho la tatu. Domo anaruka ruka tu. Huwezi kumcompare na TID Grace Matata n the likes. Jiulize kwa 'levo' ambazo Team yake inamuweka ambazo hastahili kabisa, kwanini hana band mpaka sasa. At least katika show fulani fulani afanye kitu tofauti.
Angalia acha kutazama.
 
Fella hajui kuandika. Manager wa Diamond. Ndiyo maana aliamua kumtafuta SK vinginevyo angekuwa bado hajatoka kimataifa
 
Kama kweli unaujua muziki tena kwa jicho la tatu. Domo anaruka ruka tu. Huwezi kumcompare na TID Grace Matata n the likes. Jiulize kwa 'levo' ambazo Team yake inamuweka ambazo hastahili kabisa, kwanini hana band mpaka sasa. At least katika show fulani fulani afanye kitu tofauti.
Angalia acha kutazama.
Hater!!
 
Hawezi kupewa bendera msilazimishe makosa. Labda aje msemaji wa ikulu au protocali wa serikali kueleza hili jambo.
Diamond amepewa nafasi hio kwa malipo. Amealikwa kutumbuza sio kuiwakilisha Taifa katika kutumbuiza...amealikwa kibinafsi kama msanii.
Sio kweli kila mtu anapewa kama anavo sema huyu Basata. Wamekosea wakubali makosa pale hakuna bendera ya tanzania itapeperushwa tusidanganyane....

Kabisa diamond anawakilisha DSTv wahindi wamwache za akili matangazo Yao wanatupia nchi watanzania amkeni
 
Back
Top Bottom