BASATA: Diamond amekosea kumjibu Naibu Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo, Julianza Shonza

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,759
diamond+pic.jpg




Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.

Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Machi 21, 2018, Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.

Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.

Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.

Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.

Katika malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.

Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.


Chanzo: Mwananchi


Soma hapa Diamond aliyosema;

Diamond arudisha dongo lingine kwa Naibu waziri wa Sanaa Juliana Shonza


Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond

 
Hahaaaaa wamfungie basi kama uwezo wanao hahahaha hapo mmegonga mwamba, endeleeni kupiga majungu lakini Kwa Diamond mtajisumbua
 
Mvimbisheni kichwa. Manji kanyooka sembuse yeye. Hivi hiyo tv yake minara iko kwenye makazi ya watu haina mionzi kweli?
Manji na Diamond hawafanani kabisa........ Na katika hizi case 2 ni sawa na kusema Diamond ni + ve na Manji ni - ve.......utaelewa baadae!
 
Chui anapoona swala wawili wanapigana hutulia na kuutumia vizuri mgogoro huo ili kupata kitoweo, mimi nashauri diamond afungiwe kufanya usanii milele hapa Tanzania
 
Kabla hamjatoa hayo matamko nyie Basata jiulizeni nyuma ya Diamond yupo nani. Mtashangaa mnatoka povu then mwisho wa siku mkuu wa nchi anamwambia Diamond big up. kama mnabisha subirini siku Diamond atakapoenda kuaga ikulu kwa safari yake ya World Cup
 
Kwa Mujibu wa maneno ya Diamond, Mdada Shonza alitakiwa ama aende Madale kwa Dai wakajadili hiyo issue, Yani Dai kishajiweka level Ya Waziri kamili, Na kwakuwa yupo na Mlezi wake Madereva, basi kachukua tabia za Madereva( Kumbuka huyu Madereva ni mlokole anasali kwa pasta Onesmo Ndegi , ila kawa mpinga Kristo kwa kujenga msikiti Kinondoni kwa hela A walipa kodi, pia anadhamini Show za Dai ambaye ni free Mason)

Onesmo Ndegi wa Living Water haambiliki kwa Madereva, ye anaangalia fungu la 10 tu.


Hii nchi makanisa yanebaki ya TAG, ROMA, Lutheran, KAKOBE, SABATO NA GWAJIMA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom