BASATA, COSOTA na Bodi ya Filamu kuunganishwa. Wadau waitwa kutoa maoni yao

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya awamu ya 5 yaja na mageuzi makubwa katika Sekta ya Sanaa na Ubunifu. Mkakati kuundwa mamlaka moja kusimamia sekta hii waanza

Katika kuboresha na kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Sanaa na Ubunifu (Art and Creative Industry) na kusogeza huduma kwa Wasanii na Wabunifu serikali ya awamu ya tano iko katika mchakato wa kuziunganisha taasisi zinazoshughulika na sekta hii na kuunda mamlaka moja. Taasisi hizo ni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Bodi ya Filamu na Chama cha hakimiliki na Hakishiriki (Cosota).

Kwa msingi huu Wasanii wa aina zote wakiwemo watunzi na waandishi mbalimbali, wabunifu, Waandishi wa habari na wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa katika mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Innocent Bashungwa utakaofanyika Siku ya Jumatano, Tarehe 28/08/2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 Asubuhi.

Mbali na kujadili mchakato wa uundwaji wa mamlaka moja ya kusimamia sekta ya Sanaa na Ubunifu kutakuwa pia na mazungumzo ya gawio la mirabaha kwa kazi za Wasanii wa muziki.
 
BASATA must stand alone! wheather you like or not!
::-hivyo vyama vingine vibakie kuwa wadau na washauri wa basata.
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Bodi ya Filamu na Chama cha hakimiliki na Hakishiriki (Cosota).


Huwa najiuliza sipati majibu, zile movies wanazo play kwenye mabasi zikiwa kwenye flash disk zina hati miliki mbona suala la copying halidhibitiwi na wasanii kukosa gawio lao?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom