Mlalahoi Mlalahai
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 399
- 146
Kutokana na sisi watu wengi ambao tunatafuta kazi, kupaswa au kutakiwa kutuma maombi mengi kadri iwezekanavyo sababu haijulikani hasa ni wapi na lini utapata kazi. Shida huwa inakuja pale ambapo baadhi ya maombi hutakiwa yatumwe kwa njia ya POSTA, ni vigumu kwa tulio wengi kutumia njia zenye gharama kama EMS, kwa kila ombi la kazi hivyo tunalazimika kuitumia ile njia ya bei nafuu yaani ile ya kawaida. Sasa kitu ambacho mimi huwa najiuliza, mtu anayetuma barua ya maombi kwa njia ya kawaida na yule anayetuma kwa EMS barua zao ukiachana na kwamba wa EMS itawahi, je zote zitasomwa na kuzingatiwa au aliyetumia EMS hupewa upendeleo maalum sababu ametumi gharama kubwa? Na je ikiwa waliotumia njia ya kawaida barua zao zikawa nyingi na kuifikia ofisi kwa muda muafaka, zitasomwa zote au wanafanya Sampling tu?