Barua za kuwang’oa kina Lowassa zakamilika; Yadaiwa ziko mezani kwa Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua za kuwang’oa kina Lowassa zakamilika; Yadaiwa ziko mezani kwa Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  source; Tanzania Daima

  na Mwandishi wetu  Barua za makada watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Azizi, Edward Lowassa, na Andrew Chenge, za kuwataka wajiondoe katika nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, ziko tayari.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umethibitisha kwamba makada hao, waasisi wa mtandao uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani mwaka 2005, wanaweza kupokea barua zao wakati wowote kuanzia leo Jumatano.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, barua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) iliyomaliza kikao chake hivi karibuni mjini Dodoma.

  Inadaiwa makada hao maarufu na wenye ushawishi mkubwa ndani ya nje ya chama hicho tawala, walipewa siku 90 tangu siku ya kikao, wapime wenyewe uzito wa kashfa zinazowakabili na wajiengue kwenye nafasi za uongozi, vinginevyo chama kitawaengua katika kikao kijacho cha NEC.

  “Barua za Lowassa, Chenge na Rostam ziko tayari, na suala lao liko mikononi mwa Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama. Wiki hii watakabidhiwa,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya CCM.

  Pamoja na mambo mengine, barua hizo zimeorodhesha tuhuma zao na kurejea maazimio ya NEC yanayowahusu.

  Alipohojiwa na Tanzania Daima Jumatano juu ya barua hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alithibitisha kwamba tayari barua hizo zimeshaandaliwa. Naye alisema watakabidhiwa barua hizo wakati wowote kuanzia leo Jumatano.

  “Kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa maazimio ya NEC, si jambo geni. Ninachojua, tulikuwa tunasubiri mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka yapite, kila mtu ale Pasaka yake,” alisema Nape.

  Wakati barua hizo zikisubiriwa kwa hamu, baadhi ya makada wajumbe wa NEC wamekaririwa na vyombo kadhaa vya habari na katika mazungumzo yasiyo rasmi wakisema hakukuwa na azimio lolote lililopitishwa la kuwataka makada hao wapewe siku 90 za kujiengua. Vilevile, wamekanusha kuwapo kwa azimio lolote la kuwaandikia barua.
  Hata hivyo, Nape amekuwa akisema kwa waandishi na katika mikutano ya hadhara kwamba NEC ilitoa azimio hilo. Baadhi ya makada wasiokubaliana na kauli za Nape, katika hali ya kuwaonea huruma au kuwatetea watuhumiwa, wamekuwa wakidai kwamba kauli za Nape zimetoka nje, si ndani ya kikao cha NEC.

  Lakini baadhi yao wamekuwa wakidokeza kuwa si rahisi Nape kujitungia maneno makali ya aina hii, huku wengine wakisema anatumwa na wakubwa “kuwashughulikia” kina Rostam.

  Katika kujaribu kuthibitisha kwamba Nape anazungumza jambo lisilotokana na maazimio ya NEC, baadhi ya makada wanakumbushia kauli za hivi karibuni za mtangulizi wake, John Chiligati, ambaye amepata kutaja mara kadhaa taarifa zisizosahihi za maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na NEC, tofauti na kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo.

  Wanasema, kwa mfano, Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kuilipa au kutoilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai TANESCO shilingi bilioni 94.

  Vilevile, wanasema Chiligati aliwahi kutoa maazimio ya kupotosha aliposoma maazimio ya NEC kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Hata hivyo, Nape anasisitiza kuwa kauli yake ni ya chama na inatokana na maazimio ya NEC. Katika mikutano ya hadhara inayodaiwa ni ya kujitambulisha, amekuwa akisisitiza kwamba Lowassa, Rostam na Chenge wametakiwa kujiondoa kwenye ujumbe wa NEC ndani ya siku 90, vinginevyo watang’olewa kwa nguvu.

  Ndiye pia aliyesema kwamba wataandikiwa barua za kuwaorodheshea tuhuma zao na kuwataka waondoke kwenye uongozi wa chama. Hata hivyo, hakuna kiongozi hata mmoja aliyesema kama makada hao watavuliwa pia ubunge.

  Lowassa ni Mbunge wa Monduli, Chenge anawakilisha jimbo la Bariadi Magharibi, na Rostam Azizi ni mwakilishi wa Igunga.

  Wadadisi wa mambo ya siasa wanasema kilichotokea mjini Dodoma ni muendelezo wa minyukano ndani ya CCM na kwamba hoja kuu inayosababisha haya si ufisadi, bali urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hasa kwa kuwa baadhi yao wanasemekana wanatamani kugombea au kuunga mkono baadhi ya wagombea.

  Nguvu yao ya kifedha na ushawishi wao ndani ya chama ni baadhi ya mambo yanayoogopwa na washindani wao ndani ya chama tawala. Ingawa wote watatu wamekuwa watu wa karibu sana na Rais Kikwete, habari zinasema kumekuwapo na taarifa za kuchongeana miongoni mwao, zikichochewa na makachero wanaomwaminisha Rais Kikwete kwamba sifa yake iliyopotea mbele ya jamii inaweza kurudi iwapo ataondokana na watatu hao.

  Rais Kikwete naye anatumia ushauri huo kama fursa ya kurejesha matumaini ya wananchi kwake na CCM, akitumia kaulimbiu ya kujivua gamba.

  Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wakosoaji wa Rais Kikwete wamesema kujivua gamba kunakofanywa naye ni unafiki mtupu, kwani kama lengo ni kupiga vita ufisadi, naye yu miongoni mwa waliotajwa kwa ufisadi pamoja na Chenge, Rostam na Lowassa.

  Baadhi ya makada wamesema kwamba kama CCm inaazimia kuondoa mafisadi, basi kiwaondoe viongozi wote waliopatikana kwa pesa za kifisadi za EPA.

  Katika orodha ya viongozi waliofaidika na ufisadi wa EPA, anatajwa pia Rais Kikwete, kwa maelezo kwamba pesa hizo zilitumika kununua kura ili ashinde.

  Wanasema hata kuvunja Kamati Kuu na kuingiza wajumbe wengine hakukusaidia kuisafisha, kwani walioingia ni wachafu kama waliotoka, maana historia zao na wasifu wao vinafahamika. Wengine wanakwenda mbali na kusema kwamba iwapo Rais Kikwete atatekeleza azima yake hii, atakuwa anaandaa anguko lake lisilotarajiwa, maana atakuwa anaongeza idadi ya maadui miongoni mwa watu wanaomjua vema, waliomjenga na kumsaidia hadi hapo alipo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wakitekeleza hii mission watajuta ndani ya muda mfupi sana, maana mfumo wa kujivua GAMBA haukufanyiwa utafiti...mkulu alijisemea tu bila kushirikishana na pannel za chama!
  Lets sit back and watch every bit of these tantalizing episodes!
   
 3. z

  zamlock JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yan mimi naona mpaka saizi wamechelewa kutoa barua ili chama kife kabisa
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  PJ........ wavue wasivue majuto makuu yapo palepale
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  kama nape atamkabidhi lowassa in person,.lowassa ataichanachana vipande na kumtupia usoni na kumwambia akashtaki kwa jk na jk hatafanya kitu.Hapa ni maigizo tu yanafanyika,nnauye na msekwa wanajua kuwa wanawazuga watu..mapacha watatu ni untouchable even the president himself fears them..this movie will end like this"they lived happily ever after"
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hizo barua zinaandikwa kwa magreda?
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo ina Maana majimbo matatu yatahitaji Wabunge Wapya? Hurray CHADEMA !!!
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  CCM wanatapatapa tu.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,417
  Trophy Points: 280
  hakuna barua wala nini, hizi ni longolongo tu
   
 10. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Barua kwa Msekwa?

  Kwanini Msekwa na siyo Kikwete!

  Kansa ikivuka kiuno sijui kama unaweza kukata kiwiliwili, CCM inasubiri kufa au imekufa inasubiri kuzikwa!

  Siku ya kufa nyani kila mti unatereza, alijaribu kushika mti wa udini naona umetereza, akashika mti wa sijui, Dowans sijui, Richmond sijui, umetereza, akashika mti wa udikteta na kuzuia maandamano kwa mahuaji umetereza, akashika mti wa CDM wanafadhiliwa kuvuruga amani yetu tuliyoachiwa na Baba wa Taifa umetereza!

  Hivi CCM Baba wa Taifa aliwaachia amani peke yake? au mnataka kusema aliwaachia na Ufisadi! Mbona hata hotuba za Nyerere kati ya mwaka 995 hadi mauti yanampata inaonekana hamzisikirizi wala hamzielewi!
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  SOURCE: TZDaima!
  Guy, sikumbuki hayo ya kuandikiana barua kama ilikuwemo kwenye maazimio ya NEC?
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo Hamna kitu ni usanii ambao haukuratibiwa vizuri ila kwa pupa ya kuchanganyikiwa. Halafu wanakuja watu na theory za ajabu eti chama kimeimarika baada ya kujivua gamba hivyo wanafungua tawi New York city wakati tawi la hapa jirani yangu mtaa wa pili limekufa? CCM haiwezi kuendeshwa na matawi ya London na New York wakati ya Nyumbani yanakufa. Tusidanganyane.
   
 13. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Source: Tanzania Daima, hahahaaa.... the established Lowasa and Rostam spin doctors.... mtaspin sana, ila mabwana zenu lazima watoswe mwaka huu. Kibanda roho inamuuma kitumbua chake kina Nape wanataka kukitia mchanga, alijua between now and 2015 kazi ya kuwaremba Lowasa na Rostam kwenye Tanzania Daima angejenga hekalu la maana, angevuna mamia ya mamilioni kwa malipo yake na kitengo cha Salva ikulu kilikua chake mambo yakikubali...no wonder toka mambo yabadilike CCM, amekua analialia tu...na wapambe wao wengine...njoo na stori ingine basi, ehe Tanzania nayo itameguka Lowasa akikosa cheo, au vitazuka vita vya civil war tusipompa urais?... Wenzako kina Guninita washaanua matanga baada ya kusoma upepo. Habari ndiyo hiyo....
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,844
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Usilolijua ni sawa na usiku wa giza, unachokitaka ndicho tunachokitaka tena waharakishe wamechelewa kuwatosa baada yakuwatosa tunageuka tena mmewaonea teh teh teh.
   
 15. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  No, kwa matone ya wino kutoka pluto.
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii habari uliidaka kabla haijawa printed? Maana naona habari ya gazeti la leo Jumatano uliiandika jana Jumanne!
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Mazingaombwe haya ni matokeo ya mfumo hafifu wa kisiasa aliotuachia Nyerere hasa pale alitamka yale maneno kuwa kiongozi mzuri lazim atoke CCM. Inamaa CCM wakimasimaisha Lowasa basi atakuwa ni kiongozi mzuri, wakimasimamisha Rosatma, basi walaa. Halafu CCM kimekuwa chama kinyonge sana mbele ya watu hao wa vijisenti walivyotuibia. Ningekuwa na uweo wa kuingia madarakani, wote wangeishia kule kunakohusika bila kuchelewa. Sheria za rushwa ziko wazi kabisa ila akina Hosea wanaogopa kuzitumia.
   
 18. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wasiwasi wangu nani atasalimika katika vita hii sina hakika sana na usalama wa JK ndani ya chama kwani hao wanaopewa barua ndio waliomweka pale na 75% ya watoa maamuzi ya chama ni wanaolipwa mshahara na EL na RA.sijui naomba iwe mapema zaidi kushuhudia CCM ikivunjika nami bado sijazeeka nitawasimulia wajukuu zangu kuwa kulikuwa na CCM YA MAFISADI .
   
 19. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni muendelezo wa porojo tu,jana nimemuona white hair sijui kama alimpa mkono mzee wa kaya alipowasili,huu ujasiri hiki chama cha maiti aka magamba hawana,kama walishindwa kuwafukuza huko walipokaa ndio wataweza kuwaandikia barua sasa?:lying::lying::lying:
   
 20. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama hili ni la kweli!!
   
Loading...