Barua yangu ya wazi kwa Mwanafunzi Chuo Kikuu Tanzania

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Mpendwa mwanafunzi,

Natumaini kuwa u buheri wa afya, na ni imani yangu kuwa unaendelea vizuri na masomo yako. Kama unaokumbana na changamoto kitaaluma na kijamii pole sana, naomba Mungu akupiganie.

Leo sina mengi sana, ila naomba nikukumbushe tu ile hela unayopewa na serikali yako ya kujikimu (malazi na chakula) itumie vizuri. Jibane kadri uwezavyo ili badae usijekutulaumu.

Najua unajua hali iliyopo sasa nchini, kama hauna konekisheni, ajira utaisikia tu kwenye redio na kuiona kwenye runinga.

Wenzako waliotunza huo mkopo, sasa angalau wamejiajiri, wapo wanachoma mahindi, wapo wanashona nguo, wapo wanauza nguo za mtumba, n.k.

Hata mimi najua, unasoma kozi za sayansi, ila nachokuambia ni ukweli mtupu. Kama huamini, nenda, Uhuru sekondari skuli, yenye wanafunzi 1000 na kidogo ila ina mwalimu mmoja wa baiolojia. Au nenda kituo cha afya cha Tanzania Mpya, chenye majengo mapya manne lakini kina wauguzi wawili tu na daktari mmoja mwenye dispensary yake.

Sawa, we kama utajitolea JKT ni juu yako, ila kumbuka kuna watu walijitolea, leo tupo nao mtaani tunaangaika nao kulisukuma tairi la maisha.

Usidhani, Clara na Johnson walibahatisha, naomba ukumbuke kuwa mjomba wao ni Kanali wa Jeshi. Na yule Sophia alipewa kazi kwa sababu like shirika la dhehebu lake la Wasabato.

Najua una GPA ya 4.2 ila si unamkumbuka Jakob mtoto wa mzee Isaka? Achana na Jakobo kada wa chama, yule mwenye gari na nyumba nzuri. Namzungumzia Jakob kichwa, yule dogo aliyekuwa kichwa toka primary, dgo ana 4.5 ya UDSM ila siku hizi anahudumia kwenye mgahawa wa shangazi yake.

At least wewe ni Mhaya, kidogo unaweza pata nafasi pale St. Shomile Schools, ila usipategemee sana maana hali haitabiriki.

Mi mwenyewe, vyeti vyangu ni A',s na nina uwezo mzuri wa ufanisi, ila ndio hivyo, niliokuwa nawafundisha chuoni, wameajiriwa, yule Ruth, girlfriend wangu na yy ameajiriwa na yule jamaa niliyemfumaga nae amasema ni kaka yake.

Najua hujui kuhusu Hussein yule mwenye shahada ya sheria ya UDSM, yupo anarusha miziki. Yule John engineer wa St. Joseph yupo stationary ya Venny anatoa copy.

Ila nashukru Mungu nimepata nafasi ya kujitolea hpa nalipwa 60,000 kwa mwezi. Na chai ya asubuhi napewa.

Halafu naomba kama una kabalance kidogo unitumie mdgo wangu, nifate cheti changu chuoni, niombe scholarship ulaya.

Wako,
ALUMNI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila tuache utani kusoma mpaka chuo kikuu bila kuwa na connection nikujitakia kupata BP bule.Mm ndugu yangu akitaka kwenda uko nitamshauri Bora kwenda NIT akajifunze udereva au ufundi. Kidogo waliosoma IT na computer science ni wepesi kujiajiri lakini hizi fani tulizo soma sisi sijui procurement and supply Management au Human resources management walai utatafta kazi mpaka miguu iote sugu.
 
Chuo tunafundishwa kupata degree,hawafundishi maisha Baada ya wewe kupata degree.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ila tuache utani kusoma mpaka chuo kikuu bila kuwa na connection nikujitakia kupata BP bule.Mm ndugu yangu akitaka kwenda uko nitamshauri Bora kwenda NIT akajifunze udereva au ufundi. Kidogo waliosoma IT na computer science ni wepesi kujiajiri lakini hizi fani tulizo soma sisi sijui procurement and supply Management au Human resources management walai utatafta kazi mpaka miguu iote sugu.
B

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu ila kuna kitu kinaitwa bahati kila mtu anabahati yake katika maisha pia 80% ya graduates hawapo competent kabisa kuweza kukabidhiwa kazi katika taasisi au kampuni nyingi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa mwanafunzi,

Natumaini kuwa u buheri wa afya, na ni imani yangu kuwa unaendelea vizuri na masomo yako. Kama unaokumbana na changamoto kitaaluma na kijamii pole sana, naomba Mungu akupiganie.

Leo sina mengi sana, ila naomba nikukumbushe tu ile hela unayopewa na serikali yako ya kujikimu (malazi na chakula) itumie vizuri. Jibane kadri uwezavyo ili badae usijekutulaumu.

Najua unajua hali iliyopo sasa nchini, kama hauna konekisheni, ajira utaisikia tu kwenye redio na kuiona kwenye runinga.

Wenzako waliotunza huo mkopo, sasa angalau wamejiajiri, wapo wanachoma mahindi, wapo wanashona nguo, wapo wanauza nguo za mtumba, n.k.

Hata mimi najua, unasoma kozi za sayansi, ila nachokuambia ni ukweli mtupu. Kama huamini, nenda, Uhuru sekondari skuli, yenye wanafunzi 1000 na kidogo ila ina mwalimu mmoja wa baiolojia. Au nenda kituo cha afya cha Tanzania Mpya, chenye majengo mapya manne lakini kina wauguzi wawili tu na daktari mmoja mwenye dispensary yake.

Sawa, we kama utajitolea JKT ni juu yako, ila kumbuka kuna watu walijitolea, leo tupo nao mtaani tunaangaika nao kulisukuma tairi la maisha.

Usidhani, Clara na Johnson walibahatisha, naomba ukumbuke kuwa mjomba wao ni Kanali wa Jeshi. Na yule Sophia alipewa kazi kwa sababu like shirika la dhehebu lake la Wasabato.

Najua una GPA ya 4.2 ila si unamkumbuka Jakob mtoto wa mzee Isaka? Achana na Jakobo kada wa chama, yule mwenye gari na nyumba nzuri. Namzungumzia Jakob kichwa, yule dogo aliyekuwa kichwa toka primary, dgo ana 4.5 ya UDSM ila siku hizi anahudumia kwenye mgahawa wa shangazi yake.

At least wewe ni Mhaya, kidogo unaweza pata nafasi pale St. Shomile Schools, ila usipategemee sana maana hali haitabiriki.

Mi mwenyewe, vyeti vyangu ni A',s na nina uwezo mzuri wa ufanisi, ila ndio hivyo, niliokuwa nawafundisha chuoni, wameajiriwa, yule Ruth, girlfriend wangu na yy ameajiriwa na yule jamaa niliyemfumaga nae amasema ni kaka yake.

Najua hujui kuhusu Hussein yule mwenye shahada ya sheria ya UDSM, yupo anarusha miziki. Yule John engineer wa St. Joseph yupo stationary ya Venny anatoa copy.

Ila nashukru Mungu nimepata nafasi ya kujitolea hpa nalipwa 60,000 kwa mwezi. Na chai ya asubuhi napewa.

Halafu naomba kama una kabalance kidogo unitumie mdgo wangu, nifate cheti changu chuoni, niombe scholarship ulaya.

Wako,
ALUMNI

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww acha tutumie boom bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi wangapi wanaajiriwa
 
Nasoma na watu wanafaulu sana ila natafuta akili wanakozitoa nakosa. Uwezo wa kujieleza hana, mambo ya kawaida mno kijamii hajui, kujenga hoja ikaeleweka hawezi ila ukimpa test ya alichosoma anafaulu vizuri tu. Mimi nipo napuyanga kwenye masomo hakuna course work nimezidisha 25/40.
Sasa napata wakati mgumu sana kuelewa akili ni nini, na maisha ya mtaani yanataka nini. Je yanataka ufaulu masomo kwa GPA kubwa uajiliwe ukafie uko au uwe na akili za kuchanganua mambo ufaulu kiasi ukapambane mtaani. Connection hizo ninazo. Mkopo sina ila napambana wala sifi njaa kivile. Niwekee mwongozo.
Kesho nina UE ngoja nikasomesome kujikumbusha.
 
Back
Top Bottom