Barua yangu kwa mh rais Magufuli. Nimeguswa...

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
salaamu,
Natumai umzima wa afya, mungu akuongoze uione haki uifate na uione batili uiepuke.
Mh rais, naomba usome barua yangu na uifanyie kazi na kama itakufaa siku utakapo toa hotuba usisahau kuyatolea ufafanuzi

1. Bomoabomoa nchi nzima.
mh rais nakuunga mkono kubomoa nyumba zote zilizopo mabondeni na sehemu hatarishi. Nakuomba mh. rais kwa taadhima, kwanza kabla ya kuvunja ungeteua tume ifanye tathmini,kisha yafanyike mojawapo au yote mawili , kuwalipa fidia kidogo,au kuwatafutia viwanja mbadala kisha waelekezwe kwa msaada wa serikali kwenda huko kwani lengo sio kuwakomoa Bali kuwanusuru. tambua mh rais mpk MTU anagoma au anabaki bondeni si jeuri Bali ni umaskini wa kutupa tulionao.mh rais nimesema uunde tume kwani watendaji wanasema wametupa viwanja mabwepande lakini ukweli tuliopewa ni wachache. sikiliza kilio cha mnyonge, usifanye kama ilivokuwa kuanzisha vjiji vya ujamaa ambapo amri zilitawala busara.

2 Ruhusu mchakato wa katiba uendelee.
mh rais kwa kuwa serikali huundwa na watu na mifumo nakuomba mh rais umestukiza vya kutosha,umefukuza vya kutosha,umepeleka watu kortini sasa mh rais tumeona dhamira yako, tumeona nia yako, sasa jenga mfumo Tanzania itakukumbuka ,afrika itafahamu,dunia itajifunza.
mfumo ni katiba utaeleza maadili ya viongozi,utapunguza nguvu za rais, mawaziri kupitishwa na bunge, kuwa na wagombea binafsi,time huru ya uchaguzi nk. mh rais kama utapenda rudisha rasimu ya warioba kisha tafuta watu wasio wabunge ndio wawe wajumbe na wasiofungamana na upande wowote.
mh rais hakuna kiongozi aliefanikiwa kwa kuwa na dhamira pekee bila mfumo. mfumo utawakataa wezi,mafisadi,upendeleo, na utaweka namna unavofaidika na rasilimali zako na kila MTU ukiwemo wewe utakuwa accountable kwa vitendo vyetu.

3. Usionyeshe ukali sana kwa wafanyabiashara.
nakuunga mkono kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wasiolipa kodi,lakini mh tambua wengi wanakwepa kodi kwa kuwa urasimu uliopo hawapati faida. mh unatakiwa kufanya research katika hili ni wazi kariakoo tayari wafanyabiashara wanalia hali imekuwa ngumu. mh liangalie kwa umakini ukizidisha ukali Bali punguza mlolongo wa kodi ambazo huongeza shida kwa wafanyabiashara wadogo.

5.Badala ya viwanda imarisha kilimo na umeme
mh rais napenda nchi yetu iwe na viwanda na ulipigania sana kwenye kampeni,lakini mhvrais unampenda mungu viwanda kwa hii miaka mitano naona ni suala zito, wafanyabiashara wengi wamepata hofu, wengine wanasikilizia nini kitawatokea siamini watatoa mabilioni yao kuweka kwenye risk, mpaka sasa umeme haueleweki unakatikakatika, kilimo kipo chini, mh rais postpone suala la viwanda imarisha kwanza nishati iwe ya uhakika ili watu wengi km kina dangote wavutike,kisha kilimo hubeba 80% ya watu kikiimarika utakumbukwa daima.
mh umesoma chemistry, hata Mimi nilisoma tunaamini katika practical zaidi kuliko theory. mh rais Tanzania kuwa katika viwanda bila kuwa na nishati ya uhakika na nafuu ni. theory, pia viwanda bila kilimo Tija,yani quantity n quality ni theory.

HYPOTHESIS WITHOUT SCIENTIFIC EXPERIMENTATION IS NULLFIED
nisamehe mh rais pale nilipokosea, au utakapoudhika kwa ukosoaji.

WASALAMU.
 
Ujumbe na ushauri mzuri hata kama si yote ila ya msingi ni mengi
 
Ngoja nitulie kwanza ndiyo nikomenti maana mambo mengine bhana unatakiwa kuwa kama mbuzi unakula kwanza baadaye unacheua taratibu na kumeza
 
mh magufuli, hivi unabomoa nyumba je umefikiria haya
1 aliepeleka maji unamwachaje?
2 aliepeleka umeme unamwachaje?
3 mkuu wa wilaya alefumbia macho wakijenga unamwachaje?
4 katibu mkuu alieona unamwachaje
5 na wengine wengi walioona kwan nyumba zikijengwa zinaonekana wazi kwann stop order na vijiko havikufanya kaz mpk hivileo.
 
Kashauri kwanza Chadema kumvua uenyekiti Mbowe kwa Ubabe na Tamaa ya pesa aliyonayo, Lowasa na Sumaye wapewe uongozi kama inafaa..
Huna Cha kumshauri Magu ana wataalam wa kila aina.
 
Kwa hiyo waache waendelee kuishi sehemu hatarishi?? Au unataka watendaji wachukuliwe hatua?
 
Kwani haufahamu hao wa mabondeni walilipwa na kmaa kunaodai hawakupata viwanja walikuwa wapi miaka yote kwenda kudai haki yao?

Wengi wameishi kwa kufharau au kwenda kuonga ili serikali isifanye kazi yao.

Wengi nyumba zao zina alama ya X hivyo wameshapewa kufa kuwa tumeweka X ondoka ila ndio wanataka pima upepo.

Siku watakayobomoa ya yule mama mchungaji ndipo wengi tutajua kweli hawezi kuonga tena. Wote watendewe sawa wa uzunguni na mabondeni na popote.pia Sumaye na wenzake walioingilia viwanja vya kuchezea mpira TPDC, Mikocheni.
 
Kashauri kwanza Chadema kumvua uenyekiti Mbowe kwa Ubabe na Tamaa ya pesa aliyonayo, Lowasa na Sumaye wapewe uongozi kama inafaa..
Huna Cha kumshauri Magu ana wataalam wa kila aina.

Nakuona wewe ni mgeni wa hili jukwaa, mleta uzi ni gamba mwenzio wa siku nyingi
 
Ila wewe mleta mada hivi Mh. Magufuli kakukuna wapi? Maana naona umedediketi maisha yako kumpinga kazi na kutaka sijui iweje.leo umeingia kwa gia tofauti ili akusome aaaagh ID yako haibadiliki tunajua umetumbuliwa jipu au bado mnamengine.

Haya atakusoma, ila ajur tu haupendi kazi zake.
 
1. Tathimi ilishafanyika ndio maana idadi inajulikana, waziri ameshatoa muda watu wahame na wenye malalamiko wapeleke vidhibitisho.

2. Waziri wa sheria ameshakabidhiwa mikoba sijui ataweza kukata kiu ya wananchi au vipi.

3. Rais aliongea na wafanyabiashara kirafiki kabisa, alizungumzia urasimu na mlolongo wa kodi kama vitu vinavyomkera. Aliagiza EFD zigawiwe bure na akawaambia watakaowakwamisha wakitaka kuwekeza apewe taarifa atawashughulikia.

4. Hakuna

5. Hatuwezi kujenga kwanza shule ndio tuanze kuandaa walimu, vyote vinakwenda pamoja.
Wakati uwekezaji ukiwa unaendelea na juhudi za kupata umeme wa uhakika zinaendelea vilevile.
 
mkuu kumpinga rais ni uhain watch ur mouth
 
hapo kwenye viwanda unafijkiri utafanyeje umejenga kwa mkopo toka bank halfu wakati unasubiri umeme utatoa wapi pesa za kurudisha bank
kulipa walinzi
wanao deki
bili ya maji
bili ya umeme domestic
bili ya simu
wakandarasi wa ujenzi nk.kumbuka hata waliokuwa wanasambaza umeme wa rea hawajalipwa itv jana
 
Tanzania ni taifa la watu wajinga, lau wangeupta hata robo tu ya ufaham wako wangeelewa
 
Back
Top Bottom