Barua yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua yako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Nov 19, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mpenzi

  Sema habari za huko Baby unaendeleaje ? Vipi hali ya hewa huko , siku nyingi sana hujaniandikia email wala mimi sijakuandikia chochote samahani sana kwa hilo na wewe pia nakusamehe kwa hilo – usijali kwa sababu kila siku nakupenda zaidi my baby .

  Hata hivyo ni muhimu sana kwangu mimi kukueleza jinsi ninavyokupenda kila mara ninapopata nafasi hiyo kama saa hizi jioni hii , natamani ningekuwa nasema maneno haya huku nimekubaba , nimekushika mauno huku nikikuangalia usoni uzuri wa macho yako na nywele zako nzuri kuliko za wanawake wote duniani .

  Lakini kwa sababu tumetengana kwa mamia ya kilomita , upweke , hisia zangu nazieleza kwa njia ya barua kama hii unayoisoma sasa hivi my baby , najua ni ngumu kwako na kwangu kutenganishwa kama hivi sasa kwa kipindi kirefu .

  Jua kwamba maisha yanamajaribio mengi , huu umbali wetu wa sasa ni moja ya majaribio hayo ya kimaisha , jinsi tunavyowasiliana sasa hivi ndio tunajenga misingi mizuri ya mahusiano yetu na zaidi ya yote ni mapenzi yetu na ushirikiano kwenye penzi letu hata hivyo mapenzi hayana mipaka wala aina Fulani ya vipimo na hupitia njia nyingi sana . kwa kweli kama ni mapenzi ya kweli yatasimama na kukua.

  Mpenzi

  Jina lako ni muziki mzuri sana kwenye masikio yangu , sauti yako ni ala nzuri kwenye moyo wangu , nikiita jina lako na kusikia sauti yako mwingi wangu husisimka na kujiandaa kwa kitu kizuri zaidi .

  Mpenzi

  Naomba uamini nilichokuambia kwa kweli siwezi kukaa dakika kadhaa bila kukufikiria wewe , muda mwingi hisia zangu hujaa mambo mazuri kuhusu wewe mpango mizuri kuhusu mimi na wewe sitaki hata kupoteza sekunde moja kuacha kufikiria juu yako na jinsi tunavyoweza kuwa karibu zaidi ya ilivyosasa .

  Natamani ungekuwa hapa karibu nami , tushikane tupeane mabusu moto moto , karibu tukae wawili tubembelezane kwa shuguli zote za siku ya leo , mpenzi natamani sana ungekuwa karibu yangu jioni ya leo .

  Saa zingine nafikiria hata ni jinsi gani ninavyoweza kulala niamke tena siku inayofuatia bila ya wewe kwa jinsi ninavyokupenda .

  Mpenzi nakupenda na nitazidi kukupenda zaidi ntaendelea kungoja siku hiyo ambayo tutaungana kimwili .

  Mpaka siku hiyo I fike naomba nitume barua hii fupi kupitia maelfu ya kilometa yenye mapenzi yangu ya dhati kwako na busu moto moto .
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna watu bado wanaandikaga barua?
   
Loading...