Barua ya waziri Muhongo na magazeti ya leo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,986
Nimeshanga sana kuona magazeti karibu yote yakiwemo ya serikali na lile la chama hayajaandika chochote kuhusu uamuzi waziri Muhongo kuipiga 'stop' EWURA kupandisha bei ya umeme.

Katika magazeti yote niliyopitia,ni gazeti la TanzanuaDaima tu ndio limeandika hii habari wakati hata magazeti ya serikali ya Sunday news na HabariLeo pamoja ni lile la chama(Uhuru) hayajaandika chochote kuhusu uamuzi huu.

Magazeti ya MTANZANIA na JAMUHURI ndio sijayaona labda haya ndio yanaweza kuwa yameandika kuhusu hii habari.

Maswali:

Inawezekana barua hii ilitoka muda ambao magazeti mengi yalishaanza kuchapishwa hivyo ikawa vigumu habari kuandika na magazeti mengi ya leo?

Au Wahariri wameona hii habari sio muhimu?

Inawezekana kweli hii habari isiwe muhimu kwa wahariri hawa?

Au wadau hii barua ni fake?
 
Wamechoshwa na maigizo.

Mawaziri wanatengeneza chaos ili waje na makanusho na matamko ya yasiyoeleweka. Utawala wa bongo movie.
 
Yawezekana Ewura Ina Nguvu Kuliko Waziri. Hivyo Wanajua Soon Tamko Litapuuzwa
ile barua (kama kweli ipo) itakuwa imeandikwa ku-manage backlash.

huku mkono wa kushoto unasema "ndiyo" halafu baadae kidogo unautonya wa kulia na kuuambia useme "hapana". mambo ya siasa ndiyo yako hivyo. mnaoota sijui uchumi wa kati au wa viwonder chini ya watu wale wale endeleeni tu na usingizi wenu mtamu.

inanikumbusha pia stori ya machinga. mara "waondoke" lakini baada ya kusoma upepo "hakuna kuwaondoa".
 
Stop order ya Muhongo ilitoka mida ya night kali, around saa nne usiku wakati magazeti mengi yakiwa yamekwisha enda kwenye press... Na gazeti likishaenda kwenye press, sio rahisi sana kubadilisha chochote, lazivyo unaweza ukaathiri uchapishaji wa nakala kulingana na production schedule iliyopangwa...
 
Kwani kwenye television stations walionyesha? Nadhani wahariri walikuwa bado hawajazihakiki hizo taarifa kama ni za kweli.
 
Huenda hii barua ikawa ni fake na kama sio fake basi mwandishi arudi shule kujifunza uandishi wa barua za kikazi.
Barua imejaa makosa hatari na cc kwa Rais. Dunia nzima wanatushangaa tunapoandika barua mbovu kama hizo halafu tunaziweka kwenye mtandao. Utadhani tumepata uhuru leo. Inasikitisha sana
 
Nimeshanga sana kuona magazeti karibu yote yakiwemo ya serikali na lile la chama hayajaandika chochote kuhusu uamuzi waziri Muhongo kuipiga 'stop' EWURA kupandisha bei ya umeme.

Katika magazeti yote niliyopitia,ni gazeti la TanzanuaDaima tu ndio limeandika hii habari wakati hata magazeti ya serikali ya Sunday news na HabariLeo pamoja ni lile la chama(Uhuru) hayajaandika chochote kuhusu uamuzi huu.

Magazeti ya MTANZANIA na JAMUHURI ndio sijayaona labda haya ndio yanaweza kuwa yameandika kuhusu hii habari.

Maswali:

Inawezekana barua hii ilitoka muda ambao magazeti mengi yalishaanza kuchapishwa hivyo ikawa vigumu habari kuandika na magazeti mengi ya leo?

Au Wahariri wameona hii habari sio muhimu?

Inawezekana kweli hii habari isiwe muhimu kwa wahariri hawa?

Au wadau hii barua ni fake?
Tangazo limetoka saa mbili usiku,hata TV zingine zimeshindwa kurusha,magazeti mengi yanaingia mitamboni kuanzia saa12
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom