Barua ya wazi: you should never wait for the second chance to meet the first impression

Humorous Junior

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
1,468
2,000
Salaam sana ndugu zangu wana JF wale wote ambao ni waajiriwa na ambao sio waajiriwa. Leo tarehe 13 December 2018 zimesalia siku 18 kumaliza mwaka huu. Tumuombe mungu kwa pamoja ili tuweze kuiona tarehe 1 January 2019.

Nimelazimika kuandika waraka huu baada ya vilio vya pensheni kutawala. Ni jambo la huzuni na masikitiko kwa wote. Maswali yangu ni haya lakini, "Kwanini tunalilia mafao ya uzeeni kwa asilimia 100?" "Je. tukipata hayo mafao kwa asilimia 100 tutaishi milele?" "Je, Ina maana tumeshindwa kutafuta au hatuwezi kutafuta mafanikio wakati wa ujana wetu mpaka tufuke uzeeni tulipwe mafao?" Ashahakum si matusi ndugu zangu wote wale ambao ni waajiriwa na mnataka mafao kwa asilimia 100!

Chanzo cha vilio hivi ni utumwa wa fikra! Hisia ni kitu kibaya sana . Hisia zetu zimezidi uwezo wetu wa kufikiri. Wengi wetu tumekuwa tukiajiriwa na kudhani kuwa ajira itamaliza matatizo yetu yote tuliyonayo, kumbe si kweli! Zinduka ndugu yangu hakuna mwajiri anayeweza kukulipa wewe kama unavyostahili kulipwa. Anachofanya ni kukutosheleza wewe mahitaji yako ya msingi tu!

Ifanye kazi kuwa kitu cha ziada kwako katika maisha yako. Tengeneza mifumo itakayo kufanya uwe na financial Freedom nje ya ajira na hata kama hautakuwa na ajira. Wengi wetu hatuishi maisha yenye thamani. Wakati nikiwa darasani askofu mmoja aliwahi kusema, "Live life meaningful" Vijana wote na wale wote abao bado hamjastaafu mnapaswa kuishi maisha yenye thamani.

Wengi wetu tunatumia vibaya kipato chetu. Starehe kwetu imekuewa kama chakula na maji. Pombe na ngono ndiyo maisha ya ufahali kwetu! Mwalimu wangu wa mathematics o'level aliwahi kusema "Ngono ni starehe za watu masikini" Kwanini tusiwe masikini ikiwa tunapenda starehe kuliko kujijenga kiuchumi toshelevu? Tukumbuke hili, ujana wako wa leo ndiyo majuti ya uzeeni kwako ndugu yangu!

Je ulisoma maisha yako yote ili uajiriwe alafu ungoje pensheni uzeeni? Kila mwajiriwa ni mtumwa. Unadhani nani atakupa uhuru wako? TUCTA? NSSF? TUNDU LISSU? Mtu anaogopa kuajiriwa mahali ambapo atapewa mkataba wa mwak mmoja kwa mshara wa dola za marekani 55.000 kila mwezi laikini yupo tayari afanye kazi mpaka kufa akisubir mshahara wa milioni 7! Anachongojoea ni mafao yake! Never wait fot the second chance to meet the first impression.

Ishi leo kama ndiyo siku yako ya mwisho "Live to daya as your last day-OG MANDINO,in THE GREAT SALESMA". Kwanini ufanye kazi katika ofisi moja mpaka kufa au ustaafu wakati kwingine kupo ambapo maslahi mazuri yapo na sifa unazo? Tatizo la haya yote ni kwamba tumekuwa watu ambao hatutaki kujifunza kila siku mambo mapya! Elimu inaanzia palepale uliposhia. Ndiyo maana unakuta mtu ana PhD. au ni Profesa lakini ana maisha ya kawaida sana!

Jipange leo, kesho ni siku ya watu wapumbavu! Hata Macom X aliwahi kusema "Thw future belongs to those who preapre it for today" MSINGOJE MAFAO YA UZEENI. Hata Don Robert Marquiz aliwahi kusema, "Unaweza kufanya kazi kwa bidii na maarifa ukawa tajiri lakini inategemea unafanya kazi ya nani"

Ndimi,
Humorous
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom