Barua ya wazi Wizara ya Elimu kuhusu Elimu bure Mkoani Mtwara

Dupe

JF-Expert Member
Jan 21, 2013
1,668
811
Kwanza nianze kumpongeza Mh; John Joseph Pombe Magufuli kwa kuanza vyema katika uongozi wake huku ndani ya mwezi mmoja akifanikisha kuandika record ya ukusanyaji wa mapato kufikia Tilion 1.4.

Pongezi zangu pia ziende kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na ufundi Mh Ndalichako kwa kuteuliwa kuwa waziri wa elimu katika nchi yetu pendwa ya Tanzania huku akipewa jukumu la kuhakikisha elimu ya Tanzania inasimama vyema huku akianza na changamoto za kutekeleza sera ya Elimu bure kwa shule za msingi na sekondari nchini kote,

Katika sakata hili la kutekeleza sera hii ya elimu bure kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya shule na.moja wapo ni shule ya Msingi Magomeni Mkoani Mtwara manispaa ya Mtwara Mikindani kwa kuchangisha watoto fedha huku tukiaminishwa elimu bure, tatizo hili nimeliona kwa mtoto wa dadaangu baada ya kuona form ambayo mtoto huyu kapewa ili akaanze masomo ya darasa la kwanza lakini Form hii ikiwa na michango lukuki … nitaambatanisha chini kama ushahidi wangu…

Je? Hii ndio elimu bure? Nani anapewa jukumu la kutekeleza kwa ufasaha sera hii katika mashule pasi mashule haya kujiwekea mikono yao wenyewe?

Mh: Ndalichako nafikiri unatembelea kwenye Kurasa za Jamii Forums kwani ata uwaziri wako wa elimu ulianza kuupata huku kabla JPM hajakuteua hivo tunaomba ushughulikie sakata jili.
 
Form ya kujinga elimu ya msingi darasa la kwanza
 

Attachments

  • 1452841248826.jpg
    1452841248826.jpg
    38.6 KB · Views: 60
Mh Simbachawene tembelea pia Manispaa ya Mtwara Mikindani kuna kama ao uliwafuta kazi Dodoma wanachangisha watoto michango ya ulinzi
 
Back
Top Bottom