Barua ya wazi wa Waziri wa Kilimo: Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, NA, CAN, SA, PA, CAN, MAPS na DAP)

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,317
8,228
Kwako Mheshimiwa waziri wa kilimo,
Natumai ni mzima wa afya njema.

Mheshimiwa waziri wa Kilimo,
Rejea kichwa cha barua hii ya wazi kama kilivyo jieleza.

Naomba kurejea tena.

Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, Ammonium Nitrate (NA), Ammonium Sulphate (SA), Ammonium Phosphate (PA), Calcium Ammonium Nitrate (CAN), Monoammonium Phosphate (MAP), na Diammonium Phosphate (DAP)).

Mheshimiwa waziri,
Gesi asilia ndio malighafi kuu inayotumika kuzalishia mbolea zote zenye ubora zitumikazo kwenye kilimo hapa duniani.
Mataifa yote yanayotuuzia mbolea hapa Tanzania yanazalisha hiyo mbolea kwa kutumia gesi asilia.

Mheshimiwa waziri,
Tanzania ni nchi pekee Afrika mashariki iliyojaliwa kwa uwepo wa gesi asilia yenye futi za ujazo trillioni 57.54. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa neema hiyo. Lakini pamoja na neema hiyo bado gesi asilia haitumiwi ipasavyo katika taifa letu ili kuweza kuwaletea maendeleo watanzania.

Naweza kusema kwa sasa gesi asilia inatumika kuzalisha umeme. Ambapo asilimia 62 ya umeme unaozalishwa Tanzania unatokana na gesi. Unaweza kuona jinsi gesi ilivyookoa punguza mgao wa umeme katika sekta ya nishati ambao tuliupata miaka ya nyuma kipindi tunazalisha umeme kwa kutumia majenerata yanayotumia mafuta. Serikali imeokoa fedha nyingi ambazo zilitumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi. Lakini pia gesi inatumika kwenye badhi ya vyombo vya moto na mashine na kupikia. Hapa naweza kusema wizara ya nishati iliionyesha uthubutu mkubwa kuingiza gesi asilia katika sekta hii ya nishati.

Mheshimiwa waziri wa kilimo, kama nilivyo ainisha faida tulizozipata kutoka kwenye gesi asilia hapo juu, naweza kusema tena kuwa gesi asilia inamatumizi mengi. Mataifa makubwa duniani yanatumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutokana na gesi. Mbali ya kupikia, kuwashia, kuzalishia umeme, kutumika viwandani na kutumika kwenye magari na machine zingine mbalimbali. Gesi asilia ni kemikali nzuri sana inayotumika kuzalishia mbolea. Mbolea zote zinazozalishwa Urusi, Ukraine, Qatar na mataifa mengine duniani zinatokana na gesi asilia, ndio malighafi na ndio mbolea zenye ubora katika kuzalisha mazao ya kilimo.

Mheshimiwa waziri,
Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa la Tanzania. Watanzania wanategemea kilimo ili waweze kujiendesha kimaisha. Kilimo kimeajiri idadi kubwa ya watanzania na maisha yanaendelea, ila tatizo la mbolea limeendelea kuongezeka Tanzania. Watanzania wanategemea mbolea ili waweze kulima kilimo bora kinachotoa mazao bora. Lakini mheshimiwa waziri mbolea bado ni tatizo. Mimi kama mkulima naweza kusema tatizo la mbolea Tanzania linatatulika, na nitaeleza tufanyeje ili tuweze kutatua tatizo hili lakini in long term.

Ndugu Mheshimiwa waziri, Mimi naona dawa pekee ya kutatua tatizo la mbolea nchini Tanzania ni kujenga kiwanda cha mbolea bora zinazozalishwa kwa kutumia gesi asilia. Hizo ndio mbolea zenye nguvu ya kutoa virutubisho vya kutosha kwenye mimea. Na ndio sababu unaona mbali na kwamba tuna kiwanda cha mbolea Tanzania lakini bado huwa tunaagiza mbolea kutoka mataifa ya nje. Sio kwamba tu ni kwasababu mbolea inayozalishwa ndani haitoshelezi lahasha hata ubora wa mbolea yenyewe hautoshelezi kuzalisha mazao bora na mengi.

Ndugu Mheshimiwa waziri analysis za kujenga kiwanda cha mbolea Lindi zilishafanywa, na wawekezaji walijitokeza wakakubali kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea Tanzania. Na kwakua wateja wapo mimi naona huo mradi utaweza kuleta faida. Mheshimiwa waziri hili ni jambo la neema sana endapo ukilipa kipaumbele zaidi katika wizara yako ya kilimo.

Ndugu mheshimiwa waziri,
Naomba niweze kuelezea kidogo jinsi ambavyo gesi asilia itaweza kubadilishwa kuwa mbolea kama kichwa kinavyo jieleza hapa chini.

KUIBADILI GESI ASILIA KUWA MBOLEA ZA KILIMO KUTAINUA UCHUMI WA TANZANIA.

MBOLEA zinazotumika kwenye kilimo huzalishwa kwa kuibadili GESI ASILIA katika nchi zilizo endelea. Kilimo kinaweza kutufaidisha kama tukianzisha kiwanda cha kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA nchini.

Tanzania huaagiza 90% ya mbolea kutoka nje, 10% huzalishwa ndani.
1/4 ya Uchumi wetu hutegemea kilimo. Kinatoa 85% ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kinaajiri 80% ya watanzania.

Tukianzisha kiwanda cha kuzalisha tani 2300 za AMMONIA na tani 4000 za UREA kwa siku (tani Millioni 1.3 za urea kwa mwaka), tutakidhi mahitaji ya ndani na kiasi cha mbolea inayobaki kikauzwa nje ya nchi.

Hatua za kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.
1. GESI ASILIA (CH4) itabadilishwa kuwa AMMONIA kwa miungano ya kikemikali. AMMONIA yenyewe ni mbolea tayari.

2. AMMONIA itabadirishwa kuwa UREA kwa kutumia miungano ya kikekimali.
Lakini pia kutoka kwenye AMMONIA tutafanya miungano mingine ya kikemikali kupata mbolea za; AMMONIUM NITRATE (NA), AMMONIUM SULPHATE (SA), AMMONIUM PHOSPHATE (PA).

Kutoka kwenye AMMONIUM NITRATE (NA) tutapata mbolea ya CALCIUM AMMONIUM NITRATE (CAN). Kutoka kwenye AMMONIUM PHOSPHATE (PA) tutapata mbolea ya MONOAMMONIUM PHOSPHATE (MAP), na DIAMMONIUM PHOSPHATE (DAP).

Mheshimiwa waziri
Zipo faida nyingi tutazipata kama tukitengeneza mbolea yetu wenyewe.
1. Tutaacha kutegemea mbolea zinazotengenezwa nje ya nchi.

2. Tutakua na usalama wa chakula. Kipindi ambacho mbolea zitakua hazipatikani kwa wingi katika soko la dunia na kuathiri shughuli za kilimo Sisi tutaendelea kulima kilimo bora.

3. Hatutoweza kuathiriwa na upandaji wa bei za mbolea katika soko la dunia.

4. Yanapotokea majanga ya vita yanayoharibu usambasaji wa mbolea katika soko la dunia sisi hatutoweza kuathiriwa kabisa.

Ndugu mheshimiwa waziri baada ya kuibuka kwa vita vya Urusi na Ukraine, yafuatayo yameweza kutokea katika kipindi kifupi katika sekta hii ya mbolea.

1. Bei za mbolea zimepanda katika soko la dunia.

2. Bei za malighafi za kutengenezea mbolea pia zimepanda katika soko la dunia.

3. Taifa la Urusi limewekewa vikwazo vya kuto kuuza mbolea katika soko la dunia.

4. Umoja wa ulaya wameshauri mataifa ya Afrika kuacha kununua mbolea inayotengenezwa na taifa la Urusi badala yake wameshauri tutafute mbadala mwingine.

Rejea hapa: EU Says Africa Should Stop Buying Russian Fertilizer

Mheshimiwa waziri, kuna kilasababu za kuweka mikakati ya muda mrefu na endelevu katika swala la mbolea ili kuendeleza kilimo katika taifa letu. Kilimo chetu kinategemea mbolea ili kiweze kuwa chenye tija.

Mheshimiwa waziri nichukue fursa hii kukushukuru kwa dhati kwa kuisoma barua yangu.

Ahsante.
 
Ndugu mleta mada yule profesa sidhani kama hajui kitu kama hiko ulicho wasilisha hapa. Wanajua sana ila sijui nini kinacho wapelekea kuwa wazito katika kutekeleza mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yatainua hali ya taifa na wananchi moja kwa moja.
 
Barua ya wazi wa Waziri wa Kilimo: Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, NA, CAN, SA, PA, CAN, MAPS na DAP).

Kwako Mheshimiwa Waziri wa Kilimo,

Natumai ni mzima wa afya njema.

Mheshimiwa Waziri wa Kilimo,

Rejea kichwa cha barua hii ya wazi kama kilivyojieleza.

Naomba kurejea tena.

Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, Ammonium Nitrate (NA), Ammonium Sulphate (SA), Ammonium Phosphate (PA), Calcium Ammonium Nitrate (CAN), Monoammonium Phosphate (MAP), na Diammonium Phosphate (DAP)).

Mheshimiwa Waziri,

Gesi asilia ndio raw material inayotumika kuzalishia mbolea zote zenye ubora zitumikazo kwenye kilimo hapa duani. Mataifa yote yanayo import mbolea hapa Tanzania yanazalisha hiyo mbolea kwa kutumia gesi asilia.

Mheshimiwa Waziri,

Tanzania ni nchi pekee Afrika mashariki iliyojaliwa kwa uwepo wa gesi asilia, around 57 Trillion cubic feet. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa neema hiyo.

Mheshimiwa Waziri,

Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa la Tanzania. Watanzania wanategemea kilimo ili waweze kujiendesha kimaisha. Kilimo kimeajiri idadi kubwa ya watanzania na maisha yanaendelea, ila tatizo la mbolea limeendelea kuongezeka Tanzania.

Dawa pekee ya kutatua tatizo la mbolea nchini Tanzania ni kujenga kiwanda mbolea inayozalishwa kwa kutumia gesi asilia. Hizo ndio mbolea zenye nguvu ya kuprovide nutrients za kutosha kwenye mimea..

Mheshimiwa Waziri,

Mheshimiwa waziri analysis zilishafanywa na wawekezaji walijitokeza wakakubali kujenga kiwanda cha mbolea Tanzania. Na kwa kua wateja wapo mimi naona huyo mradi utaweza kuleta faida.

Mheshimiwa Waziri,

Naomba niweze kuelezea kidogo jinsi ambavyo gesi asilia itaweza kubadilishwa kuwa mbolea kama kichwa kinavyovyo jieleza hapa chini.

KUIBADILI GESI ASILIA KUWA MBOLEA ZA KILIMO KUTAINUA UCHUMI WA TANZANIA.

MBOLEA zinazotumika kwenye kilimo huzalishwa kwa kuibadili GESI ASILIA katika nchi zilizo endelea. Kilimo kinaweza kutufaidisha kama tukianzisha kiwanda cha kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA nchini.

Tanzania huaagiza 90% ya mbolea kutoka nje, 10% huzalishwa ndani.

1/4 ya Uchumi wetu hutegemea kilimo. Kinatoa 85% ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kinaajiri 80% ya watanzania.

Tukianzisha kiwanda cha kuzalisha tani 2300 za AMMONIA na tani 4000 za UREA kwa siku (tani Millioni 1.3 za urea kwa mwaka), tutakidhi mahitaji ya ndani na kiasi cha mbolea inayobaki kikauzwa nje ya nchi.

Prosesi za kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.

1. GESI ASILIA (CH4) itabadilishwa kuwa AMMONIA kwa miungano ya kikemikali. AMMONIA yenyewe ni mbolea tayari.

2. AMMONIA itabadirishwa kuwa UREA kwa kutumia miungano ya kikekimali.

Lakini pia kutoka kwenye AMMONIA tutafanya miungano mingine ya kikemikali kupata mbolea za; AMMONIUM NITRATE (NA), AMMONIUM SULPHATE (SA), AMMONIUM PHOSPHATE (PA).

Kutoka kwenye AMMONIUM NITRATE (NA) tutapata mbolea ya CALCIUM AMMONIUM NITRATE (CAN). Kutoka kwenye AMMONIUM PHOSPHATE (PA) tutapata mbolea ya MONOAMMONIUM PHOSPHATE (MAP), na DIAMMONIUM PHOSPHATE (DAP).

Mheshimiwa waziri nichukue fursa hii kukushukuru kwa dhati kwa kuisoma barua yangu.

Ahsante.
 
Nimekuelewa sana; hata hivyo naomba ufafanuzi, unamaanisha mbolea za asili mfano samadi hazitoleta matokeo tarajiwa kwenye kilimo chetu?
 
Mbolea organic ni nini? Ni zipi faida zake? Kwanini hatuipi kipaumbele?
Hizi sina uzoefu nazo japo kwa kumbukumbu zangu zitakua ni mbolea zinazotokana na masalia ya mimea na, vinyesi vya wanyama kama kuku, ng'ombe, punda, mbuzi n.k. Shida ya hizo mbolea uhifadhi wake ni shida zinatoa harufu mbaya pia, zinatoa nutrients kidogo sana. Watakuja wajuvi watakueleza zaidi. Mimi ni expert kwenye hizo inorganic tu
 
Kwako Mheshimiwa waziri wa kilimo,
Natumai ni mzima wa afya njema.

Mheshimiwa waziri wa Kilimo,
Rejea kichwa cha barua hii ya wazi kama kilivyo jieleza.

Naomba kurejea tena.

Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, Ammonium Nitrate (NA), Ammonium Sulphate (SA), Ammonium Phosphate (PA), Calcium Ammonium Nitrate (CAN), Monoammonium Phosphate (MAP), na Diammonium Phosphate (DAP)).

Mheshimiwa waziri,
Gesi asilia ndio raw material inayotumika kuzalishia mbolea zote zenye ubora zitumikazo kwenye kilimo hapa duniani. Mataifa yote yanayo import mbolea hapa Tanzania yanazalisha hiyo mbolea kwa kutumia gesi asilia.

Mheshimiwa waziri,
Tanzania ni nchi pekee Afrika mashariki iliyojaliwa kwa uwepo wa gesi asilia, around 57 Trillion cubic feet. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa neema hiyo. Lakini pamoja na neema hiyo bado gesi asilia haitumiwi ipasavyo katika taifa letu.

Mheshimiwa waziri wa kilimo,
Gesi asilia inamatumizi mengi, mataifa makubwa yanatumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutokana na gesi. Mbali ya kupikia, kuwashia, kuzalishia umeme, kutumika viwandani na kutumika kwenye magari na machine zingine mbalimbali. Gesi asilia ni kemikali nzuri sana inayotumika kuzalishia mbolea.

Mheshimiwa waziri,
Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa la Tanzania. Watanzania wanategemea kilimo ili waweze kujiendesha kimaisha. Kilimo kimeajiri idadi kubwa ya watanzania na maisha yanaendelea, ila tatizo la mbolea limeendelea kuongezeka Tanzania. Watanzania wanategemea mbolea ili waweze kulima kilimo bora kinachotoa mazao bora. Lakini mheshimiwa waziri mbolea bado ni tatizo. Mimi kama mkulima naweza kusema tatizo la mbolea Tanzania linatatulika, na nitaeleza tufanyeje ili tuweze kutatua tatizo hili lakini in long term.

Ndugu Mheshimiwa waziri, Mimi naona dawa pekee ya kutatua tatizo la mbolea nchini Tanzania ni kujenga kiwanda cha mbolea bora zinazozalishwa kwa kutumia gesi asilia. Hizo ndio mbolea zenye nguvu ya kuprovide nutrients za kutosha kwenye mimea. Na ndio sababu unaona mbali na kwamba tuna kiwanda cha mbolea Tanzania lakini bado huwa tunaagiza mbolea kutoka mataifa ya nje. Sio kwamba tu ni kwasababu mbolea inayozaliwa ndani haitoshelezi lahasha hata ubora wa mbolea nyenyewe hautoshelezi kuzalisha mazao bora.

Ndugu Mheshimiwa waziri analysis za kujenga kiwanda cha mbolea Lindi Mtwala zilishafanywa, na wawekezaji walijitokeza wakakubali kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea Tanzania. Na kwa kua wateja wapo mimi naona huo mradi utaweza kuleta faida.

Ndugu mheshimiwa waziri,
Naomba niweze kuelezea kidogo jinsi ambavyo gesi asilia itaweza kubadilishwa kuwa mbolea kama kichwa kinavyo jieleza hapa chini.

KUIBADILI GESI ASILIA KUWA MBOLEA ZA KILIMO KUTAINUA UCHUMI WA TANZANIA.

MBOLEA zinazotumika kwenye kilimo huzalishwa kwa kuibadili GESI ASILIA katika nchi zilizo endelea. Kilimo kinaweza kutufaidisha kama tukianzisha kiwanda cha kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA nchini.

Tanzania huaagiza 90% ya mbolea kutoka nje, 10% huzalishwa ndani.
1/4 ya Uchumi wetu hutegemea kilimo. Kinatoa 85% ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kinaajiri 80% ya watanzania.

Tukianzisha kiwanda cha kuzalisha tani 2300 za AMMONIA na tani 4000 za UREA kwa siku (tani Millioni 1.3 za urea kwa mwaka), tutakidhi mahitaji ya ndani na kiasi cha mbolea inayobaki kikauzwa nje ya nchi.

Prosesi za kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.
1. GESI ASILIA (CH4) itabadilishwa kuwa AMMONIA kwa miungano ya kikemikali. AMMONIA yenyewe ni mbolea tayari.

2. AMMONIA itabadirishwa kuwa UREA kwa kutumia miungano ya kikekimali.
Lakini pia kutoka kwenye AMMONIA tutafanya miungano mingine ya kikemikali kupata mbolea za; AMMONIUM NITRATE (NA), AMMONIUM SULPHATE (SA), AMMONIUM PHOSPHATE (PA).

Kutoka kwenye AMMONIUM NITRATE (NA) tutapata mbolea ya CALCIUM AMMONIUM NITRATE (CAN). Kutoka kwenye AMMONIUM PHOSPHATE (PA) tutapata mbolea ya MONOAMMONIUM PHOSPHATE (MAP), na DIAMMONIUM PHOSPHATE (DAP).

Mheshimiwa waziri nichukue fursa hii kukushukuru kwa dhati kwa kuisoma barua yangu.

Ahsante.
Wakati mwingine kusoma habari kama hizi inaumiza. Hii gesi ya asili tuliaminishwa ndiyo suluhisho la umeme, mbolea, nishati ya kuendesha magari na hata nishati majumbani. Kinachoendelea sasa:

1. Umeme tumerudi kwa nguvu kwenye chanzo cha maji
2. Nishati ya kuendesha mitambo- nimeona tu malori machache ya Kiwanda cha Dangote yanendeshwa na gesi, kwa ujumla hakuna kinachoonekana
3. Mbolea ni stori tu, hakuna seriousness tangu stori zianze
4. Nishati ya majumbani - napo hakuna la maana hadi sasa hivi

Kwa ujumla wake hapajaonekana la maana tangu tuanze wimbo wa gesi, mbali na vurugu huko Mtwara
 
Ni kweli mkuu kwa kweli inahitaji moyo
 
Tukizungumzia mambo ya muhimu watu mnakimbia.
Haya mambo yanatia hasira mwisho utaishia kutukana bure uutoe huu uzi thamani yake!

Viongozi wetu are not willing and capable to provide life changing solutions zaidi ya kujali matumbo yao na familia zao tu. Yes, you can tell them I said it.
 
Niliwambia lakini
Utekelezaji wa idea yako na mengine mengi ya kulikwamua taifa kiuchumi primarily unategemea na utayari wa viongozi wetu (political willingness) ambayo kimsingi haipo. Tanzania ina resources nyingi sana ambazo iwapo zingetumiwa sawasawa uchumi wetu ungebadilika(to the better) shida ni utayari wa viongozi wetu na uwepo wa sera mbovu.
 
Kabisa mkuu, viongozi wetu na mfumo.
 
Back
Top Bottom