Barua ya wazi: Tutasema Freeman Aikael Mbowe sio gaidi

CONSCIOUS1996

New Member
Mar 13, 2014
2
14
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Kwako mhe. Freeman Aikael Mbowe.

Ninapokuwa katika umri wangu huu wa karibu robo karne hakuna siku imewai kupita sijasikia jina Freeman au Mbowe maishani mwangu aidha niwe ndani ya nchi au nje ya nchi, aidha niwe online au offline.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Kuanzia vijiwe vya Pweza, Kahawa,Alkasus, Sokoni, vijiwe vya siasa kwenda mpaka vijiwe vya kisasa vya Facebook, instagram, Whatsapp groups, Telegram, JamiiForum na Twitter. Hakuna siku inapita sijasikia jina lako Freeman mtoto wa Tanzania.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

FREEMAN umekuwa ukisema Chadema haiwezi kuwa chanzo cha kuigawa nchi yetu, Freeman August 2020, ulisema Chadema siyo chama cha WAASI, ni chama cha siasa. kama ni hivyo Freeman ukiwa UKONGA sisi tuliopo nje hatutadai uhuru wako kwa kuharibu mali/uhai wa yeyote. Tunaamini katika KARMA , watavuna wapandacho.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Wapo wengi wanaokusema kwa mazuri Freeman na wachache wasiokujua wanakusema kwa mabaya, ninaamini wazi haya mazuri hayajawai kukufanya uvimbe kichwa na kujiona wewe ni bora sana kuliko mwingine, ninaamini wazi wanaokusema kwa mabaya hawajawai kukunyong'onyesha katika harakati zako za kudai haki, katiba na maendeleo ya watu.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Freeman Mbowe kwangu sio tu mwanasiasa bali Freeman ni mfumo wa kupambania Uhuru wa watu, Haki za watu na maendeleo ya watu.

Nani asiejua umuhimu wako Freeman? Nani asiyejua umuhimu wa mawazo yako katika maendeleo yaliyopo Tanzania leo Freeman?
Nani asiejua umuhimu wako katika kuwajengea uwezo vijana kwenye uongozi Freeman?

Wasiojua sie waungwana tutawajulisha.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawajulisha vijana kwa wazee kuwa hizo Elimu zao na elimu za watoto wao wengi wanazotambia sasa walizopata shule za kata ilikua wazo la Freeman A. Mbowe, Kwa sie tuliosoma shule za kata. Freeman Mbowe sio tu m/kiti wa CHADEMA, wewe ni mkombozi wa elimu yetu pamoja na mapungufu yake.

Kwa wasiojua history ya nchi hii tutawaambia maendeleo yoyote huanzia kwenye mawazo, wazo la "SHULE ZA KATA" liliasisiwa na Mbowe na shule ya kwanza ya kata ilikua Harambee secondary kwa tuliofika HAI tunaifahamu.

Hata hawa vijana wanakuona leo wewe sio mtu wa maana wamesoma hizi shule (pamoja na mapungufu yake).Na kama hawakusoma basi wana ndugu/rafiki zao au wafanyakazi wao waliosoma huko . Leo wengine wanashabikia wewe kuteswa na watesi wako.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawajulisha vijana kwa wazee namna ulivoamini kwenye kuwajengea uwezo vijana, namna ulivozunguka vyuo vikuu na mtaani, na kuibua talents za kina ZZK, mtoto wa mjini Lijualikali, Silinde, Nassari,Mdee, Gekul, Ally bananga n.k ambao wengine waligeukia upande wa watesi wako na wengine wakageuka kuwa watesi wako hadharani. Unachonishangaza hujawai kukata tamaa Freeman, hujawai kunyoosha mikono na kuamua kupumzika mzee wangu hata siku moja , baadhi ya watu wako wa karibu kila ninapoongea nao wananiambia "Hakuna wakati Mwenyekiti yuko committed kama huu", kila siku zinavozidi kwenda unazidi kuwa imara.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawajulisha vijana kwa wazee namna unavopenda amani ya nchi hii, wengi wamesema CHADEMA ni chama cha fujo na watu wasiotaka amani ya hii nchi, Freeman umekuwa mstari wa mbele kuilinda amani ya nchi yetu hasa kwa kuhubiri na kuwafunza watawala kuwa "AMANI ni tunda la HAKI", hujawai choka kusema hili Freeman toka niko kidato cha kwanza nakufatilia umekuwa ni wimbo wako kila siku.

Hata wakati wa Mwendazake ulipoteswa kwa kupigwa, kunyang'anywa mali, kufungiwa mshahara, viongozi na wanachama wako kutekwa na kuuwawa bado ulienda Mwanza mbele ya Mwendazake na ukamweleza Tanzania uitakayo, ukamweleza umuhimu wa maridhiano kama taifa kwa kuwa bwana yule Moyo wake ulikua mgumu, Mungu alishighulika naye na wote tuliona ukuu wake.
Ulikataa serikali kupuuza ugonjwa wa CORONA na ulionesha mfano kwa kutoka na wabunge wa CDM nje, wengi walikubeza lakini leo Kiko wapi, wengi walipoteza ndugu zao na leo hii wako bize kutuelimisha tuchukue chanjo.
Freeman misimamo yako
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawajulisha vijana kwa wazee kuwa wewe Freeman Mbowe sio mpiga dili(opportunist) ulikua na options za ku-compromise toka Nyerere akiwa hai uwe upande wa watawala na ule mema ya nchi pamoja na wengine, Pengine kwa uwezo wako, kwa mchango wa mzee Aikael Mbowe kwenye uhuru wa nchi hii usingekosa kuwa raia namba 1,2 au 3. Lakini hujawai ku-compromise Freeman, hujawai kuchagua raha hizi bila kuona sie vijana tukisi kwenye nchi ya Uhuru wa kweli, haki na maendeleo ya kweli.
Tutawaambia namna ulivyopambana kukikuza chama chetu pasina kulipwa mshahara hata Sh. 100.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawaambia hawa vijana wanaopiga mdomo kuwa unavunja katiba ya chama, kuwa wewe ni mungu-mtu, tutawauliza Freeman ni nani mpaka Serikali ya CCM na msajili wa vyama( anaeteuliwa na Mwenyekiti CCM) imuangalie tu akivunja sheria za chama chake.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Tutawajulisha vijana kwa wazee kuwa pamoja na wewe kutoka familia yenye utajiri umekuwa ukiishi kwa kujishusha, umeishi kwa kujifunza vingi kutoka kwa vijana na watu mbalimbali wenye exposure, Freeman ninaekujua ni mtu mwenye busara na unajifunza kila siku. Hujaacha kutoa elimu na hamasa kwetu hasa pale tunapohisi kukata tamaa katika mapambano ya kudai haki zetu na maendeleo ya kweli.
Tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI"

Huku nje tumeku-miss kaka Freeman, huku nje hatuna amani baada ya wewe kuitwa Gaidi na kupewa mashtaka na washenzi na wahuni wanaoona Tanzania ni nchi yao peke yao kwa vile tu wana mamlaka, nguvu, jeshi, polisi, TISS n.k.

Ninaamini ipo siku utatoka nje ya nondo na tutaongea kaka Freeman, kama hutatoka James atakuletea ujumbe huu uusome ukiwa Gerezani ungali hai.

Vijana na watanzania wote wapenda haki tunakupenda, tunakuombea na tutasema popote iwe ndani ya nchi au nje ya nchi, iwe online au offline tutasema " FREEMAN AIKAEL MBOWE SIO GAIDI". Haya yote yana mwisho na mwisho wa kila afanyaye yaso-haki utafika.

Nakuombea afya kwenye NYAMA, DAMU na MIFUPA.
Imeandikwa na: GABRIEL M. PATSON
E-mail: gabrielpatson@protonmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom