Ndugu Waziri Mkuu,
Kwa hili sakata linaloendelea la ukiukwaji Mkubwa Wa haki za binadamu kwa mateso na mauaji ya raia katika operesheni tokomeza Mh. Pinda lazima awajibike na kuachia uwaziri mkuu kwa heshima la sivyo utamponza Rais na kuonekana serikali yake haifuati misingi ya Utawala bora wa sheria na hii inaweza kuchangia kuichafua kabisa serikali ya Jakaya M. Kikwete.
Waziri Mkuu lazima uachie ngazi kwa sababu hii operesheni imesimamiwa na wewe mwenyewe kwa kutumia kikosi kazi Maalum. Pamoja Na mawaziri wako kuwajibishwa lazima na wewe mwenyewe awajibike kwa makosa ya serikali yako. Kuwajibishwa kwa hao mawaziri wanne haitoshi kwa uzito Na 'nature' ya kosa.
Pia Kumbuka-kauli yako ya 'Wapigwe tu'- kauli ya aibu kwa waziri Mkuu yeyote duniani kwa nchi inayoongozwa na Utawala wa sheria. Hata Kwa kauli hii tu pekee ulipaswa kuwa -umekwishawajibika.
Nashangaa Kama unasubiri uambiwe na rais Au -Kama unasubiri bunge likuwajibishe! Najua rais hataweza kwa sababu anakuonea huruma. Hata uking'ang'ania uwaziri Mkuu utaendesha hii nchi bila heshima unayostahili Kutoka kwa wananchi wako.
Bungeni ulikiri kwamba unaweza kuondoka kwa kutakiwa na rais au bunge. Lakini ukashindwa kutaja njia nyingine ya kuwajibika na kujiuzulu mwenyewe-ambayo ndio njia rahisi zaidi. Sasa nakushauri andika barua kimyakimya ya kujiuzulu kwa rais Na Kama rais akikukatalia kujiuzulu kwa kuwajibika basi tutajua makosa ni ya rais.
Bora tutunze mizigo ya mawaziri wastaafu kuliko kuwa Na waziri Mkuu mzigo ndani ya serikali.
Haya ni mawazo yangu lakini Nadhani kuna watanzania wengi wenye mawazo Kama yangu.
Naomba Kuwasilisha.