Barua Ya Wazi: Mh. Pinda lazima uwajibike la sivyo utamponza Rais

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
0
Ndugu Waziri Mkuu,
Kwa hili sakata linaloendelea la ukiukwaji Mkubwa Wa haki za binadamu kwa mateso na mauaji ya raia katika operesheni tokomeza Mh. Pinda lazima awajibike na kuachia uwaziri mkuu kwa heshima la sivyo utamponza Rais na kuonekana serikali yake haifuati misingi ya Utawala bora wa sheria na hii inaweza kuchangia kuichafua kabisa serikali ya Jakaya M. Kikwete.

Waziri Mkuu lazima uachie ngazi kwa sababu hii operesheni imesimamiwa na wewe mwenyewe kwa kutumia kikosi kazi Maalum. Pamoja Na mawaziri wako kuwajibishwa lazima na wewe mwenyewe awajibike kwa makosa ya serikali yako. Kuwajibishwa kwa hao mawaziri wanne haitoshi kwa uzito Na 'nature' ya kosa.

Pia Kumbuka-kauli yako ya 'Wapigwe tu'- kauli ya aibu kwa waziri Mkuu yeyote duniani kwa nchi inayoongozwa na Utawala wa sheria. Hata Kwa kauli hii tu pekee ulipaswa kuwa -umekwishawajibika.

Nashangaa Kama unasubiri uambiwe na rais Au -Kama unasubiri bunge likuwajibishe! Najua rais hataweza kwa sababu anakuonea huruma. Hata uking'ang'ania uwaziri Mkuu utaendesha hii nchi bila heshima unayostahili Kutoka kwa wananchi wako.

Bungeni ulikiri kwamba unaweza kuondoka kwa kutakiwa na rais au bunge. Lakini ukashindwa kutaja njia nyingine ya kuwajibika na kujiuzulu mwenyewe-ambayo ndio njia rahisi zaidi. Sasa nakushauri andika barua kimyakimya ya kujiuzulu kwa rais Na Kama rais akikukatalia kujiuzulu kwa kuwajibika basi tutajua makosa ni ya rais.

Bora tutunze mizigo ya mawaziri wastaafu kuliko kuwa Na waziri Mkuu mzigo ndani ya serikali.

Haya ni mawazo yangu lakini Nadhani kuna watanzania wengi wenye mawazo Kama yangu.

Naomba Kuwasilisha.
 
Supervisor

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
559
250

Binafsi i concur he must go.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,759
2,000
hivi unaweza kumtenganisha rais na ukatili huu,nani aliwapa amri wanajeshi?jk hakuwa presidential material acheni kuuma maneno..
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,465
2,000
Mbaya zaidi inaelezwa kwamba Nchimbi alimwandikia barua mara mbili juu ya mambo yaliyokuwa yanatokea huko kwenye operesheni tokomeza, lakini kamwe hakuchukua hatua ya kufuatilia sanasana alijibu kuwa hiyo ni operesheni maalum akiwa ofisini -ingia kwa hii link hapa chini

jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/576508-siri-zafichuka-kung%92oka-mawaziri-ripoti-ya-lembeli-yakosolewa%3Bdk-nchimbi-amwanika-pinda-2.html#post8219412
 
Royals

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,450
1,500
Lakii pia umri wake umekuwa mkubwa sana, anataka kushindana na Mugabe?
 
blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
0
Mbaya zaidi inaelezwa kwamba Nchimbi alimwandikia barua mara mbili juu ya mambo yaliyokuwa yanatokea huko kwenye operesheni tokomeza, lakini kamwe hakuchukua hatua ya kufuatilia sanasana alijibu kuwa hiyo ni operesheni maalum akiwa ofisini -ingia kwa hii link hapa chini

jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/576508-siri-zafichuka-kung%92oka-mawaziri-ripoti-ya-lembeli-yakosolewa%3Bdk-nchimbi-amwanika-pinda-2.html#post8219412

Kweli kabisa Mkuu nimekwishaisoma Na hii taarifa.

Pinda ni mzigo namba moja, aachie ngazi haraka.
 
zaleo

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,905
2,000
Sasa unataka awajibike kwa nani kama sio kwa aliyempa kazi? hata jimboni kwake wanamjua anawajibika kwao kama anavyowajibika kwa Rais aliyempa ulaji
 
Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
250
Baada ya Hapo Viongozi wote walioongoza maandamano batili yaliyosababisha Vifo na vilema kwa mamia ya watanzania nao lazima wajiwabishe na sheria ichukue mkondo wake.
 
Ekikunila

Senior Member
Mar 25, 2013
119
225
Pinda anatakiwa kuachia ngazi ili kulinda heshima yake cku nyingine apewe mwaliko kuzinduwa labda miradi mbalimbali vinginevyo akiendelea kukaa atakuja kutoka kwa aibu kubwa kiasi atasaulika milele.
 
MAHORO

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
7,587
2,000
wakuu hapo mnajisumbua tu,, source ya yote hayo ni JK NA CHAMA CHAKE NI LEGELEGE
 
Ba E's

Senior Member
Aug 20, 2013
145
170
Msije mkamfanya mtoto wa mkulima akaporomosha michozi tena bungeni japo kiukweli anapaswa kujiuzulu, pia rais wetu amekuwa busy mno na safari za nje huenda hatukuchagua rais isipokuwa tumechagua mtalii, wewe mtu gani kila leo anatembeza bakuli kuomba, mimi nilifikiri wagogo ndo wanatabia hiyo kumbe wakwere ni funga kazi aisee!
 
MAHORO

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
7,587
2,000
Msije mkamfanya mtoto wa mkulima akaporomosha michozi tena bungeni japo kiukweli anapaswa kujiuzulu, pia rais wetu amekuwa busy mno na safari za nje huenda hatukuchagua rais isipokuwa tumechagua mtalii, wewe mtu gani kila leo anatembeza bakuli kuomba, mimi nilifikiri wagogo ndo wanatabia hiyo kumbe wakwere ni funga kazi aisee!

JK na yeye inatakiwa ajiuzulu coz ameshindwa kuongoza nchi
 
Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,598
2,000
Mbaya zaidi inaelezwa kwamba Nchimbi alimwandikia barua mara mbili juu ya mambo yaliyokuwa yanatokea huko kwenye operesheni tokomeza, lakini kamwe hakuchukua hatua ya kufuatilia sanasana alijibu kuwa hiyo ni operesheni maalum akiwa ofisini -ingia kwa hii link hapa chini

jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/576508-siri-zafichuka-kung%92oka-mawaziri-ripoti-ya-lembeli-yakosolewa%3Bdk-nchimbi-amwanika-pinda-2.html#post8219412

weka vzur link ifunguke
 
Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,943
1,500
hivi unaweza kumtenganisha rais na ukatili huu,nani aliwapa amri wanajeshi?jk hakuwa presidential material acheni kuuma maneno..

Mkuu,

Hivyo ndivyo Tanzania ilivyo. Heshima anayopewa rais ni zaidi ya miungu. Watanzania kwa heshima za woga tuwape namba moja. Pinda alishakiri bungeni, hawezi kufanya mahamuzi magumu bila kumhusisha Rais....rejea sakata la Gairo, in fact ,yako matukio mengi ya kumulalamika rais moja moja lakini watu wanazunguka kwingine. Tusipobadirika heshima za aina hii zitatuponza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom