Barua ya wazi kwako Rais Samia Suluhu Hassan

Jun 11, 2021
6
1
Kwako Mheshimiwa Rais Samia Suluhu

Salam!

Mimi ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 40 ambaye nimesoma nchini Tanzania kuanzia shule ya Msingi, Sekondari na pia Chuo Kikuu. Elimu yangu kubwa nimeipata kwa watanzania ndani na nje ya Darasa.

Nashukuru katika kuitumikia nchi nimehusika kwa njia moja au nyingine katika kusambaza na kutoa Elimu kwa Watanzania kwa njia mbalimbali. Lakini pia katika hilo nimeweza kupata Elimu toka kwa watanzania mbali mbali pasipo kuhusisha vyeti vyao vya Elimu. Katika Elimu kikubwa ambacho nilijifunza ni kuendelea kujifunza siku zote pasipo kukoma.

Mheshimiwa Rais. Si kawaida katika siasa au jamii yetu mtu kuomba uteuzi kwa namna hii ambayo naitumia kwako. Nimekuwa nikiangalia na kutafakari mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na viongozi vijana wenzangu katika nafasi ambazo wamepewa. Na siku zote nimekuwa nikiumia kuwa pengine kuna tatizo fulani katika uelewa wetu vijana na mambo ya uongozi na wajibu wetu.

Mimi nakuja mbele yako nikiwa pembeni ya watanzania wengi ambao wanaangalia kila kinachotokea na kukitafakari kwa kina. Mh. Rais, naamini kwa yale ambayo nimejifunza katika maisha nikiwa nimeajiriwa na kujiajiri kuna mengi ambayo ningeweza pia yatumia katika kutumikia nchi yangu. Inawezekana kabisa kuna sehemu kama binadamu sikutenda au kunena ilivyopaswa lakini napokaa na kutafakari peke yangu naweza kugundua wapi nilikosea na wapi napaswa kurekebisha au pia kuweka mkazo ikiwa kunaleta matokeo chanya.

Mimi Chama Changu ni Utanzania kwanza. Imani yangu ni Utanzania kwanza na katika hili naamini ninaweza tumika vyema kabisa kwa ajili ya Watanzania kupitia Chama chako cha Mapinduzi. Nikiwa na Kadi ya Chama ya zaidi ya miaka 10. Nimekuwa nikiangalia maslahi ya Watanzania na Utu katika mitizamo yangu, hili naomba niliweke wazi mbele yako. Nikiamini katika Utu Bora, Haki na Wajibu katika kila jambo. Nimekuwa nikiamini matendo mema yanalipa na hali kadhalika matendo maovu yanalipa pasipo kujali Dini, Kabila, Itikadi, Rangi, Umri na Jinsia.

Mh. Rais, Kipekee kabisa naomba nikuombe unipe nafasi ya kuwatumikia Watanzania. Hizi nafasi nafahamu huwa haziombwi, zinahitaji mtu ambaye amekuwa kwenye Chama kwa muda mrefu, mwenye kufahamika ndani ya Chama, mwenye watu wa kumsaidia n.k Lakini hayo yote nimeona niyaweke pembeni nijikite katika Imani yangu kwa Mungu, Kwako na kwa Watanzania kuwa nahitaji kuitumikia nchi.

Mh. Rais naamini nikipata nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa nafasi ya Ukuu wa Wilaya naweza leta mchango na sifa njema kwa Nchi yangu, Serikali na Watanzania kwa Ujumla. Zaidi naweza fanikisha adhma njema uliyo nayo katika kuwatumikia Watanzania.

Kama ambavyo nimesema awali. Si kawaida kwa mtu kuomba nafasi hizi za kuteuliwa lakini naomba kwa mara ya kwanza MIMI MTANZANIA MWENYEWE NISIYE NA MTU WA KUNIPIGIA CHAPUO, KUNIOMBEA AU KUNITAMBULISHA KWAKO. NIKUOMBE UNIPATIE NAFASI YA KUWATUMIKIA WATANZANIA. Uwezo mzuri ninao, Nia njema ninayo, Ari ya Utendaji mwema ninayo.

Nina uzoefu wa kutembelea mikoa mingi Tanzania na kukaa sehemu zenye changamoto nyingi. Huko kote nilifanikiwa kujifunza mengi. Sitochagua Wilaya au Mkoa. Nipo Tayari kuanza kutumika wakati wowote mahali popote. Nipo tayari pia kuonana nawe wakati wowote.

Natumaini Ombi langu litakufikia nawe utalifikiria.

Wako Katika Ujenzi wa Taifa.

Napatikana kwa anuani ya barua pepe hii - a.mbamba@yahoo.com
 
Natamani kila mkuu wa wilaya anatuma maombi hapa jf tunamtathimini uwezo wake kama wewe halafu tunamfania endorsement.

Binafsi nimekukubali. Mama akupe tu ukuu wa wilaya.
 
Hakuna mzalendo nchi hii wote wanafuata maslahi na mishahara minono. Inabidi viongozi wote wakubwa waajiliwe kwa mikataba na mishahara iwe chini ya 2M
 
Unakuta mbunge anajisifia kusema watu wangu. Huku hao watu wakiteseka, fukara. Shule majengo shida, huduma za afya tabu. Mtu mmoja analipwa mamilioni.
Hakuna haki. Wabunge wenyewe majimboni hawaonekani. Wakienda Bungeni maswali ni yale yale toka nazaliwa hakuna linalo badilika. Utasikia korosho, Pamba, ufugaji, madini, elimu. Hivi haya yote hayajapata ufumbuzi toka wakati wa Nyerere hadi Leo! Miaka 60 tunaongelea jambo lile lile!
Ulaya ya miaka ya hamsini na tisini ilikuwa masikini si kama ya Leo. China, Malyasia, India, Korea na nyinginezo walikuwa masikini.
Je sisi watanzania tumelaniwa nini? Nyerere alitupatia viwanda leo vyote hakuna.
Shida ni nini? Nilibahatika kufanya kazi serikalini, nilipo ingia nilishangaa mengi. Hapo nikajua Tanzania kwendelea ni kazi. Tutapiga mark time.
Tunahitaji kubadili mfumo wa kiutumishi. Tunahitaji kubadili matumizi ya fedha na mshahara. Tunahitaji kubadili mfumo wa utekelezaji wa miradi.
Pia kubadili mfumo wa Bunge. Na kuwa na wabunge wachache. Kufuta viti maalum. Na wabunge wawajibishwe mara wanapokuwa si wawajibikaji.
Hivyo tunahitaji muundo mpya wa serikali. Hata baraza la mawaziri hatuhitaji utitiri wa mawaziri.

Kuna mtaalamu wa ujenzi ni Afisa mkubwa walijenga barabara isiyo na kiwango ktk kumhoji akanambia akijenga ya kiwango yeye na familia yake watakula nini?
Anajua hyo isiyo na kiwango baada ya muda itahitaji matengenezo hivyo atapata fedha. Nilichoka!

Afisa mmoja mkubwa anateuliwa na Rais akanambia usipo kula fedha ya serikali wengine wanakula. Usiangalie kuendeleza nchi. Jiendeleze mwenyewe.
Baada ya muda niliona niache kazi ya serikali na kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa.

Tuombeni na kudai Katiba mpya. La sivyo hata vyama shindani vikiingia bado ni yale yale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom