Barua ya wazi kwako mke mtarajiwa

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,942
3,606
IKIWA UTAKUBALI KUOLEWA NAMI BASI USINIPIKIE HIVI
1.JPG

Tembele katika upishi wake wote.....Hii kwangu nikiliona tu nashiba ghafla...Nawachukia hadi wauzaji wake sujui kwa nini....Sina aleji nayo ila likiwa tu mdomoni nasisimka mwili na roho.Yani kama wewe unalipenda basi lipike nisiwepo.Ndugu yangu analipenda ila anajua kabisa nikimtembelea kwake anabadili ratiba ya mboga iyo au kuwepo na nyingine.Nikila halinizuru ila nafsi inataabika ndani kwa ndani.

20150201_173431.jpg
Viazi mbatata - Hivi hata uweke nazi sili....Nina msemo wangu viazi mbatata ni kwaajili ya chipsi tu. Sasa ukiungia mboga sijui kwenye dagaa wengine kwenye nyama wengine kwenye pilau nk basi utavikuta nimevikwepa.Hata ukayarost yani mazima mazima au mapande pande wengine hupikia sambusa na kachori hakika utayakutaaaaaa..Ivyo nala chipsi tu....Navyo nikivikuta popote vimepikwa basi naichukia familia nzima,jiko na mpishi wake...Yani hivyo bora niwe na njaa yangu tu hata ukaweka kuku mimi navikwepa tu utavikuta kama vilivyo.

33473500_129504141178602_2651983632008216576_n.jpg
Mindizi mizima - Kwanza inakaba na haivutii hata ukiyaangalia. Ndizi bana iwe na rojo tena rojo itokane na kuiva ndizi. Ndizi uikate vipande walau ndio moja vitoke vinne nau zaidi. Ndizi isiyokuwa na rojo(sio mchuzi) basi utayakuta hapa nakula ndizi yenye rojo na rojo ikiisha basi utaikuta mindizi imebaki mana vyakukaba siviwezi....Basi ikakosekana rojo basi uwepo basi walau mchuzi wakumezea japo hii ni ishara ya upishi mbovu.

a5e6a6cbe0709689c80d8cc1e40562b2.jpg

Mchina mteketeke - Hapa ili unilishe mchicha basi ukaange sio kunilisha mchicha unachuruzika mchuzi sijui maji au sijui supu....Siuwezi bora ugali nile na sukari au maji ya chumvi kuliko iyo michicha yenye umajimaji...Mchicha uliokaangwa ndio naweza kula.

EWE MKE WANGU MTARAJIWA JITAHIDI KUNIANDALIA MLO HUU

MAZIWA MTINDI 1.jpg
Maziwa mtindi - Haya hakikisha hayakosekani ndani mana kwangu ni dozi asubuhi mchana jioni....Haya kwangu pia ni mboga naweza kulia ugali hata wa watu wanne (sijui kwanini) nilishai walaza na kuwashindisha watu njaa.....Nilimwambia bibi nakuja niandalie chakula nitakacho kipenda....Nilipofika nikakuta ugali na maziwa hakika nilimbusu uso mzima kanijulia mana ndio mlezi wangu.....Haya naweza kuyafungia safari kuyafuata mji/mtaa mwingine.Yan nakuwakama nina uraibu/arosto nayo.Mke ukiona nimekasirika basi niletee grass ya maziwa hakika utatuama moyo

WANGU.
513468935.jpg
Nazi - Yani hakikisha kila kifaacho kupikwa na nazi basi unaweka nazi...Namaanisha hata kama ugali unafaa kuwekwa nazi wewe weka nakipenda sana icho kiungo....Wali bila nazi hujanilisha tena nazi uikune sio bakheresa....Mboga tia nazi ikolee yan nazi weka hata kwenye chai kama yafaa.....Ntahakikisha nyumba haikosekani nazi yan uko jalalani kujae vifuu na machicha ya nazi. Tatizo tumelelewa na nazi...Nakumbuka bibi alikuwa anatumia vimafuta kidogo sana kukaangia viungo ila ilo tui lake soo poa...Wali unukie nazi mboga nazi ikibidi na namafuta tutapaka ya nazi pia.

Trivandrum-Fish-Curry-dRUMSTICK-FISH-CURRY.jpg

Mchuzi - Kama nilivyo kwisha kukueleza kwamba vikavu siviwezi basi sitoitambua mboga ya majani yoyote kama ndio mboga kuu ila kuwe na mboga nyingine ya mchuzi....Na mchuzi hautokuwa halali kama utakosekana nazi ndani yake. Kama itakosekana mboga ya mchuzi kwenye ugali basi maziwa yataokoa jahaz...Wali usio na mchuzi hauliki kwangu yan kuisha kwa mchuzi ndio mwisho wa kula icho chakula. Kuna mama lishe nilimwambia awage ananiweka mchuzi mwingi ila kila akileta nikawa namlalamikia mchuzi kidogo.. Kuna siku akaamua kunikomoa akanijazia mchuzi had ukawa wali umetota kabisa akawa analeta huku anataraji kususiwa,,yan ndio alinipatia siku iyo nikamwambia kila siku unileteage hivi mana bila hivyo inanibidi ninuniage soda kushushia.....Vikavu sivipende mke mtarajiwa.

Zingatio...Sina ugonjwa wala aleji ya chakula chochote cha halali ila katka vyakula kuna mapendeleo ili kurizka na mlo....Ewe mke mke wangu mtarajiwa kumbuka mapishi pia ni sababu ya wewe kukuoa na kungwi mzuri huenda ni bibi yangu juu ya upishi au bintize(mama wadogo/wakubwa).

Karibu sana
 

Attachments

  • 513468935.jpg
    513468935.jpg
    27.9 KB · Views: 43
Blaza wewe unajua kupika? Nakushauri ujifunze ili uweze kuja kumuelekeza mkeo akupikie unachataka na ikiwezekana ufanye kwa vitendo.
Hawa wachumba wa sasa wengi hawajui kupika na wala hawana juhudi za kujifunza.....
MKUU ALIYE LELEWA NA BIBI ATAKOSAJE KUJUA KUPIKA...YAN WIFE AKIZINGUA NAINGIA MWENYEWE JIKONI ILO NI SUALA DOGO
 
Tatizo wanaume siku hizi mmekuwa na nyodo sana.
Oooh ngoja niandae tembere langu niweke na nyanya za kutosha na ndimu au limao .
Nisonge na ugali mtamu nikae chini nile mpaka.
NISHAKUKOSA
 
Sijui Nitaoa Lini Maana Sina Feeling Kabisa Na Ndoa Ila Kama Nikioa Nishapanga Kabisa Nikikuta Mwanamke Hajui Kupika Namlipia Ada Veta Akajifunze Maana Ipo Kwa Ajili Yao
 
Back
Top Bottom