Barua ya wazi kwa zitto kabwe

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
34
Mheshimiwa Zitto Kabwe,
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
na Katibu Mkuu Msaidizi wa CHADEMA.
Mheshimiwa,
Kwa siku za karibuni jina lako limevuma sana katika vyombo vya habari kwa masuala mbali mbali na Watanzania hasa wanachama na wapenzi wa chama chako wamegawanyika ktk mapande mawili, wengine wakikushutumu na wengine wakikuunga mkono! Mimi leo kupitia JF ambako najua wewe ni mwanachama, naomba kupita mstari wa katikati na kukushauri kitu cha kufanya katika kipindi hiki kigumu kwa chama chako na wewe binafsi.

Kama sikosei mheshimiwa, umri wako bado ni mdogo hivyo kunipa imani kwamba bado unayo miaka mingi ya kufanya kazi hizi za kisiasa kuliko viongozi wenzako wengi mlioko CHADEMA. Najua na nina amini kuwa unao uwezo mkubwa wa kufanya siasa lakini kwa hakika wale wote tunaokupenda umetuweka roho juu na hatujui your next move. Lakini Mheshimiwa, kwa jinsi hali ilivyo nakuomba usifanye move yoyote itakayo kuumiza wewe binafsi, kuumiza chama chako au kutuumiza sisi tunaokupenda na kukushabikia!

Hivi sasa najua umekuwa lulu kwa wanaCCM, wanakutaka pia wanataka kukuchanganya kwa sababu wangependa kuona chama chako kikisambaratika ili ifikapo mwaka 2015 wasipate changamoto kama walizopata ktk uchaguzi uliopita. Najua pia kuwa vyama vya NCCR MAGEUZI na CUF wanakumezea mate na wangependa ufanye chochote ili uondokane na hawa CHADEMA na ikiwezekana uungane nao bila kujali maisha yako kisiasa.

Mheshimiwa Zitto,
Usikubali kupoteza mtaji wa kura zaidi ya Milion 2.5 zilizopatikana kwenye uchaguzi mkuu kwa chama chako. Najua kuwa ulichangia moja kwa moja au inderectly kupatikana kwa kura hizo ambazo mimi naona ni mtaji kwako wewe Mheshimiwa. CHADEMA siyo ya Mbowe, Slaa, Mtei wala Kiongozi yeyote. Naamini kuwa Chadema ni yetu sisi wananchi na wanachama wote hivyo mapambano yoyote yanayoendelea kwenye chama ni kielelezo cha mstakabali wetu na lazima historia itakuja tujuza pumba na mchele.

Mheshimiwa, nakuomba uvumilie kama kuna matatizo yoyote kwenye chama, nakuomba ufanye uamuzi wa kishujaa utoke hadharani uombe msamaha kwa yote unayotuhumiwa nayo haafu uchukue hatua ya kuwaandikia barua ya kuomba msamaha viongozi wenzako. Ukifanya hivyo, utakuwa umeshinda vita zote zilizoko mbele yako na utaonekana shujaa ktk chama chako. Najua kwa kufanya hivyo, CCM watasikitika na kukusema kuwa umeisha kisiasa lakini mimi nadhani kuwa utakuwa umezikumbatia zile kura milioni 2.5 zilizopatikana kwenye uchaguzi uliopita na utakuwa umejitengenezea njia nzuri ya kuelekea 2015.

Mheshimiwa, ni vema nikasema kuwa ni heri kupiga hatua moja mbili nyuma kuliko kurudi mwanzo na kuanza upya ili uweze kusonga mbele. Wanaokwambia ujiondoe CHADEMA hawakutakii mema wewe binafsi wala chama chako na wale wanaosema ufukuzwe hawajui mtaji uliowekeza kwenye chama na wala hawakitakii chama chako prosperity. Ndugu yangu Zitto, nakuomba utumie changamoto zilizoko sasa ufanye siasa ambyo itakuimarisha wewe na chama chako ili hata wapinzani wako waanze kukuamini na kujua kuwa wewe ni kijogoo wa siasa za Chadema.

CHADEMA for Life.
Sikiliza sauti kutoka kwa mama yako Mzazi,
Heshimu viongozi wenzako na kila anayekutakia mema kwenye Chama

Uwiwanyu Agukunda
 
watamsamehe lakini hawata muhamini kamwe

Yeye ndiye atakaye fanya wote tumuamini. Nina hakika akifanya hili, sisi wapenzi wake na washabiki wa chama chake tutamuamini na sisi tutawalazimisha viongozi wenzake waanze kumuamini wapende wasipende,
 
.....kuongezea be careful na kiburi kutokana na kufahamika na vijisenti kuongezeka, hii inaweza kukuharibia sana!! ... nasikia we bado kijana mdogo, ebu heshimu hao wazee ikiwa ni pamoja na Dr wa kweli upate kufanikiwa!!
 
Tatizo lake huyu dogo tamaaaaaaaaaaaaaaaaaa ndio zinazomponzaaaaaaaaaaaaa na siku zote watu wenye tamaaa ni rahisi sana kutumiwa na watu kama ROSTAM AZIZ na wengine wengi tuuuuuuuuuuuuuuuuuu.acha tamaaaaa bwana mdogo.
 
zitto angekuwa msikivu angejirekebisha pale ilipoanza issue ya ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans! Sasa hivi anataka kufunga mlango wakati punda ameshatoka zizini! Shame on him! Ni pandikizi la CCM kama alivyokuwa Mrema! Damu yake na iwe juu ya kichwa chake mwenyewe wakati anasubiri rasmi kifo chake cha kisiasa!
 
wasiwasi wangu ni kua yawezekana ameshaingia mikataba na ccm ambayo kuivunja inamuwia vigumu.
 
Hoja imetulia ni fundisho kwa zitto na mamulluki wengine hii ni gharama ya kuwa kibaraka, inauuma saana. Kuwa kigeugeu au usaliti ni kitu kibaya saaaaana. Asante kwa ushauri uliotukuka
 
Wewe kichaka acha kutumia lugha chafu. Ukiona huwezi kufanya argument kwa kutumia lugha safi? Wewe unaonekana ni kibaraka wa ccm.
 
Yeye ndiye atakaye fanya wote tumuamini. Nina hakika akifanya hili, sisi wapenzi wake na washabiki wa chama chake tutamuamini na sisi tutawalazimisha viongozi wenzake waanze kumuamini wapende wasipende,


Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo, hapo kwenye RED naomba ufafanuzi, kwanza ningependa kujuwa jinsia yako, pili wewe kwenye chama unafuata itikadi au unafuata mtu? na ningeomba unijubu hapahapa nini falsafa ya CHADEMA? na je CHADEMA ni chama cha mlengo gani? na kama wewe ni mshabiki wa mtu na sio chama kama yule mtu akiamuwa kuhamia CCM uko tayari kwenda nae?
nakulilia Tanzania nchi yangu, ewe mungu muumba wa mbingu na nchi, naomba uwasaidie watanzania wenzangu waanze kutumia ubongo kufikiri badala ya kutumia tumbo kufikiri. AMAN WARID KABOURU anatoka kigoma na ndio alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA na sio naibu katibu mkuu.
Naomba Great thinker yeyote aimalizie hii post yangu, maana natype uku nimejawa na hasila naweza nikaaribu keyboard yangu.
 
Huyu ni kirusi na ameshakuwa bazazi la ccm hawezi kubadilika hata kama akiomba msamaha hawezi tengana kamwe na rostam(labda arudishe HAMMER alilompa),anajifanya kiburi na jeuri sana, atimuliwe tuu na sioni kama kutakuwa na adhari yoyote kwa chadema,kabwana mdogo kapuuzi sana haka.
 
Unasema kweli lakini Zitto ana ego problem sidhani kama atasikiliza ushauri wako. Imeripotiwa jana kwamba mamake anasema mwanae Zitto ni mbishi hashauriki kirahisi!!
 
Huo unaitwa WOSIA WA BABA! Safi sana ila wasiwasi wangu ni kama na yeye ni mwana JF na anaweza kupata ujumbe huu murwaaa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom