Natafuta kiki
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 911
- 1,284
Ndugu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa; pole na majukumu ya kitaifa.
Yah: KUZUILIWA UHAMISHO WA KUBADILISHANA.
Sisi watumishi wa serikali hususan kada ya Ualimu tunayo masikitiko makubwa sana pale tunapotaka kuhama kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine kwa njia ya kubadilishana lakini tunakutana na vikwazo kadhaa kama ifuatavyo.
1. Maafisa elimu kukataa kusaini barua za uhamisho
2. Wakurugenzi kukataa kusaini pia barua kwa kisingizio kwamba uhamisho umefungwa
3. Baadhi ya watumishi waliopo hapo ofisini TAMISEMI Dodoma kuwa na kauli mbaya dhidi ya watumishi wanaotaka kuhama hata kama ikiwa watumishi wanabadilishana vituo.
Tunafahamu kwamba uhamisho uliozuiliwa na serikali ni ule wa watumishi wanaotaka kuhama bila replacement yeyote hali iliyopelekea sehemu moja kuwa na upungufu na ndio maana mkazuia uhamisho huo.
Lakini pia kumekuwa na tabia ya upendeleo kwa baadhi ya walimu/watumishi kuhama ili hali wengine wanazuiliwa hali inayoonyesha viashiria vya rushwa.
Ombi letu:
1. Tunakuomba mheshimiwa Waziri ingilia hili suala kwani uhamisho wa kubadilishana hauna athari zozote yaani kila kituo kinakuwa na balance ya watumishi.
2. Utoe tamko rasmi kwa watumishi wa halmashauri ikiwemo wakurugenzi na maafisa elimu kwamba uhamisho wa kubadilishana usizuiiwe kwa namna yoyote ile.
3. Kukemea viashiria vyote vya rushwa hapo ofisini kwako TAMISEMI kwani kuna watumishi wachache wanaomba rushwa kwa watumishi ili wawasaidie kuhama.
Wako katika ujenzi wa taifa......
Walimu wanaobadilishana vituo vya kazi.