Barua ya wazi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa TAMISEMI na IGP

wehave

New Member
Jan 1, 2022
2
33
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MHESHIMIWA GEORGE SIMBACHAWENE (MB), WAZIRI WA TAMISEMI MHE UMMY MWALIMU PAMOJA NA IGP SIMON SIRO

Waheshimiwa viongozi. Shikamoo Waheshimiwa viongozi Nawasalimu kwa Jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania " kazi Iendele"Poleni kwa majukumu makubwa, mliyonayo lakini pia hongera kwa kuyatimiza kikamilifu majukumu makubwa mliyo nayo, ya kuliinua Taifa la Tanzania, Hakika mnafanya kazi nzito usiku na mchana bila kuchoka,

Ninaomba niwaangukie Waheshimiwa mawaziri wangu wa mambo ndani pamoja na TAMISEMI kwa kuandika barau hii ya wazi kwako hasa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI pamoja na IGP Ili muweze kunisaidia kwa mamlaka mliyopewa.

Mimi Geofrey Ernest ngatunga mkazi wilaya ya Mpwapwa, ambae pia ni mtumishi wa umma katika idara ya afya kituo changu cha kazi chunyu nafanya kazi kama Afisa Tabibu Daraja la pili. Mnamo tarehe 14 July 2021 niliakwa kuhudhuria mafunzo ya Nyenzo za upimaji wa virusi vya ukimwi nikiwa katika majukumu yangu ya kikazi mara baada ya kuisha mafunzo, mnamo tarehe 17-07-2021 nikiwa katika mitaa ya National saa 9:3spm tukiwa tunaelekea kupata chakula cha usiku nikiwa pamoja na rafiki yangu ndugu Mwita Makori, tulivamiwa na kukamatwa na watu wawili ambao usiku ule hatukuweza kuwatambua, hata hivyo hawakujitambulisha zaidi ya kutukaba na kuanza kutuvuta kuelekea sehemu ambayo walisema ni kituo cha polisi mpwapwa. Baada ya umbali kidogo, tulijikuta tupo katika kituo cha polisi cha Mpwapwa.

Baada ya kufika pale Askari polisi aitwae RAMIA KISEGE aliwapigia simu askari wengine wawili ili waje kituoni na kuwaambia kuwa yule mtu amekwisha patikana. Baada ya hapo mmoja wao akasema tuwafungulie mashtaka ya KUJIHUSISHA NA UHALIFU. Askari mmoja anaefahamika kwa Jina la AFANDE NANGU alimuita pembeni rafiki yangu.na kumuambia kuwa atoe kiasi cha SHILINGI LAKI MOJA ili aweze kuachiwa hali ya kuwa aliambiwa hana kosa,Mda huo ilikua tayari imeshakuwa saa nne usiku, mimi nikiwa nimewekwa chini, askari wanne akiwemo POLISI, RAMIA KISEGE, NANGU NA WENZIE WAWILI. Walianza kunishambulia kwa kunipiga na marungu, ngumi, makofi, mateke na kunikanyaga maeneo mbalimbali ya mwili wangu, bila kunipa ufafanuzi wa kosa langu ni UHALIFU gani ninao tuhumiwa nao.

Baada ya hapo nikahamishiwa kwenye chumba kingine ambapo askari hao walinipeleka, Tukiwa kule kwenye kile Chumba, Walianza kuniambia kuwa MIMI nimeshirikiana na askari police wa kituo cha mpwapwa kufanya utapeli kwa kutumia simu pamoja nakutoa siri za kituo, kitu ambacho niliwajibu sikifahamu na sijui chochote kuhusu hilo. Waliendelea kunipiga vibaya huku huku wakisema nimtaje askari ninae shirikiana nae hata kama ni OCD au askari yoyote mwenye cheo cha juu nimtaje. Polisi anaefahamika kwa Jina la RAMIA KiSEGE alionipa maelezo kuwa kwa kipindi kirefu siri za ndani ya kituo Chao cha polisi zimekua zikivuja, hivo ni lazima nimtajie kwa majina askari ninae shirikiana nae, huku akiitaja kesi ya mauaji iliyotokea kijiji cha galigali, kuwa nimekuwa nikipewa taarifa za muendelezo wa kesi hio, ikiwemo maandalizi ya majarada uchapaji wa majarada mpka kupelekea ndugu wa watuhumiwa wa kesi ya mauaji kutapeliwa kwa njia ya simu pamoja na kusema kwa uhakika kuwa sijui chochote kuhusu jambo hilo na wala sijawahi kufika kijiji hicho na sina mawasiliano na mtu wa kijiji anachokitaja na sikifahamu.

Bila kujali usalama wangu, Askari hao wanne waliendelea kunishambulia kwa kunipiga kinyama, huku wakitumia waya mweusi na marungu, ambapo wengine walitumia, ngumi mateke kunishambulia wakinitaka nimtaje askari ninae shirikiana nae. Huku askari anaefahamika kwa Jina la ramia AKINITISHA kuwa atanifungulia kesi ya madai na kumchafua kwani askari wenzie wamekua wakimshuku yeye ndie mtoa siri, Kitu ambacho sikuweza kukitaja kwa sababu sikufahamu chochote.

Baaada ya hapo mimi na rafiki yangu, tuliwekwa mahabusu.

Aidha tuliomba nafasi ya kutoa taarifa kwa ndugu au jamaaa wa karibu, nafasi hio tuliambiwa haipo. Siku ya tarehe 18 - 07-2021. Rafiki yangu yule ambae walisema hana kosa alikuja kuonwa na ndugu yake, na kutoa kiasi cha shilingi laki moja. Waka mkabidhi askari anaefahamika kwa Jina la NANGU. Kisha akachiwa. Mara baada ya kuachiwa. Ndipo akamtafuta mmoja ya watumishi wenzangu katika kituoninachofanyia kazi na kumpa taarifa kuwa. Nipo mahabusu. Aidha mtumishi yule alifanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya ya mpwapwa, na kumweleza jambo langu. Ambapo kutokana na kuwa ni usiku aliahidi kuwa tarehe 19 - 07-2021 atakuja kuniona.

Mara baada ya kufika tarehe 19-07-2021 mganga mkuu(w) alituma mwakilishi kwa ajili ya kuja kujua ninatuhumiwa na nini na kuona kama kosa linadhamika. Ndipo nikatolewa mahabusu na kuja kuonana na yule mwakilishi wa DMO Dr Charles Mara baada ya hapo DR. Akaambiwa kuwa natuhumiwa kwa kufanya utapeli, kwa njia ya mtandao. Na nilifanya utapeli wa kiasi cha shilingi laki 7. Hata hivyo hawakusema kuwa ni lini ulitokea na ni wapi, na ni nani aliyetapeliwa. Dr alipohoji kuhusu dhamana walimpa taarifa kuwa kuwa sihitaji dhamana wataniachia tu bila dhamana.

Mara baada ya kuondoka, wakaendelea kunifanyia vitendo vya kinyama, huku mmoja wa askari RAMIA akitamba kuwa pamoja na nafasi yangu kazini, amenizidi Mali na kila kitu. Huku akitamka wazi kuwa hata aje mkurugenzi, sitaachiwa, na sasa anataka nitapike kiasi cha SHILINGI milioni moja na laki tano i (1.5M),, ili niachiwe, wakati huo nikiwa nimelala chali.

Askari mmoja ambae anafahamika kwa Jina la Nangu. Aliniwekea ubao wenye sura ya ngao. Huku akijaribu kunikandamiza kifuani, na kuniambia kuwa kama nitaleta ubishi wowote atahakikisha naumia. Mara baaada ya mateso yale ya kinyama, kukandamizwa kiasi chakukosa pumzi. Niliamua nikubali kutoa pesa kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1.5M) ili niokoe, maisha yangu. Hii ni baada ya kuona naendelea kuteseka napewa kauli za vitisho na kudhalilishwa utu wangu. Nakumbuka askari mmoja Ramia alisema likiingia giza ntaona kitakachotokea. mara baada ya kusema kuwa nipo tayari, askari anafahamika kwa Jina la RAMIA KISEGE alinipa simu na kuniambia nimpigie simu rafiki yangu, alete kiasi cha Fedha wanachohitaji, wakati huo nilikua na kiasi shilingi laki 4 nikampigia simu rafiki yangu zichukue azilete.

Mara baaada ya kuzileta, wakadai ni kiasi kidogo, wanahitaji zaidi, rafiki yangu akanipa laki tatu, ndipo tukampa afande RAMIA KISEGE. Kiasi cha shilingi laki 7. Bado akasema kuwa anahitaji zaidi wakati wananikamata walinikuta Na ATM ya NMB, akaniambia kuwa nikatoe Fedha kwenye ATM. Nije nimalizane nae. Tukiwa watatu mimi, AFANDE RAMIA NA AFANDE NANGU. KUPITIA simu yake ya mikononi afande RAMIA alimpigia simu rafiki yangu, aje tena kituoni na kunilazimisha nimpatie kadi ya benki na namba za siri akatoe Fedha benki. Akampa ATM CARD na nikamwandikia namba za siri kiganjani akaenda benk ya NMB . Na kutoa kiasi cha Fedha shilingi 230,000tsh na kuileta kisha tukamkabidhi afande ramia. Jumla ya kiasi cha Fedha SHILINGI 930,000 Mara baada ya hapo nilianza kuulizwa historia ya maisha yangu. Huku askari anaefahamika kwa Jina la nangu akiandika kwenye karatasi. Baada ya hapo nikapewa nisaini. Kutokana na hali yangu kuwa mbaya kiafya pamoja na njaa kali siku zote nilizwekwa mahabusu sikula wala kunywa , sikuweza kusoma na kuelewa yaliyoandikwa kwa ufasaha.

Ninachokumbuka maelezo hayo yaliandikwa kuwa nilipata namba za watu waliotapeliwa kutoka kwenye sehemu ya kuuza pombe yaani kilabuni tulipokua tukinywa pombe. Hali ya kuwa niliwaeleza wazi kuwa sijawahi kutumia kilevi chochote, wala kujihusisha na uvutaji wa sigara. Wakanimbia saini usipo saini likiingia giza utaona kitakacho tokea hivyo kwa kuhofia usalama wangu nilisain ili niondoke mahali pale huku nikiamini mimi ni muhimu kuliko pesa wanazo hitaji.

Mara baada ya kumpatia kiasi kile cha Fedha. Askari mwingine wa umri wa kiutu uzima. Aliniambia kuwa nikitoka pale kituoni niende moja kwa moja nyumbani na ole wangu niseme chochote kilichotokea popote maana yeye AMESHIKA KWENYE MAKALI nakiasi cha shilingi 470,000 kilichobaki niende nikakitafute siku ya pili ambayo ni tarehe 20-07-2021 nikipeleke kiasi hicho kilichobaki. Nilipotoka pale, huku nikiwa sijiwezi nikijikongoja kwa kutembea hatua Chache na kupumzika. sikwenda nyumbani, nilienda moja moja hospital ya wilaya ya mpwapwa ili nikapate matibabu. Nilitibiwa. Nilipotoka pale tarehe 20-07-2021 nilipeleka malalamiko yangu ofisi za TAKUKURU wilaya ya mpwapwa nikiwataarifu hali halisi iliyokuwa lakini bado nahitajika kupeleka Fedha zilizobaki kiasi cha shilingi 470,000/= ambazo wameniambia nizipeleke kesho yake. Takukuru waliniambia nisipeleke kiasi hicho hadi pale watakapo nipa taarifa. lipofika siku ya pili tarehe 21-07-2021. Niliitwa kwenye kikao pamoja na TIMU YA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA WILAYA( CHMT) . Huku wakitaka nieleze kwa uwazi juu ya tukio hilo hata hivyo. Baada ya maelezo timu iliamua kupeleka malalamiko kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya. Tukiwa tumeongozana mimi pamoja na katibu afya na daktari ambae aliombwa atusindikize kwa mkuu wa wilaya, tulipo fika pale tukaambiwa mkuu wa wilaya yupo busy anajiandaa kwenda kwenye safari ya kikazi Tukawasilisha malalamiko yangu kwa Das, na akatuahidi atayafanyia kazi. Naye pia alishauri police niende tu nikaripoti lakini, nisipeleke kiasi kile cha fedha kilichobaki.

Hivyo siku ya tarehe 21-07-2021 nilikwenda polisi na kukutana na askari police RAMIA KISEGE Ambae aliniambia kuwa anafahamu kila sehemu nilipoenda baada ya kuachiwa katika kituo Chao cha polisi na nilienda kinyume na makubaliano. tarehe 29-07-2021 nikapigiwa simu NA TAKUKURU majira ya mchana saa 2:47pm nikielekezwa nikaonane na OCD pamoja na kutumiwa meseji yenye number za OCD , kwa hatua ili tatizo langu lifanyiwe utatuzi itarehe 2-8-2021

Nilienda kwa OCD a kaniambia yeye alikua hajui kesi yangu amejulishwa na mtu wa takukuru, baada ya hapo aliwahoji askari wake na kweli walikiri kuwapo kwa kesi yangu. Na ni kweli walichukua Fedha 930,000 na laki moja kutoka kwa rafiki yangu Mwita Makori Akanimbia kuwa amewapa siku saba wafanye Uchunguzi. Ili ukweli ujulikane hivyo Jumatatu kaniambia nikachukue majibu ya Uchunguzi ambapo amesema ikibainika sijahusika nitarudishiwa Fedha yangu.

Endapo kama nina husika nitapelekwa mahakamani, Jumatatu ya tarehe 09-08-2021 nilienda kuonana na OCD wa Mpwapwa, akamwita yule askari na kumuuuliza je upelelezi wa suala langu umefikia wapi. Akajibu bado ndo ameanza kufanya Uchunguzi Nikaambiwa inahitajika nikakae tena kwa muda wa siku saba nirudi tena ofisin kwake ikiwa jumla ya siku 14.

Nilipoona hivyo nikaamua kupeleka malalamiko kwa mkuu wa wilaya mpwapwa, hii ni kutokana na kwamba, nilichoka kusafiri nikiwa bado mgonjwa, pamoja na hayo niliumia kuona wananchi wa kituo ninachotoa tiba na kuwasaidia kina nili lazimika mda mwingine kuondoka huku wateja wakipata huduma kwa kuchelewa na wengine kukosa kabisa Mkuu wa wilaya alitupokea, na kunieleza kuwa malalamiko yangu niyaweke kwenye maaandishi na kuagiza madaktari wakanifanyie Uchunguzi na kunitibu na apelekewe ripoti ya matibabu yangu.

MPAKA LEO TAREHE 02-01-2022 tangu nilipokamatwa na kuteswa na kunyang'anywa Fedha zote nilizokuwa nazo Bado sijapata haki yangu yoyote, aidha nimekua nikiishi kwa wasiwasi mkubwa sana ,kwa sababu ya mmoja wa askari, alinipa onyo kuwa niondoke mpwapwa. Hata hivyo taarifa hiyo niliitoa kwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.

Na akanihakikishia hakuna kitakachotokea niwe na amani

Siku ya tarehe 9-10-2021 nilimpigia simu, OCD wa wilaya ya Mpwapwa nikimuulizia kuwa bado nasubiria majibu ya Uchunguzi ulionituhumu. Akaniambia yeye alikwisha fungua jalada na kulipeleka kwa RCO dodoma hivyo kama nina nafasi. Nifuatilie huko na RCO mkoani DODOMA Ndie mwenye mamlaka ya kusema nirudishiwe Fedha zangu au lah.

Askari hao wa kituo cha Mpwapwa, wamekua wakishirikiana mwanachi ambae askari mwenye Jina la RAMIA KISEGE alimtambulisha kama Girlfriend wake katika kufanya kazi za kukamatwa watu, na kuwaweka ndani. Huku mmoja ya watu anaoshirikiana nao anajulikana kwa Jina la magreth andarson. Ambae amekua akitumia majina tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti.

Mara baaada ya kumpigia simu alikiri wazi kuwa askari hao Ramia na nangu wamekuwa wakimtumia kwa kumpa namba za simu za watu wanao wataka au na badae yeye hupiga simu kwa kujifanya kakosea namba ili ajue walipo kisha badae hukamatwa. Na amesema mara nyingi amekua akishirikiana nao. Akitumia namba yake ya mkono 0657351216, 0623993125, Ambapo mara ya kwanza kunipigia ilikua ni 11-06-2021 saa 8:42 usiku na kisha kunitumia jumbe (sms) ambazo nilizihifadhi na mpka sasa ninazo. Akaja tena kunitafuta tarehe 7-7-2021 Hata hivyo alinitumia meseji kwenye namba zangu za simu, ambazo hadi sasa ninazo.

Na si namba walizonionesha pale kituoni

Waheshimiwa viongozi pamoja na IGP SIMON SIRO binafsi sitasahau unyama niliofanyiwa na askari hao Ramia na wenzake. Mpaka sasa ninavyoandika barua hii nimepoteza uwezo wangu wa kukaa muda mrefu, nikikaa muda mchache napatwa maumiwa makali ya pingili za mgongo. Hali inayoathiri mwenendo wa maisha niliyoyazoea hapo awali.

Pamoja na yote nina mashahidi wa kutosha na vielelezo vya kutosha vya kuthibitisha madai yangu MHESHIMIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MHESHIMIWA GEORGE SIMBACHAWENE (MB) na WAZIRI WA TAMISEMI PAMOJA NA IGP SIRO Nina waomba sana hili suala liangaliwe kwa jicho la kipekee, binafsi nipo tayari kutoa ushirikiano wote, aidha naamini kabisa nchi yetu imepevuka kitechnologia na si rahisi kwa mtu yeyote kukwepa mkono wa sheria kwani Uchunguzi utafanyika na kuweza kubaini ukweli

Hawa askari wawili Ramia na mwenzake nangu walinifanyia unyama bila sababu za msingi ikiwa ni pamoja kuninyang'anya Fedha niliyoitafuta kwa jasho langu . Hadi sasa Nimekuwa nikisumbuliwa na matatizo ya mgongo matatizo ambayo sikuwahi kuwa nayo. Walidai mimi nilikua natumia namba ya airtel ambayo wanayo wao. TANGU siku ya kwanza huyo askari ramia kisege alikua ananipigia kwenye namba yangu hata siku ya kwanza yule mwanachi wanaemtuma alinipigia simu alipiga kwenye namba yangu ya simu na sio namba ya simu waliyonionesha nikiwa pale kituoni.

Mimi sifahamu chochote kile kuhusu matukio ya mauaji yaliyo tokea gali gali na sijawahi kushirikiana na askari yoyote kufanya utapeli,sina uwezo wa kujua chochote juu ya kinachoendelea kwenye kituo cha polisi mimi kwenye wilaya hii ni mgeni nimeajiriwa miaka ya hivi karibun tu lakini nimekutana na manyanyaso na mateso makuu.

Naomba nisaidiwe kwa kadri ya uwezo wako. niliwahi kupiga simutigo huduma kwa wateja nikauliza kwann mtu apige namba ya simu nyingine . Afu iite simu yangu mimi wakasema haiwezekani. Hao askari walisisitiza sana na kusema wao wameshika kwenye makali wanaweza kufanya lolote juu yangu naomba viongozi mnisaidie kwa uwezo wenu wote niishi kwa amani.

Binafsi yangu nimehangaika kila sehemu, Tangu tarehe 20-07-2021 hadi Leo tarehe 02-01-2022 hata kuhakikisha kwamba haki yangu inapatikana. Lakini hadi sasa sijapata kitu. Pamoja na kudhurumu haki yangu, kuniharibia sifa yangu katika jamii, kunishambulia bila sababu askari hao wamenifanya niishi kwa tabu na wasiwasi mkubwa ndani ya wilaya ninayofanyia kazi.

Hata hivyo naomba serikali inibadilishie kituo cha kazi na inipeleke sehemu yoyote yenye uhitaji

Nina imani kubwa na serikali yangu kwamba, Uchunguzi wa kina utafanyanyika ili kubaini ukweli wa tukio hili,niweze kupata haki yangu,

Pamoja na yote yaliyotokea naamini Uchunguzi utafanyika na ukweli utafahamika

Pia ninaiomba serikali baada ya kufanya Uchunguzi iwafungulie kesi ndugu Ramia KISEGE na wenzake kwani wametumia vibaya nafasi zao za kuwa askari pamoja na kujipatia Fedha kwa mabavu.

MHE RAIS, WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SAMIA SULUHU HASSAN, amekua akisisitiza siku zote juu ya haki sawa kwa wananchi wake. Amesisitiza mara nyingi kuwa sisi sote ni sawa mbele sheria,Ninawaomba Viongozi mbalimbali, watakao ona ujumbe huu wausogeze karibu na waziri wa mambo ya ndani, au ikiwezekana hata mbele ya RAIS ili waweze kunisaidia. Mungu ibariki Tanzania.

Geofrey Ernest ngatunga

Mpwapwa DC, DODOMA

0742366180, 0676660359
 
pole sana pia embu jitathmini hujawahi tembea na mke wa mtu uko au kutafuna tamu ya mkubwa?

kama sio basi hao uliowshtumu ni wahalifu na si askari,ungekariri na namba zao ingekua vyema sana.

Askari wanaodhulumu mwisho wao ni mbaya sana
 
Du hii ni kashfa kubwa sana kwa Jeshi la polisi. Kama kweli alitenda kosa walilomtuhumu nalo kwa vyovyote wangempeleka mahakamani na wasingemwachia bila dhamana.

Pili kitendo cha kutaka pesa na kukiri kwa OCD (kama ni kweli) basi ni mtandao mpana wa Rushwa ambao hata baadhi ya viongozi wao wanahusishwa.

Mtuhumiwa akitoa pesa yeyote kituoni lazima irekodiwe na ihifadhiwe sehemu salama lakini huo OCD hata hakutaka kujua ilipo hiyo fedha.

Hawa ndio wanalichafua jeshi
 
Mpaka OCD anashirikiana na polisi wahalifu kupora fedha za raia maana yake ni kwamba adkari wetu wengi ni majambazi na wanawafanyia uhalifu raia kinyume na jukumu lao la kuwalinda raia.

Mkuu wa Wilaya naye ni bure kabisa, kuna jambo halipo sawa. Nakumbuka kuna incident kama.hiyo ilitokea kwa Mtu mmoja wilaya ya Temeke ambapo polisi walitishia kumuua kwa risasi na bahati nzuri aliokewa na mkuu mmoja wa kituo lakini suala lilipofika kwa OCD na DC walilipotezea huku muathirika akishaeishiwa kupokea kiasi cha fedha yaishe.

Vetting zinafanyika kwa kuangalia CV za watu na siyo tija zao
 
BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MHESHIMIWA GEORGE SIMBACHAWENE (MB), WAZIRI WA TAMISEMI MHE UMMY MWALIMU PAMOJA NA IGP SIMON SIRO

Waheshimiwa viongozi. Shikamoo Waheshimiwa viongozi Nawasalimu kwa Jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania " kazi Iendele"Poleni kwa majukumu makubwa, mliyonayo lakini pia hongera kwa kuyatimiza kikamilifu majukumu makubwa mliyo nayo, ya kuliinua Taifa la Tanzania, Hakika mnafanya kazi nzito usiku na mchana bila kuchoka,

Ninaomba niwaangukie Waheshimiwa mawaziri wangu wa mambo ndani pamoja na TAMISEMI kwa kuandika barau hii ya wazi kwako hasa WAZIRI WA MAMBO YA NDANI pamoja na IGP Ili muweze kunisaidia kwa mamlaka mliyopewa.

Mimi Geofrey Ernest ngatunga mkazi wilaya ya mpwapwa, ambae pia ni mtumishi wa umma katika idara ya afya kituo changu cha kazi chunyu nafanya kazi kama Afisa Tabibu Daraja la pili. Mnamo tarehe 14 July 2021 nialikwa kuhudhuria mafunzo ya Nyenzo za upimaji wa virusi vya ukimwi nikiwa katika majukumu yangu ya kikazi mara baada ya kuisha mafunzo ,mnamo tarehe 17-07-2021 nikiwa katika mitaa ya National saa 9:3spm tukiwa tunaelekea kupata chakula cha usiku nikiwa pamoja na rafiki yangu ndugu mwita makori, Tulivamiwa na kukamatwa na watu wawili ambao usiku ule hatukuweza kuwatambua, hata hivyo hawakujitambulisha zaidi ya kutukaba na kuanza kutuvuta kuelekea sehemu ambayo walisema ni kituo cha polisi mpwapwa. Baada ya umbali kidogo, tulijikuta tupo katika kituo cha polisi cha mpwapwa.

Baada ya kufika pale Askari polisi aitwae RAMIA KISEGE aliwapigia simu askari wengine wawili ili waje kituoni na kuwaambia kuwa yule mtu amekwisha patikana. Baada ya hapo mmoja wao akasema tuwafungulie mashtaka ya KUJIHUSISHA NA UHALIFU. Askari mmoja anaefahamika kwa Jina la AFANDE NANGU alimuita pembeni rafiki yangu.na kumuambia kuwa atoe kiasi cha SHILINGI LAKI MOJA ili aweze kuachiwa hali ya kuwa aliambiwa hana kosa,Mda huo ilikua tayari imeshakuwa saa nne usiku, mimi nikiwa nimewekwa chini, askari wanne akiwemo POLISI, RAMIA KISEGE, NANGU NA WENZIE WAWILI. Walianza kunishambulia kwa kunipiga na marungu, ngumi, makofi, mateke na kunikanyaga maeneo mbalimbali ya mwili wangu, bila kunipa ufafanuzi wa kosa langu ni UHALIFU gani ninao tuhumiwa nao.

Baada ya hapo nikahamishiwa kwenye chumba kingine ambapo askari hao walinipeleka, Tukiwa kule kwenye kile Chumba, Walianza kuniambia kuwa MIMI nimeshirikiana na askari police wa kituo cha mpwapwa kufanya utapeli kwa kutumia simu pamoja nakutoa siri za kituo, kitu ambacho niliwajibu sikifahamu na sijui chochote kuhusu hilo. Waliendelea kunipiga vibaya huku huku wakisema nimtaje askari ninae shirikiana nae hata kama ni OCD au askari yoyote mwenye cheo cha juu nimtaje. Polisi anaefahamika kwa Jina la RAMIA KiSEGE alionipa maelezo kuwa kwa kipindi kirefu siri za ndani ya kituo Chao cha polisi zimekua zikivuja, hivo ni lazima nimtajie kwa majina askari ninae shirikiana nae, huku akiitaja kesi ya mauaji iliyotokea kijiji cha galigali, kuwa nimekuwa nikipewa taarifa za muendelezo wa kesi hio, ikiwemo maandalizi ya majarada uchapaji wa majarada mpka kupelekea ndugu wa watuhumiwa wa kesi ya mauaji kutapeliwa kwa njia ya simu pamoja na kusema kwa uhakika kuwa sijui chochote kuhusu jambo hilo na wala sijawahi kufika kijiji hicho na sina mawasiliano na mtu wa kijiji anachokitaja na sikifahamu.

Bila kujali usalama wangu, Askari hao wanne waliendelea kunishambulia kwa kunipiga kinyama, huku wakitumia waya mweusi na marungu, ambapo wengine walitumia, ngumi mateke kunishambulia wakinitaka nimtaje askari ninae shirikiana nae. Huku askari anaefahamika kwa Jina la ramia AKINITISHA kuwa atanifungulia kesi ya madai na kumchafua kwani askari wenzie wamekua wakimshuku yeye ndie mtoa siri, Kitu ambacho sikuweza kukitaja kwa sababu sikufahamu chochote.

Baaada ya hapo mimi na rafiki yangu, tuliwekwa mahabusu.

aidha tuliomba nafasi ya kutoa taarifa kwa ndugu au jamaaa wa karibu, nafasi hio tuliambiwa haipo. Siku ya tarehe 18 - 07-2021. Rafiki yangu yule ambae walisema hana kosa alikuja kuonwa na ndugu yake, na kutoa kiasi cha shilingi laki moja. Waka mkabidhi askari anaefahamika kwa Jina la NANGU. Kisha akachiwa. Mara baada ya kuachiwa. Ndipo akamtafuta mmoja ya watumishi wenzangu katika kituoninachofanyia kazi na kumpa taarifa kuwa. Nipo mahabusu. Aidha mtumishi yule alifanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya ya mpwapwa, na kumweleza jambo langu. Ambapo kutokana na kuwa ni usiku aliahidi kuwa tarehe 19 - 07-2021 atakuja kuniona.

Mara baada ya kufika tarehe 19-07-2021 mganga mkuu(w) alituma mwakilishi kwa ajili ya kuja kujua ninatuhumiwa na nn na kuona kama kosa linadhamika. Ndipo nikatolewa mahabusu na kuja kuonana na yule mwakilishi wa DMO Dr CharlesMara baada ya hapo DR. Akaambiwa kuwa natuhumiwa kwa kufanya utapeli, kwa njia ya mtandao. Na nilifanya utapeli wa kiasi cha shilingi laki 7.hata hivyo hawakusema kuwa ni lini ulitokea na ni wapi, na ni nani aliyetapeliwa. Dr alipohoji kuhusu dhamana walimpa taarifa kuwa kuwa sihitaji dhamana wataniachia tu bila dhamana.

Mara baaada ya kuondoka, wakaendelea kunifanyia vitendo vya kinyama, huku mmoja wa askari RAMIA akitamba kuwa pamoja na nafasi yangu kazini, amenizidi Mali na kila kitu. Huku akitamka wazi kuwa hata aje mkurugenzi, sitaachiwa, na sasa anataka nitapike kiasi cha SHILINGI milioni moja na laki tano i (1.5M),, ili niachiwe,wakati huo nikiwa nimelala chali.

Askari mmoja ambae anafahamika kwa Jina la nangu. Aliniwekea ubao wenye sura ya ngao. Huku akijaribu kunikandamiza kifuani, na kuniambia kuwa kama nitaleta ubishi wowote atahakikisha naumia. Mara baaada ya mateso yale ya kinyama, kukandamizwa kiasi chakukosa pumzi. Niliamua nikubali kutoa pesa kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1.5M).ili niokoe, maisha yangu.hii ni baada ya kuona naendelea kuteseka napewa kauli vitisho na kudharirishwa utu wangu. Nakumbuka askari mmoja ramia alisema likiingia giza ntaona kitakachotokea. mara baada ya kusema kuwa nipo tayari, askari anafahamika kwa Jina la RAMIA KISEGE alinipa simu na kuniambia nimpigie simu rafiki yangu, alete kiasi cha Fedha wanachohitaji, wakati huo nilikua na kiasi shilingi laki 4 nikampigia simu rafiki yangu zichukue azilete.

Mara baaada ya kuzileta, wakadai ni kiasi kidogo, wanahitaji zaidi, rafiki yangu akanipa laki tatu, ndipo tukampa afande RAMIA KISEGE. Kiasi cha shilingi laki 7. Bado akasema kuwa anahitaji zaidi wakati wananikamata walinikuta Na ATM ya NMB, akaniambia kuwa nikatoe Fedha kwenye ATM. Nije nimalizane nae. Tukiwa watatu mimi, AFANDE RAMIA NA AFANDE NANGU.KUPITIA simu yake ya mikononi afande RAMIA alimpigia simu rafiki yangu, aje tena kituoni nakunilazimisha nimpatie kadi ya benki na namba za siri akatoe Fedha benki. Akampa ATM CARD na nikamwandikia namba za siri kiganjani i akaenda benk ya NMB . Na kutoa kiasi cha Fedha shilingi 230,000tsh na kuileta kisha tukamkabidhi afande ramia. Jumla ya kiasi cha Fedha SHILINGI 930,000 Mara baada ya hapo nilianza kuulizwa historia ya maisha yangu. Huku askari anaefahamika kwa Jina la nangu akiandika kwenye karatasi. Baada ya hapo nikapewa nisaini. Kutokana na hali yangu kuwa mbaya kiafya pamoja na njaa kali siku zote nilizwekwa mahabusu sikula wala kunywa , sikuweza kusoma na kuelewa yaliyoandikwa kwa ufasaha.

Ninachokumbuka maelezo hayo yaliandikwa kuwa nilipata namba za watu waliotapeliwa kutoka kwenye sehemu ya kuuza pombe yaani kilabuni tulipokua tukinywa pombe. Hali ya kuwa niliwaeleza wazi kuwa sijawahi kutumia kilevi chochote, wala kujihusisha na uvutaji wa sigara. Wakanimbia saini usipo saini likiingia giza utaona kitakacho tokea hivyo kwa kuhofia usalama wangu nilisain ili niondoke mahali pale huku nikiamini mimi ni muhimu kuliko pesa wanazo hitaji.

Mara baada ya kumpatia kiasi kile cha Fedha. Askari mwingine wa umri wa kiutu uzima. Aliniambia kuwa nikitoka pale kituoni niende moja kwa moja nyumbani na ole wangu niseme chochote kilichotokea popote maana yeye AMESHIKA KWENYE MAKALI nakiasi cha shilingi 470,000 kilichobaki niende nikakitafute siku ya pili ambayo ni tarehe 20-07-2021 nikipeleke kiasi hicho kilichobaki. Nilipotoka pale, huku nikiwa sijiwezi nikijikongoja kwa kutembea hatua Chache na kupumzika. sikwenda nyumbani, nilienda moja moja hospital ya wilaya ya mpwapwa ili nikapate matibabu. Nilitibiwa. Nilipotoka pale tarehe 20-07-2021 nilipeleka malalamiko yangu ofisi za TAKUKURU wilaya ya mpwapwa nikiwataarifu hali halisi iliyokuwa lakini bado nahitajika kupeleka Fedha zilizobaki kiasi cha shilingi 470,000/= ambazo wameniambia nizipeleke kesho yake. Takukuru waliniambia nisipeleke kiasi hicho hadi pale watakapo nipa taarifa. lipofika siku ya pili tarehe 21-07-2021. Niliitwa kwenye kikao pamoja na TIMU YA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA WILAYA( CHMT) . Huku wakitaka nieleze kwa uwazi juu ya tukio hilo hata hivyo. Baada ya maelezo timu iliamua kupeleka malalamiko kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya. Tukiwa tumeongozana mimi pamoja na katibu afya na daktari ambae aliombwa atusindikize kwa mkuu wa wilaya, tulipo fika pale tukaambiwa mkuu wa wilaya yupo busy anajiandaa kwenda kwenye safari ya kikazi Tukawasilisha malalamiko yangu kwa Das, na akatuahidi atayafanyia kazi. Naye pia alishauri police niende tu nikaripoti lakini, nisipeleke kiasi kile cha fedha kilichobaki.

Hivyo siku ya tarehe 21-07-2021 nilikwenda polisi na kukutana na askari police RAMIA KISEGE Ambae aliniambia kuwa anafahamu kila sehemu nilipoenda baada ya kuachiwa katika kituo Chao cha polisi na nilienda kinyume na makubaliano. tarehe 29-07-2021 nikapigiwa simu NA TAKUKURU majira ya mchana saa 2:47pm nikielekezwa nikaonane na OCD pamoja na kutumiwa meseji yenye number za OCD , kwa hatua ili tatizo langu lifanyiwe utatuzi itarehe 2-8-2021

nilienda kwa OCD a kaniambia yeye alikua hajui kesi yangu amejulishwa na mtu wa takukuru, baada ya hapo aliwahoji askari wake na kweli walikiri kuwapo kwa kesi yangu. Na ni kweli walichukua Fedha 930,000 na laki moja kutoka kwa rafiki yangu mwita makori Akanimbia kuwa amewapa siku saba wafanye Uchunguzi. Ili ukweli ujulikane hivyo jumatatu kaniambia nikachukue majibu ya Uchunguzi.Ambapo amesema ikibainika sijahusika nitarudishiwa Fedha yangu.

Endapo kama nina husika nitapelekwa mahakamani , juma tatu ya tarehe 09-08-2021 nilienda kuonana na OCD wa mpwapwa, akamwita yule askari na kumuuuliza je upelelezi wa suala langu umefikia wapi. A kajibu bado ndo ameanza kufanya Uchunguzi Nikaambiwa inahitajika nikakae tena kwa muda wa siku saba nirudi tena ofisin kwake ikiwa jumla ya siku 14.

Nilipoona hivyo nikaamua kupeleka malalamiko kwa mkuu wa wilaya mpwapwa, hii ni kutokana na kwamba, nilichoka kusafiri nikiwa bado mgonjwa, pamoja na hayo niliumia kuona wananchi wa kituo ninachotoa tiba na kuwasaidia kina nili lazimika mda mwingine kuondoka huku wateja wakipata huduma kwa kuchelewa na wengine kukosa kabisa Mkuu wa wilaya alitupokea, na kunieleza kuwa malalamiko yangu niyaweke kwenye maaandishi na kuagiza madaktari wakanifanyie Uchunguzi na kunitibu na apelekewe ripoti ya matibabu yangu.

MPAKA LEO TAREHE 02-01-2022 tangu nilipokamatwa na kuteswa na kunyang'anywa Fedha zote nilivokua nazo Bado sijapata haki yangu yoyote, aidha nimekua nikiishi kwa wasiwasi mkubwa sana ,kwa sababu ya mmoja wa askari, alinipa onyo kuwa niondoke mpwapwa.Hata hivyo taarifa hiyo niliitoa kwa mkuu wa wilaya ya mpwapwa.

Na akanihakikishia hakuna kitakachotokea niwe na amani

Siku ya tarehe 9-10-2021 nilimpigia simu, OCD wa wilaya ya mpwapwa nikimuulizia kuwa bado nasubiria majibu ya Uchunguzi ulio nituhumu. Akaniambia yeye alikwisha fungua jarada na kulipeleka kwa RCO dodoma hivyo kama nina nafasi. Nifuatilie uko na RCO mkoani DODOMA Ndie mwenye mamlaka ya kusema nirudishiwe Fedha zangu au lah.

Askari hao wa kituo cha mpwapwa, wamekua wakishirikiana mwanachi ambae askari mwenye Jina la RAMIA KISEGE alimtambulisha kama Girlfriend wake katika kufanya kazi za kukamatwa watu, na kuwaweka ndani. Huku mmoja ya watu anaoshirikiana nao anajulikana kwa Jina la magreth andarson. Ambae amekua akitumia majina tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti.

Mara baaada ya kumpigia simu alikiri wazi kuwa askari hao Ramia na nangu wamekuwa wakimtumia kwa kumpa namba za simu za watu wanao wataka au na badae yeye hupiga simu kwa kujifanya kakosea namba ili ajue walipo kisha badae hukamatwa. Na amesema mara nyingi amekua akishirikiana nao. Akitumia namba yake ya mkono 0657351216, 0623993125, Ambapo mara ya kwanza kunipigia ilikua ni 11-06-2021 saa 8:42 usiku na kisha kunitumia jumbe (sms) ambazo nilizihifadhi na mpka sasa ninazo. Akaja tena kunitafuta tarehe 7-7-2021 Hata hivyo alinitumia meseji kwenye namba zangu za simu, ambazo hadi sasa ninazo.

Na si namba walizonionesha pale kituoni

Waheshimiwa viongozi pamoja na IGP SIMON SIRO binafsi sitasahau unyama niliofanyiwa na askari hao Ramia na wenzake. Mpaka sasa ninavyoandika barua hii nimepoteza uwezo wangu wa kukaa mda mrefu, nikikaa mda mchache napatwa maumiwa makali ya pingili za mgongo. Hali inayo athiri mwenendo wa maisha niliyo yazoea hapo awali.

Pamoja na yote nina mashahidi wa kutosha na vielelezo vya kutosha vya kuthibitisha madai yangu MHESHIMIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, MHESHIMIWA GEORGE SIMBACHAWENE (MB) na WAZIRI WA TAMISEMI PAMOJA NA IGP SIRO Nina waomba sana hili suala liangaliwe kwa jicho la kipekee, binafsi nipo tayari kutoa ushirikiano wote, aidha naamini kabisa nchi yetu imepevuka kitechnologia na si rahisi kwa mtu yeyote kukwepa mkono wa sheria kwani Uchunguzi utafanyika na kuweza kubaini ukweli

Hawa askari wawili Ramia na mwenzake nangu walinifanyia unyama bila sababu za msingi ikiwa ni pamoja kuninyang'anya Fedha niliyoitafuta kwa jasho langu . Hadi sasa Nimekuwa nikisumbuliwa na matatizo ya mgongo matatizo ambayo sikuwahi kuwa nayo. Walidai mimi nilikua natumia namba ya airtel ambayo wanayo wao. TANGU siku ya kwanza huyo askari ramia kisege alikua ananipigia kwenye namba yangu hata siku ya kwanza yule mwanachi wanaemtuma alinipigia simu alipiga kwenye namba yangu ya simu na sio namba ya simu waliyonionesha nikiwa pale kituoni.

Mimi sifahamu chochote kile kuhusu matukio ya mauaji yaliyo tokea gali gali na sijawahi kushirikiana na askari yoyote kufanya utapeli,sina uwezo wa kujua chochote juu ya kinachoendelea kwenye kituo cha polisi mimi kwenye wilaya hii ni mgeni nimeajiriwa miaka ya hivi karibun tu lakini nimekutana na manyanyaso na mateso makuu.

Naomba nisaidiwe kwa kadri ya uwezo wako. niliwahi kupiga simutigo huduma kwa wateja nikauliza kwann mtu apige namba ya simu nyingine . Afu iite simu yangu mimi wakasema haiwezekani. Hao askari walisisitiza sana na kusema wao wameshika kwenye makali wanaweza kufanya lolote juu yangu naomba viongozi mnisaidie kwa uwezo wenu wote niishi kwa amani.

Binafsi yangu nimehangaika kila sehemu,Tangu tarehe 20-07-2021 hadi Leo tarehe 02-01-2022 hata kuhakikisha kwamba haki yangu inapatikana. Lakini hadi sasa sijapata kitu. Pamoja na kudhurumu haki yangu, kuniharibia sifa yangu katika jamii, kunishambulia bila sababu askari hao wamenifanya niishi kwa tabu na wasiwasi mkubwa ndani ya wilaya ninayofanyia kazi.

Hata hivyo naomba serikali inibadilishie kituo cha kazi na inipeleke sehemu yoyote yenye uhitaji

Nina imani kubwa na serikali yangu kwamba, Uchunguzi wa kina utafanyanyika ili kubaini ukweli wa tukio hili,niweze kupata haki yangu,

Pamoja na yote yaliyotokea naamini Uchunguzi utafanyika na ukweli utafahamika

Pia nina iomba serikali baada ya kufanya Uchunguzi iwafungulie kesi ndugu ramia KISEGE na wenzake kwani wametumia vibaya nafasi zao za kuwa askari pamoja na kujipatia Fedha kwa mabavu.

MHE RAIS, WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SAMIA SULUHU HASSAN, amekua akisisitiza siku zote juu ya haki sawa kwa wananchi wake. Amesisitiza mara nyingi kuwa sisi sote ni sawa mbele sheria,Ninawaomba Viongozi mbalimbali, watakao ona ujumbe huu wausogeze karibu na waziri wa mambo ya ndani, au ikiwezekana hata mbele ya RAIS ili waweze kunisaidia. Mungu ibariki Tanzania.

Geofrey Ernest ngatunga

Mpwapwa DC, DODOMA

0742366180, 0676660359
Pole sana ,soon hao mbwa watakuwa nje ya ulingo , trust me

USSR
 
Daaa 🥲kama ni kweli afu mtu akirudia ya hamza hapa lawama zinaanza mkuu fanya ufanyavyo usipoteze haki yako mfanye lolote nenda hata kwa wataalamu waloge yani usikubali kuonewa mpige tukio la kihistoria maswala ya rco na dco bila konekesheni unapoteza mda huyo askari mpige tukio tu roho imeniuma asee
 
Back
Top Bottom