Barua ya wazi kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu

Ngomile

Member
Mar 18, 2018
18
14
Kwako mheshiwa waziri,

imani yangu ujumbe huu utausoma wewe binafsi ama wasaidizi wako watakufishia.
Mh, waziri mimi ni miongoni mwa watumishi wizara ya afya nikifanya kazi moja ya hospital za mikoa hapa Tz chini ya wizara yako.

Mimi binafsi ninayo masononeko makubwa sana, ingawa na wengine pia wapo najua kwa kuwa nilikuwa nao wakati wa hili ninalokwenda kulieleza hapa chini.

Masononeko haya yanauchoma sana moyo wangu mimi binafsi kwa kuwa nimejiridhisha pasi na chembe ya mashaka kuwa tunabaniwa pasi na sababu za msingi za kisheria sisi baadhi watumishi tulio chini ya wizara yako.

Mnaomo tarehe 15 mpaka tarehe 29 mwezi wa nane, palifanyika usaili wa taasisi mbalimbali za serikali kupitia sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma.

Katika tangozo lao la ajira sekretarieti ya ajira walitangaza kuwa hata watu walio kwenye utumishi wa umma tayari wanaruhusiwa kuomba kwa sharti tu barua yako ya maombi ipitishwe na mwajiri wako.

Baadhi ya tulio wengi tuliitikia wito huo na tukaomba mie nikiwemo na tukaitwa kwenye usaili katika hatua kadhaa na mwisho tulifuzu usaili huo.

Sasa kinacholeta sonono kubwa moyoni kuwa, mara baada ya usaili tuliofaulu usaili huo kutangazwa tulipokea barua za kuitwa kazini na taratibu zingine kufuata, pamoja na kutoa taarifa kwa katibu mkuu wizarani ambaye ndiye muajiri kuhusu kusudio la kuhamisha utumishi kwenda kwenye taasisi nyingine ambayo ni MOI.

Tuliandika barua kumjulisha katibu mkuu kupitia kwa wasimamizi wa vituo vyetu vya kazi na kupitishiwa na wasimamizi.
Balaa linakuja baada ya kufika wizarani pasipo sababu zinazo eleweka wakurugenzi wamezirudisha barua zetu na kutukatalia kuondoka kwenda kufanya kazi MOI na hospital ya Taifa Muhimbili.

Kwa kweli tulijitahidi sana kufanya jitihada tuonane na wakurugenzi wizarani baada ya kuambiwa katibu mkuu hayupo ofisini kweli tulifanikiwa kuonana nao, lkn majibu hayajakidhi haja na kutuacha tukisononeka mioyo yetu.

Sasa ikiwa pasi na chembe ya shaka kwamba utaratibu unaruhusu na tukafuata, sijapata sababu ya kwanini tunazuiliwa kwenda kufanya kazi taasisi nyingine tena chuni ya serikali moja.

Huku ikizingatiwa kwa kweli watu tuliona hii ni kama fursa kupanda juu baada ya kutumika vituoni kwetu kwa muda wa kutosha na vile vile firsa pia kusogea karibu na familia baada ya muda mrefu sana mbali na familia zetu.

Tulipata faraja sana kupata nafasi lakinj matarajio yamekuwa tofauti sana mheshiwa waziri.

Tukizingatia pia kwamba lipo agizo la waziri wa utumishi wa umma kuzuia kwa muda uhamisho wa watumishi kuweka utaratibu sawa, lakini kwa suala hili liko tofauti hauwi uhamisho bali mtumishi kutoka kwa muajiri katibu mkuu kwenda kwa taasisi chini ya mkurugenzi. Wakati huo huo kuna agizo la waziri mkuu kuwa hata kama watumishi wanataka kuhama basi wasizuiwe.

Hivyo nikuombe muheshimiwa waziri hata kama sio sasa kwa nyakati za baadae muwaache huru watumishi pasi na kuvunja utaratibu wa utumishi wa umma kama zinamruhusu aruhusiwe tu. Hii itasaidia kufanya kazi kwa ari na kuoongeza morari ya kazi kwa mtu kufanya kazi sehemu anayopenda baada ya kufanya jitihada za kuoambana sana kwenye usaili.

Hili binafsi linaua morali ya kazi kabisa mheshimiwa wangu.
Mie bado naamini kuwa serikali yetu sikivu nawe mheshiwa wetu na watendaji ni wasikivu chini ya kiongozi wetu mh rais, utakaa tena na watendaji wako kuliangalia jambo hili linaumiza mno likimpata mtumishi kukosa fursa muhimu kwa jambo ambalo lipo ndani ya utaratibu kabisa.
Kwa unyenyekevu mkubwa sana nikutakie utumishi mwema uliotukuka.

Wako katika utumishi.
Kijr.
 
pole mkuu, Hata mimi imenishangaza kusikia hivyo. naamini waziri na wasaidizi wake ni wadau wa JF , watalisolve hilo

ila ungekuwa wazi kuwa sababu za kulilia MOI na Muhimbili ni dau nono (ikumbukwe kwa taasis hizo take home ni mara mbili ya huko ulipokuwa)
 
Pamoja na nayo mkuu mapato ni motisha ya katika kazi. Nashukuru kwa pole!
pole mkuu, Hata mimi imenishangaza kusikia hivyo. naamini waziri na wasaidizi wake ni wadau wa JF , watalisolve hilo

ila ungekuwa wazi kuwa sababu za kulilia MOI na Muhimbili ni dau nono (ikumbukwe kwa taasis hizo take home ni mara mbili ya huko ulipokuwa)
 
Back
Top Bottom