Barua ya wazi kwa Waziri wa Afya, Bi. Ummy Mwalimu

Uta Uta

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
3,353
2,000
MH Waziri pole kwa majukumu ya ujenzi wa taifa.

Mh Waziri tumeitikia kwa dhati wito wako ulioutoa kwa jamii nzima ya watanzania kuhahkikisha wanapata kadi za bima za afya wao na familia zao. Tunashukuru lengo ni zuri na inatusaidia sana sisi wa kipato cha chini kupata matibabu ya gharama nafuu. Tumesikia na tumeitikia azma ya serikari ili tupate afya bora.

Mh Waziri sisi watumiaji wa bima ya afya NHIF tunapata mateso na manyanyaso makubwa sana katika baadhi ya vituo vya kutoa huduma ya afya vinavyomilikiwa na serikali. Katika kiyuo cha Mbagala kizuani kila siku ukienda unaambiwa mtandao hakuna ukitaka huduma ulipe fedha au uende kituo cha jirani. Mh hii inauma sana mi nimeshaenda zaidi ya mara tano toka mwaka jana ila tatizo ni lile lie.

Mh waziri naomba utusaidie kukosekana kwa mtandao mimi mwananchi kuna nihusu nini, mi nimelipia ili nipate matibabu naambiwa mtandao hakuna. Na kwanini kituo hicho kimoja kiwe natatizo la daima la mtandao. Ikiwa hapo mjini kabisa. Kwa kweli Mh waziri kuna tatizo la uzembe kwenye baadhi ya taasisi za serikali, yaani mhudumu akijisikia tu kachoka kujaza form za bima anakwambia hakuna mtandao.

Mh waziri naomba imulikwe hospitari ya Kizuiani kitengo cha bima ya afya kuna tatizo kwa wahudumu.

Kuhusu suala la mtandao naomba serikali iangalie uwezekano wa mgonjwa kupewa matibabu hata kama hakuna mtandao ili kuepusha vifo visivyo vya lazima. Hili tatizo la mda mrefu la kukosekana mtandao kizuiani linarudisha nyuma jitahada za serikali za kuhahkikisha kila mwananchi anapta bima ya afya kwani wananchi wanaona kama kuwa na bima ni manyanaso.

Bima ya afya ni mkombozi kwa sisi wananchi ila mtatizo kama haya ya kizuani tunaomba wahusika waonywe ili wananchi tuweze kupata huduma bora kama tulivyoahidiwa na seriakli yetu
Mwananchi mtiifu
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
4,582
2,000
Hivi wale waliokwapua Billion 3 kutoka kwenye mfuko huu mwaka jana wamesharudisha? Yaani Isee waliokwapua hizi hela huwa nawatamani kuliko hela zenyewe! Nawatamani kuliko hiyo Billion 3 waliyokwapua
 

ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
1,130
2,000
Kwa kuongezea;
1 . Namba ya simu ya msaada kwa wateja (Hotline/HelpDesk)ya NHIF imekuwa haisaidii kabisa...muda wote iko busy unaambiwa usubiri yaani kuanzia asubuhi had jioni unapata ujumbe ule ule.Kuna kipindi walikuwa hawafanyi kazi weekend ,unless kama wamerekebisha karibuni

2. Hakuna back up plan ya kupata matibabu kwa mfano kadi umeisahau na umeumwa ghafla unaweza ukafia mapokezi ingawa inawezekana wanazo rekodi zako/file na huwa unatibiwa hapo hapo mara nyingi.Wao wanachodai ni kadi tu kama robots

3. Hakuna plan B kama mtandao unasumbua..yaani wanakutolea macho kama vile unatibiwa bure

4. Mchakato wa kupata barua/kibali cha muda ni balaa tupu....Kama umeibiwa/umeshahau/umepoteza kadi halafu ukaumwa ni balaa tupu .Watakwambia ukafuatilie barua/kibali cha muda mfupi...yaani hii kuipata ndiyo balaa kabisa ...mchakato wake ni mgumu balaa na wala hawajali kama una hali gani.

Kwa mfano niliachaga kadi Dar nikaugua nikawa nimezidiwa nikiwa Dodoma...nikaambiwa nifuatilie barua/kibali cha muda toka Town centre mpaka zilipo ofisi za NHIF kuna kaumbali na nikakuta kuna foleni ya maana.

Ule mchakato na masahibu niliyokutana nayo pale NHIF Dodoma ilibidi nikae chini niombe Mungu tu (manake nilikuwa sina hiyo hela) mpaka niliporudi Dar nikiwa hoi nikatibiwa na kadi yangu.

Mh Waziri ,hivi na haya nayo mpaka mkuu wa nchi aingilie kati?...au tum beep atupigie?
 
Top Bottom