Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 10,593
- 20,964
Kwako Mh Mwigulu Nchemba najua upo humu na huwa unapita pale upatapo nafasi.
Kama ulivyosikia mwingine kauwawa tena leo huko Kibiti kabla hata maumivu ya mauaji ya juzi hayajapoa. Toka haya mauaji yaanze naamini watu zaidi ya 40 wameuwawa (Sina idadi kamili), hawa ni wazazi, walezi, wame/wake na ndugu zetu.
Mtu hahitaji kuwa forensic expert kuelewa pattern ya mauji yaendeleayo huko Kibiti: wanauwawa viongozi, wanaume, watu wazima huku wakina Mama wakiachwa wajane na watoto yatima. Aidha mauji karibu yote Kama inavyoripotiwa yanatokea Usiku. Swali ni je kwanini polisi chini ya wizara yako hawaongezi ulinzi hasa mida ya Usiku?
Njia ya kuongea na wazee wa Kibiti kila baada ya tukio ni dhahiri imefeli. Kama hamuwezi kuwapa ulinzi basi msifanye nao mikutano kuwaonyesha sura zao ili wabaya wao wawaue ifikapo usiku.
Lakini pia kila siku tunasikia polisi wameuwa majambazi wanaodhaniwa kuwa ndo wahusika wa Kibiti, Police watapata wapi inside info kama wanaua wahusika? Haya mauji ya polisi yanatia doa uwezo na mafunzo yao achilia mbali intelegensia ya vyombo vya usalama ambao inaonekana hawana clue hadi leo
Ni wakati sasa viongozi muwajibike kwa kushindwa kutimiza wajibu wenu. Sasa kila nikisikia jina Lyanga mkuu wa polisi Kibiti japo simfahamu sura najua tayari kuna ndugu yetu huko ameshakatishwa uhai. Kuachia ngazi ni uzalendo wa Hali ya juu unapoona mwenyewe unapwaya. Mjitathimini
Kibiti salama au muwajibike.