Barua ya wazi kwa WAZIRI MKUU wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa WAZIRI MKUU wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mansakankanmusa, Aug 14, 2012.

 1. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  Mh. Waziri mkuu kwanza shikamoo!
  Mh. Waziri mkuu,Kwa heshima na taadhima naleta barua hii na uhalisia wa tatizo, kunyimwaa vyeti UDOM,


  Ikumbukwe kwamba sio wanafunzi wote wenye makosa, na hatua ya kunyimwa vyeti zipo sababu nyingine na si kukataa
  kusaini kulipiwa ada, tafadhali sana tupewe vyeti vyetu, hatuna makosa yoyote yale,
  labda nitoe sababu kwa nini zipo list za ada ambazo hatujaweka sahihi.

  1. Kukosekana kwa baadhi ya hizo HESLB name list za kusaini ada, ambazo hazikuonekana wakati tukiwa chuoni
  2. Najua Waalimu na Watawala wetu wameudhiwa na mienendo ya baadhi yetu na kuchukizwa na wanachuo, hii kwa haraka haraka utadhani ni namna ya kutuadhibu.

  Tunaomba watusamehe sana, walimu ni wazazi wetu na watawala ni wazazi wetu pia. Sisi tukiwa chuoni ni kama WANA WENU hatukustahili ADHABU HII waliosababisha matatizo ni hakika wengi wetu hatukuunga mkono na ndio maana tuliruhusiwa kurejea kufanya mitihani. Tunawaomba walimu wetu, watumishi watusamehe.

  3. Wengine wetu hatukupata wasaa hata wa kuomba kusaini wakati na hata baada ya fujo, na hata hivyo tulikuwa wengi sana ambao tunatoka shule za kata, hili ni pigo kubwa kwetu.

  Naomba kuwasilisha.

  Asante
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe umemaliza chuo kikuu na hii ndiyo barua unamwandikia Waziri Mkuu??Watanznia bado tuna safari ndefu sana huyu ni mhitimu wa ngazi ya chuo kikuu anaaandika barua kwa Waziri Mkuu wa nchi!!
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseeee baba yangu shukuru umepata elimu kajiajiri mwenyewe si lazima uwe na cheti ili uwe mkulima au mfanyabiashara watachukuwa kila kitu ila si akili ya kichwani ukitaka cheti ngoja 2015 chadema ishike dola

  karibu mbege
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  dogo kajipange upya kuandika barua yenye hadhi yako
  waziri mkuu anapitia humu
  elezea vizuri kiini cha tatizo,kwaninin mmenyimwa na mmechukua hatua gani
  jieleze wewe ulikuwa unasoma kozi gani nk
  zingatia kanuni za uandishi wa barua
   
 5. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  sawa mkuu weka ya kwako hapo, na ikiwezekana tafsiri kwa ung'ng'e imwendee mh. waziri mkuu
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Kwani umeambiwa barua ziendazo serikalini zinaandikwa kwa lugha ya kikoloni??Jipange siyo kutokwa povu!
   
 7. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Pole kwa kuchelewa kupata cheti chako. Ila inaonekana unaomba cheti chako huku ukijitenga na wenzako kwa kusema sio wote wenye makosa! Cheti ni haki zenu na mnatakiwa mdai kwa sauti moja, hawa watawala wanatumia ujinga wa utengano wa watu ili waendelee na ubabe wao!
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi kweli wewe ni mwanafunzi umemaliza CHUO KIKUU au umemaliza CHOO KIKUU.
  Kwanza hujui hata barua inaandikwa je? Pili huwezi kuweka mawazo yako katika mtiririko mzuri unaoleweka. Nina mashaka sana na elimu yako.

  USHAURI wangu wa bure nenda haraka sana leo hii ukajipange, uandike barua yako vizuri ueleze tatizo lako vizuri. Kuna wabunge wengi wanapitia humu JF. Kama utakuwa umeeleza vizuri kiini cha tatizo lako. Kesho wabunge wanaweza kupata wasaa wa kumuuliza Mh. Pinda PM hilo swali lako katika kipindi cha maswali na majibu ya kwa papo kwa papo.

  kama uwezo wako ni mdogo tafuta wanafunzi wenzako m-draft vizuri hizi grievances zenu kama wasomi kweli wa Chuo kikuuu.
   
 9. YAGHAMBA

  YAGHAMBA JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ukiona ameboronga ujue ni matokeo ya CCM kuharibu elimu ya vijana wetu, nadhani Pinda atamwelewa kwani naye (Pinda) ni sehemu ya tatizo.
   
 10. Inno laka

  Inno laka JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 1,592
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Ninamashaka kidogo na elimu yako hyo mjomba hata mtoto wa darasa la nne anaandika barua nzuuri ambayo hata msomaji inampendeza.
   
 11. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  umanataizo mkuu, draft kwa niaba. Tatizo ni misongamano na migogoro na chuo mfano migomo, na wingi wa wanafunzi, kukosekana majina ya baadhi yetu/kukosekana vitabu kwa wakati. mathalani cha 3rd yr ndio kwanza kipo sasa, na wakati huu tumeshaondoka chuo. seuze vya semistas? WAZIRI WA ELIMU ASIWASIKILIZE UTAWALA wanatuundermine, nionavyo mimi kitambulisho cha mtihani kilichotolewa wkt wa udahili upya kilitosha sana kunipa cheti changu, Maana kilipita stage nyingi hadi kufanya mitihani. Ni hayo tu Mkuu

  mkuu unapoona kasoro rekebisha usiwakewake. ndio maaana ya JF
   
 12. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  bobuk umechemsha kiukweli wanafunzi wanasoma shule tofauti na background tofauti na hii inachangia sana katika kutoa product za wasomi..elimu ya tanzania inatokana na kufaulu masomo unaweza ukakuta mtu mkali darasani ila masuala ya ofisi kuandika barua na proposal hajui ila sio kuwa hajasoma bali ni elimu aliyopitishwa hajakutana na hilo suala nakuakikishia..sio wewe ulisoma mjini mnaenda kutembelea hadi mjengo mweupe wa magogoni kama sehemu ya study tour halafu ujilinganishe na mwenzako wa namtumbo ntimbwilimbwi...mrekebishe kama wewe ni mtaaramu.mpe just skeleton nyama ataweka yeye.
   
 13. The Son

  The Son JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asilaumiwe sana, asaidiwe maana ameeleza wazi kuwa alisoma shule ya kata.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mi nlidhani labda kuna jambo la maana saaaaaaana kumbe hujapewa matokeo,andika barua kwa uongozi wa chuo,pinda hana msaada katika hili kwa sio utaratibu waziri mkuu kutoa vyeti au kutumia madaraka yake kulazimisha ukiukaji wa taratibu za nchi hasa kusimamia nidhamu na uadilifu katika taasisi za elimu hapa nchini.
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  1. Kukosekana kwa baadhi ya hizo HESLB name list za kusaini ada, ambazo hazikuonekana wakati tukiwa chuoni
  2. Najua Waalimu na Watawala wetu wameudhiwa na mienendo ya baadhi yetu na kuchukizwa na wanachuo, hii kwa haraka haraka utadhani ni namna ya kutuadhibu.

  [/QUOTE]

  kumbe jibu unalo hapo kwenye red,unalia lia nini sasa????ujirekebishe na uache KUTUMIWA KAMA MPIRA WA KIUME
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Dogo wewe ndio wale vinara wa migomo?
   
 17. F

  FATHER OF HISTORY JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 545
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 60


  We bwana mdogo kama ndiyo uandishi wenyewe wa barua kwa WAZIRI wako Mkuu ni huo ni heri hata hicho cheti usipate maana hakitakusaidia chochote huko mtaani.Hivi mwalimu wako wa lugha kule Primari hakuku namna barua rasimi zinavyokuwa?Hivi huko sekonadari hamkuwa na mwalimu wa kufundisha barua? UDOM nako somo la communication skills uliingiamitini?au ndo nyie mnaacha kusoma mnakula pombe tu.Hamna point hapo kajipange upya ueleweke,maana ulicho kiandika hapa hakijulikani kama ni ombi,mapendekezo au facts,pia uache ubinafsi wa kujitenga kwa suala linalohusu maslahi ya wengi, what do you mean by saying sisi wengine hatuna makosa?
   
 18. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  sijawaandikia nynyiem nyinyi. Mnanilazimishe niseme niligoma?
   
 19. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Kwamaana hiyo kapitapita kimagumashi hadi chuo kikuu cha Dodoma??
   
Loading...