Barua ya wazi kwa waziri Mkuu Pinda

Mikael P Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,933
0
Wahenga wanasema kuuliza si ujinga na hakuna swali la kijinga ila kunaweza kuwa na jibu la kijinga. Mimi ninamwandikia waziri mkuu barua ya wazi ili kujua ukweli maswali yanayonisumbua. Barua yangu kwake ina swali moja la Msingi.

Swali langu ni moja tu kuwa kwa nini kunapotokea jambo au habari kubwa ambalo linaisumbua sana serikali basi kunaibuka habari au jambo jingine ambalo huwa linafunika lile jambo linaloisumbua Serikali?
Nina mifano mingi sana lakini nitatoa mifano michache sana ili kujenga hoja yangu vizuri na waziri mkuu anielewe.

1) Kuharibika kwa Miundo mbinu vs kuanguka kwa helikopta.
Majuzi mvua ilinyesha na kuharibu miundo mingi sana hasa ile miundo mbinu iliyotengenezwa chini ya Kiwango kutokana na uchakachuaji wa viongozi wa serikali. Baada ya hapo bara bara zikawa hazipitiki, watu wakalala maporini, hasira za wananchi waliokuwa wanalala njiani zilikuwa kubwa. Vyombo vyote vya habari viliandika habari hizo na vingine vikiilaumu serikali kwa mpangilio mbaya wa jijj na madaraja dhaifu. Ghafla tukaambiwa helikopta iliyokuwa imembeba makamu wa Rais Dr Bilal,magufuli na mkuu wa Mkoa wa Dsm imeanguka. Mjadala ukahama, ukawa ni kuwaonea huruma viongozi wa chama chetu tawala na siyo kuwalaumu kwa miundo mbinu dhaifu. Je, ni kweli ile helikopta ilianguka na hakuumia mtu wala helikopta yenyewe au helikopta iliangushwa kwa makusudi kwenye magazeti na vyombo vya habari ili kuiokoa chama chetu tawala dhidi ya hasira za wananchi??


2) Kuchinja wanyama Buchani vs Bunge kutooneshwa.
Kulikuwa na mvutano mkali sana kati ya viongozi wa dini mbali mbali kuhusu uchinjaji wa Wanyama Buchani. Ni kipindi hicho hicho tukasikia mchungaji amechinjwa huko Mwanza. Mjadala ukawa mkali dhidi ya udhaifu wa Serikali kushindwa kulitatua hilo. Ghafla baada ya siku mbili tukasikia Bunge halitaoneshwa live kuanzia sasa. Mjadala wote wa nani wa kuchinja na sakata la Mchungaji likafunikwa na Bunge kutooneshwa. Swali ni kweli kulikuwa na dhamira ya kutokuonesha Bunge au lengo lilikuwa ni kufuta mjadala wa kuchinjwa kwa Mchungaji kule Mwanza ili kuokoa chama chetu tawala kisichukiwe kwa kushindwa kutatua mgogoro ule hasa baada ya Steven Wasira kulikoroga kule Mwanza?


3) Muundo wa Muungano vs matusi.
Majuzi kulikuwa na Bunge la katiba ambako mjadala wa Serikali tatu uliibuka na wenye kutetea serikali tatu wakaonekana kuwa na hoja nzito dhidi ya msimamo wa Serikali, wa serikali mbili. Ghafla Bungeni yakaibuka matusi na mashambulizi binafsi. Mjadala Bungeni ukahama kutoka Muundo wa Muungano hadi kuwa matusi Bungeni. wananchi wakaanza kujadili matusi na kuwarushia lawama wabunge. Swali langu kwa PINDA,ni kweli kwamba makachero walipenyeza lugha ya kuudhi Bungeni ili kuhamisha mjadala kutoka muundo wa Muungano kwenda kujadili lugha hizo na matusi?


4) Mikutano ya Chadema vs Vifo.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 Chadema walianza operesheni zao. Mwitikio wa wananchi ukawa mkubwa sana kwenye mikutano yao iliyoanza na kuisha kwa amani huko kanda ya ziwa. Chadema wakafanikiwa kuibua mjadala kwenye vyombo vya habari ya kuwa ni chama kinachokubalika. Ghafla story ikabadilika walipokuja Mikoa ya Morogoro, Iringa, Singida nk. mikutano yao ilianza kukumbwa na matukio ya vifo yaliyoihusisha jeshi la Polisi. Mjadala ukahama kutoka umaarufu wa chadema na kuwa jinsi ilivyohatari kuhudhuria mikutano ya Chadema. Chadema waliomba serikali iunde tume ya kimakama ili kuchunguza vifo hivyo, serikali ikawakatalia. Swai langu, je, ni kweli kwamba jambo hili lilipangwa ili kuharibu taswira ya Chadema na kubadilisha mjadala wa kukubalika kwa Chadema na kuwa chadema ni mbaya??


5 ) Babu wa Loliondo vs Sheria ya kununua vitu chakavu ya Richmond/Dowans / Madai ya katiba mpya
Watu wengi hawajui kuwa wakati wa Sakata la Babu wa Loliondo Serikali ilibadilisha Sheria ili kununua vitu chakavu wakati huo ikilengwa mitambo ya Richmond na dada yake Dowans. Na pia kulikuwa na madai ya Katiba mpya. Ghafla watu wote kupitia vyombo vya habari tulihamishwa kujadili sakata la Loliondo. Swali, Je, ni kweli Babu wa Loliondo aliundwa na vyombo vya habari ili kuruhusu Serikali kubadili sheria ya ununuzi wa mitambo chakavu au ni kweli babu alikuwa na umaarufu wa kiwango kile? Kwa nini TBC walitumia muda mwingi kumpamba ??


6) Muungano vs Dengue.
Mjadala wa Muungano uliopoonekana kupamba moto sana ghafla ikaibuka homa ya Dengue na kufuta ama kupunguza mjadala wa Muungano. Dengue kweli ni tatizo lakini si tatizo kwa kiwango tunachoambiwa kwa sababu idadi ya watu waliokufa kwa Dengue haifikii hata robo ya idadi ya watu wanaokufa kwa malaria kwa siku. Swali Hivi Dengue ni tishio kivile au lengo lake ni kufuta mjadala wa Muungano uliokuwa hatari kwa chama chetu jhasa hoja za Tundu Lissu??

NB

Bado najiuliza, ni kwa nini Lema alivuliwa Ubunge siku chache sana baada ya Nasari kuukwaa ubunge? Kinachonisumbua Zaidi ni pale mahakama ya Rufaa iliposema kuwa hukumu ya kumvua Lema ubunge kule Arusha ni hukumu ya hovyo kabisa na inayoiaibisha mahakama. Swali ni kwa nini?? Je, lengo ilikuwa kuhamisha mjadala wa furaha ya chadema au ni kweli yule jaji alighaflika akamvua Lema ubunge kimakosa?Ni swali la msingi ni moja tu kwa waziri mkuu pinda, Kwa nini mijadala inahama ghafla pale ambapo serikali imebanwa? Je, waandishi wa habari wanajua kuwa habari nyingine huwa wanatengenezewa makusudi kwa malengo fulani??

Nawasilisha.
 

Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
0
Magamba daima wana mbinu nyingi sana za kuzima mambo lakini dawa yao inakuja 2015.. nayo itakuwa chungu kama hii hapa:
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Mikael P Aweda,unadhani atakujibu?Ngoja kwanza aki-retire ataweza kukujibu,lakini kwa sasa tumbo lake bado linahitaji chakula.Siumeona hata kwa Sumaye?Aliongea mengi baada ya kuachia madaraka,lakini kabla ya hapo yote yalikuwa sawia.Hivyo basi usitegemee jibu hapo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom