Barua ya wazi kwa Watanzania: Tuibadirishe gesi asilia kuwa Petroli

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Habarini za mihangaiko ndugu Watanzania.

Gesi asilia ni malighafi inayoweza kutumika kuzalisha petroli.

Ndugu zangu biashara ya mafuta ya petroli ni biashara yenye faida sana.

Kama tungejitahidi kutafuta mtaji tujenge kiwanda kimoja cha kuibadirisha gesi asilia kuwa mafuta ya petroli hakika tungeokoa fedha nyingi ambazo huwa tunazitumia kuagiza mafuta haya muhimu nje ya nchi.

Formula za kuibadirisha gesi asilia tunazo na tunazijua na tunajua ni biashara yenye faida kwanini tusijiingize huko.

Kwanini pesa ya kujengea vitua vya kujaza hiyo gesi tusizitumie kujenga viwanda vya kuibadirisha kuwa petroli biashara ambayo inafaida ya haraka?

Ndugu zangu uwezo tunao ila ushirikiano ni mdogo wataalamu tupo ila hatupewi ushirikiano wa kutoa michango yetu.

Pia kuna hii biashara ya mbolea, kwa hii gesi tuliyonayo hatukua na haja ya kuendelea kuagiza mbolea nje ya nchi tena kwasababu malighafi inayotumika kuzalisha mbolea kwenye viwanda vyote duniani ni gesi asilia.

Wizara ya kilimo mlitakiwa kuwa kipaumbele kuhakikisha mnastop kuagiza mbolea kutoka mataifa ya nje, mlitakiwa kutafuta mwekezaji ajenge kiwanda cha mbolea Mtwala huko kianze kufanya kazi kabla hata mwaka 2025 haujaisha.

Biashara ya mbolea ni biashara yenye faida, wanunuzi ni hawa hawa watanzania uzuri hata watu wa hali ya chini ni wanunuzi wa mbolea kwaajili ya kilimo.
 
Point yako ya kwanza.

Me ninavyodhania kubadirisha natural gesi kuja kua petroli ni gharama sana ndio maana wanakwepa na sidhani kama kuna nchi inafanya ivyo zaidi ya Lab experiment.

Ni sawa na mtu aseme DAWASA si wafanye reverse-osmosis watoe chumvi bahari ya Indi watu tupate maji. Lakini kupata lita moja itakua ni gharama zaidi bora wafuate tu uko Ruvu. Sijui kama ma right ila.
 
Point yako ya kwanza.

Me ninavyodhania kubadirisha natural gesi kuja kua petroli ni gharama sana ndio maana wanakwepa na sidhani kama kuna nchi inafanya ivyo zaidi ya Lab experiment. Ni sawa na mtu aseme DAWASA si wafanye reverse-osmosis watoe chumvi bahari ya Indi watu tupate maji. Lakini kupata lita moja itakua ni gharama zaidi bora wafuate tu uko Ruvu. Sijui kama ma right ila.
Kuna nchi zinafanya hivyo mimi nina data zote mkuu. Ukiona nimeandika kitu ujue nimekifanyia utafiti.

Nchi ambazo hazifanyi hicho kitu ni zile ambazo zina mafuta tayari. Lakini gharama za kuibadirisha hiyo gesi kuwa petroli ni sawa na gharama za kuyasafisha mafuta crude mpaka kupata hiyo petroli. Kuipata petroli wanapitia hatua nyingi sana.
 
kuna nchi zinafanya hivyo mimi ninadata zote mkuu. Ukiona nimeandika kitu ujue nimekifanyia utafiti.

Nchi ambazo hazifanyi hicho kitu ni side ambazo zina mafuta tayari. Lakini gharama za kuibadirisha hiyo gesi kuwa petroli ni sawa na gharama za kuyasafisha mafuta crude mpaka kupata hiyo petroli. Kuipata petroli wanapitia hatua nyingi sana.
Mkuu kasheshe bado iko in economic aspect ya process nzima. Kuna nchi kadhaa wanajaribu but hawajafika popote kumake any dent ukilinganisha na kusafisha crude.

Na sidhani kama gharama ya kusafisha crude au process ni ndefu kuliko hiyo ya gas to liquid. Angalia mlolongo wa gas to liquid linganisha na crude to liquid, hii technology bado sana for large-scale.

Gas-to liquid.png
 
Chama Cha Mazezeta wanajua fika kwamba nchi zote zenye viwanda viliendelea baada ya kuwa na madini ya chuma.

Tunahubiri habari ya viwanda huku chuma cha Liganga na Mchuchuma kukiendelea tu kuwa mapori badala ya machimbo.

Gesi tumesema sio kipaumbele chetu ndio maana hamna kinachoendelezwa, hata Wanorway wameamua kuachana na utopolo wa Chama Cha Mazezeta.
 
Mkuu kasheshe bado iko in economic aspect ya process nzima. Kuna nchi kadhaa wanajaribu but hawajafika popote kumake any dent ukilinganisha na kusafisha crude. Na sidhani kama gharama ya kusafisha crude au process ni ndefu kuliko hiyo ya gas to liquid. Angalia mlolongo wa gas to liquid linganisha na crude to liquid, hii technology bado sana for large-scale.
Hiyo root uliyopitia kutengeneza gasoline mbona ni ndefu sana.

Kwanza kabisa ondoa hiyo root ya kuprocess kwasababu tutanunua gesi ambayo tayari imesha be processed baada ya hapo tutaibadirisha kuwa Methanol, tukiipata methanol moja kwa moja tutaibadirusha petroli. Haina haja ya hizo process zote ulizozionyesha hapo.

Tutatumia advanced processes.

Kwani ninavyo elewa haya mambo gharama zitakua sawa na zile tunazotumia kuzalisha petroli kutoka kwenye crude. Kwasababu hata hiyo cracking uliyoiweka hapo na kwenye kuzalisha petroli inatumika kwasababu petroli tunaipatia kwenye naphtha ambayo ina octane number ndogo sana. Ili kuingozea octane number ndio hapo lazima uingize kwenye unit zingine kama vile catalytic reformer n.k.
 
Mkuu mawazo yako tumeyasikia na tutayafanyia kazi, ila kwasasa acha kwanza tuendelee kujenga madaraja.
 
Back
Top Bottom