Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,141
- 2,267
Ndugu wana JF, Ndugu Watanzania wenzangu, mabibi na mabwana, vijana na wazee, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha uchaguzi huu mkuu. Shukurani za pekee ziwaendee viongozi wa JF, Wanachama wa JF, Vyama vyote vya siasa, wagombea wote toka udiwani mpaka urais.
Uchaguzi umekwisha, na jana tu tulikuwa tumegawanyika katika makundi, kama wana NCCR-Mageuzi, TLP, CHADEMA, CUF, CCM na kadhalika, Lakini leo sisi wote ni Watanzania. Watanzania kwa maana kusahau tofauti zetu za kivyama, kusahau majeraha ya kipindi cha kampeni na tudumishe ummoja ambao siku zote tumekuwa nao. Tukutane tena hapa JF bila ya kukumbushana mambo ya kampeni, tukutane Magomeni, mwanza, Zanzibar n.k na tupeane mikono kama zamani. Hii ndio Demokrasia na ni muhimu kuelewa kuwa mara kampeni zinapoisha basi hatuendelei nazo tena mpaka 2015 katika kipindi kile cha miezi 3. Vinginevyo tutasahau suala la ujenzi wa Taifa, na tukaendelea kupiga kampeni kwa kipindi cha miaka 5.
Kabla ya kuedelea nafikiri ni vyema nieleze nini ninachoamini mimi. Ninaamini katika Demokrasia, Ninaamini kuwa Demokrasia yetu itakuja si kwa 'Revolution bali kwa Evolution', Ninaamini kuwa Demokrasia ni Process inayochukua muda mrefu sambamba na elimu ya wananchi, uchumi na ueleo. Ninaamini kuwa CCM itapoteza viti vya ubunge Chaguzi baada ya chaguzi na kamwe haitavidharau vyama vya siasa na Rais toka upinzani atapatikana pale wabunge wa upinzan watafikia 40% ya wabunge wote wa Tanzania.
Demokrasia ni uchaguzi wa watanzania, na hatutarudi nyuma kamwe. Kuna usemi usemao pindi ukishaionja Demokrasia basi hata kwa bunduki hakuna kiongozi anayeweza kuwarudisha wananchi nyuma. Lakini siamini eti Demokrasia yetu ijengwe na watu au mataifa toka nje, hili halitowezekana na kama likitokea basi Demokrasia hiyo itakuwa sio halisia. Kwa hiyo kwa wale wanaotegemea nchi za Magharibi au Marekani ndio wajuzi wa kujenga Demikrasia yetu, wanajidanganya kwani hilo halitatokea ispokuwa vurugu. Kwa hiyo napenda kutoa ujumbe kwa wale wanaopenda kukimbilia nje ya nchi na kulalama dosari zilizojitokeza katika uchaguzi eti ndio huko kuna majibu, wanafanya kosa kubwa sana. Tuna nafasi ya kukutana wenyewe na tuelezane dosari kama vile walivyofanya Zanzibar kati ya CCM na CUF. Na tumehakikisha kuwa inawezekana! Ni vigumu kumaliza dosari katika nchi masikini kama yetu ambayo Teknolojia, ueleo, elimu na miundo mbinu bado ipo katika zama za ujima.
Watanzania ni watu wanaopenda umoja na amani. Kwa maana hiyo Chama chochote kitachotaka kuingia madarakani kwa kutengua moja kati ya hayo, chama hicho machoni mwa watanzania ni kama nguvu ya soda. Kitavuma kwa muda mfupi na kitatokomea pole pole na pengine hata kufa. Ikiwa chama kina mlengo wa Kikabila, dini, au rangi basi nacho kitakufa ama kitashinda ubunge tu katika maeneo yale ambayo walengwa wako wengi. Lakini kamwe hakitashinda urais! Kinyume chake, vyama hivyo vitaipa nguvu CCM iendelee kushinda na kuwa maarufu kwa miaka dahli. Tusaidiane kuvionya vyama au watu waliopo ndani ya vyama hivyo.
Pamoja na kulingana na nchi nyingi za Afrika na Afrika mashariki, lakini ukuaji wa Demokrasia ya Tanzania hautalingana na nchi yeyote ya Afrika. Kuna wanaopenda kulinganisha na Kenya kwa yale yaliyowasibu katika uchaguzi uliopita, lakini napenda kuwaeleza watanzania kuwa huko sisi hatutafika kwa vile tupo katika mazingira tofauti. Demokrasia ya Tanzania itakuzwa na kuimarishwa kupitia Bunge na sio mpaka chama cha upinzani kipate urais.
Mwisho napenda kuwashukuru tena Viongozi wa JF, na nina wosia mkubwa kwa wana JF na waandishi wote wa habari. Sekta yenu ni muhimu sana katika kuigeuza jamii kwa mazuri au mabaya, hivyo ni muhimu sana kwenu kufuata maadili ya uandishi. Hii ikiwa na pamoja na kutoandika kiushabiki au upendeleo wa chama fulani maadam unakipenda.
Mungu ibariki Tanzania, kibariki chama tawala kiweze kutuongoza vyema mpaka 2015.