BARUA ya wazi kwa wabunge wa UPINZANI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BARUA ya wazi kwa wabunge wa UPINZANI!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ubungoubungo, Nov 7, 2010.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kutupatia wabunge wa kutosha wa upinzani bungeni katika term hii. watu wenye uwezo mzuri na uaminifu kama Dr slaa ni wengi mno mwaka huu hata kama slaa mwenyewe hatakuwepo bungeni. watu kama kina mbowe, mnyika, zito, hata mrema tu na wana cuf wengi, ni tunu kwa maendeleo ya tz na accountability ya selikali yetu tz.

  bado imani yangu ni kwamba, Mbunge mmoja wa Chadema au cuf, ni sawa na wabunge zaidi ya hamsini wa CCM, na hoja, kujiamini, kusacrifice maisha yake kwaajili ya taifa lake, kupambana na mafisadi etc wanao uwezo mkubwa sana zaidi ya mara hamsini ukilinganisha na wabunge wa ccm ambao wengi wao ni wanafiki kabisa. Mungu atawahukumu!

  Ninachowaomba wabunge wa CHADEMA,CUF NCCR etc, Tafadhali, tafadhali, jipangeni vilivyo, jueni kwamba nyie ndo wenye upeo mkubwa na ndio mnaotazamwa na watz wengi kama ndo wasemaji mtakaoibana network ya ccm na kusababisha maendeleo ya nchi yetu. hilo halina ubishi. KAMA TULIVYOWAAMINI, TUNAOMBA MTUTENDEE HAKI KWA KUWA WAMOJA, KWA KUFANYA KAZI KWA UAMINIFU NA KUJITOA MHANGA KAMA ALIVYOKUWA AMEFANYA SLAA, mkijua ya kuwa CCM wako tayari hata wasifanya maendeleo ya nchi badala yake watumie muda wote huo kuunyong'onyeza upinzani ili wananchi waamini kuwa, kuchagua wapinzani hakuleti maendeleo.

  Tunaomba mprove yourselves kwamba chama cha upinzani kikipita katika jimbo etc au mbunge wa upinzani akipita, maendeleo yanakuja na network ya ccm inabanwa vilivyo. Macho ya watz yako kwenu, na hii itadhihirishwa 2015 pale wananchi watakapoanza kufanya auditing ya mlichofanya bungeni. nyie ndo mliopewa rungu la kuifanya ccm ianguke au ije iendelee kukaa madarakani 2015, na, ccm wamesema watajipanga ili waendelee kukaa madarakani, jueni wana mbinu nyingi na TUNAOMBA MSILALE.


  TAFADHALI, MSITUANGUSHE, TAFADHALI, MSITUANGUSHE, TAFADHALI MSITUANGUSHEEEEEEEEEEEEE! TUNAWAAMINI, TUMEWAKOPESHA KURA, TUNAWADAI MAENDELEO. ASENTE.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Thank you very much. Very well said, tuwaombee mungu pia wabunge wetu wa upinzani kwa kuwa ccm wako tayari hata kutumia kiasi chochote cha fedha kuugawa upinzani, na cha kuogopa zaidi kama watawachukua wabunge wa CUF kama muendelezo wa muafaka wa zenj si ulimwona Lipumba siku ya matokeo? Let us expect a lot of unexpected from upinzani hii ndiyo Tanzania bana.
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  si unaona hata huu wa uspeaker to walivyokuja juu, wanataka speaker ambaye atakuwa anasympathise na mafisadi, ili wale hii nchi vizuri.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono na wasikubali kununuliwa na MAFISADi, wajue chama cha mafisadi kipo tayali kutumia gharama yeyote kurejesha majimbo yao! MSIKUBALI!!! mmenisikia::
  silinde
  Mr 2
  Mdee
  Mnyika
  Vijana nyie tunawategemea kuwakilisha zaidi na zaidi!
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kutokuwepo kwa dr.slaa bungeni, nafikiri bwana mbowe ataziba ufa huo. bila jazba,tujenge hoja tuwaaibishe mafisadi. mjipange vizuri, ushindi ni wetu.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Atakaye kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni aendelee kuwa na mawasiliano na Slaa kwa karibu ili kile chanzo chetu cha habari za mafisadi na wanafanya nini kiendelee kutumiwa vizuri ili kunusuru Taifa na ushenzi wao dhidi ya rasilimali zetu. Hata kama serikali hii haiwachukulii hatua sahihi mafisadi,kuwaanika hadharani bila woga kunasaidia kuwapunguza makali kiasi fulani.
   
 7. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa, hakuna kulala. Ule wimbo mzuri, Tuwamwage , tuwamwage, mafisadi,uendelezwe bungeni kwa stahili ya hoja zenye mantiki. hakuna jazba, mnapokezana. Na sometime Speaker atakuwa anabana, lakini tafuteni mbini ya kujipanga. Mnyika akirusha kombora, mdee unaliendeleza bila kuvunja kanuni.
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waweke tahadhari kwa mamluki.
   
 9. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimefurahi KUMWONA TUNDU LISU MLE NDANI LEO. tulikuwa tunasubiri sana nafasi kama hizi zijitokeze hapa tz. Chadema wamejipanga sana, hata kama cuf hawatawaunga mkono kwasababu wanawaonea gere, chadema kwasasa inao wapiganaji wa kutosha watakao toa hoja zitakazo wafanya wananchi wakiunge mkono chama hicho mwaka 2015. kuna kina slaa mwengi sana mle. Mbowe mmoja ni sawa na ccm hamsini. Tundu lisu mmoja ni sawa na ccm hamsini. Mungu ibariki tz
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ubungoubungo tunachotaka ni wabunge wa upinzani kufanya kazi kwa maslahi ya watu wao na si kuungani ili mtu fulani afanye kazi na we 2015 useme tulikuwa wote kama ambavyo juzi kwenye kampeni kuna watu wanasema walikuw wapinga ufisadi wakati si kweli.

  Muungano si lazima kama mtu uko chama fulani na unaona uko mwenyewe na anza kufanya kazi si kulalamika tu.

  peoples power
   
Loading...