Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,495
- 51,090
Kwako Askofu Shoo, Pengo na Shehe Mkuu na wengineo
Bila shaka mnajua kinachoendelea nchini, Bila shaka mnatambua kilichotokea nchini kufuatia uharibifu wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Na mnajua jukumu lenu katika kukemea udhalimu na matendo yote yasiyo ya haki yanayoendelea nchini.
Hebu jiulizeni ni nini timing ya mkutano wenu huu na mkuu wa mkoa Dar es salaam, Jiulizeni ni kitu gani kipya kitakwenda kujadiliwa na mkuu huyu wakati ni takriban mwaka mmoja tu na miezi kadhaa mlikutana na Rais pale Ikulu. Jiulizeni serikali inataka nini this time around?
Ndugu viongozi wa dini, serikali inaweka kigingi mapema dhidi yenu ili msiwe UNITED na kuja na CONCENSUS moja ya kukemea Uovu, Uonevu na Udhalimu ilioufanya katika kuharibu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Serikali inachofanya leo ni kuwafanyia Charm offensive ili muone aibu kutoa kauli za kichungaji na mawaidha ya kukemea uvunjwaji wa wazi wa Haki za raia katika chaguzi.
Ndugu viongozi wa dini, Nyinyi ni Soft power yenye nguvu mno ambayo mamlaka haina, kwa hiyo ili kuidhibiti isitumike kwenye kuuamsha umma ili upate haki inajitahidi kuicontain kila mara inapoona inaharibu au inataka kuharibu.
Huu mkutano wenu ni aina ya Containment. Wanataka mkae kimya, msizungumze lolote.
Lakini nyinyi ni Wachunga ama wachungaji, Hamuwezi kuhimiza au kuhubiri amani kama hamhubiri haki, na wala hamziambii mamlaka zitende haki. Iwapo nyinyi mtajivua jukumu la kuwa mareferee wa haki baina ya sisi mnaotuchunga, basi tutataka wachungaji wengine na si lazima wawe nyinyi mnaovaa majoho makubwa huku mkila karamu katika meza za uonevu.
Leo hii kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zimeanza halafu ghafla bin vuup mnaitwa kukaa kuongea na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, anataka kuongea nini na nyinyi zaidi ya kufikisha maelekezo na ahadi nyingi kwenu kutoka katika mamlaka zilizomteua ili kuwafunga mdomo msiseme kitu?
Maana siku hizi Modus operendi ya serikali hii ni kujaribu kuyaita makundi yote yenye ushawishi kwenye jamii na kuyapa kila moja naweza kusema "Takrima" fulani ili kuyafunga mdomo au wakati mwingine kuyatumia tu kama ngazi za kisiasa ili Umma uhadaike kuwa mambo yanakwenda vizuri.
Ndivyo utawala huu ulivyowaita Ikulu mwaka uliopita ili kuwatuliza munkari basda ya nyaraka zile mfululizo, Ndivyo utawala huu ulivyowaita wafanyabiashara Ikulu ili kupotray sense ya kuwa unajali biashara za watu na hivyo kujivua lawama za kuharibu biashara nchini, au kukutana na wasanii na kuwapa pesa na
ndivyo utawala huu ulivyoita wasimamizi wa uchaguzi serikali za mitaa Ikulu yote hii ni kujaribu kuyavuta Makundi muhimu in favor ya bwana mkubwa!
Sasa viongozi wetu wa dini, Je mnabariki udhalimu na uonevu uliotendeka nchini. katika suala hili. la uchaguzi mkuu kisa eti mnapewa audience na mamlaka kisha mkakaa na kunywa na watawala wakawafanya mjifeel good kwa kuwasmbia maneno matamu matamu kuwa nyinyi ni watu muhimu sana na blah blah kibao?
Viongozi weti wa Dini acheni Kula kwenye Karamu za wanafiki na waharibifu bali SIMAMIENI HAKI, TIMIZENI WAJIBU WENU WA KUMSEMEA ANAYEONEWA BADALA YA KUWA UPANDE WA UDHALIMU